Warioba Tume yake inanipa mashaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba Tume yake inanipa mashaka

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Kakke, Oct 21, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  Na B. OLE,

  Baada ya kufuatilia kwa makini maoni na ya tume ya katiba inayoongozwa na Jaji Warioba kuhusu mchakato wa katiba mpya inayotegemewa ifikapo hapo mwaka 2014 ,nimepatwa na wasi wasi juu ya ukweli na lengo la wenzetu kuhusu lengo na hatma ya mchakato huu.

  Inaonekana kwamba haya maoni yanayotolewa hasa kwa upande wa Zanzibar na kupitia na vianzio mbali mbali ni geresha tu ya kuudanganya ulimwengu kwamba Tanzania ni Nchi ya demokrasia jambo ambalo sio kweli.

  Tanganyika haiko tayari kufuata matakwa ya Wazanzibar kwa kile wanacholilia cha kuwa na Zanzibar huru yenye Dola kamili. Hii imedhihirisha pale Warioba na timu yake walipotembelea na kutaka kupata maoni ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

  Wajumbe takribani wote ukiwacha wale akina minal-dhalimina walitaka kuona kwamba Zanzibar inajitegemea wenyewe kama dola huru lenye mamlaka kamili ndani na nje ya Nchi hoja ambayo Warioba na timu yake walikuwa wanaipinga wazi wazi ndani ya Baraza la Wawakilishi.

  Jaji Warioba yeye na Tume yake ilitumia sana muda kuwakatisha Wajumbe hasa pale waliupokuwa wakilizungumzia suala la kuwa na Mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar na zaidi walipokuwa wakidai Utaifa wa Mzanzibar,na kusema apewe maelezo kuhusu wale wajumbe wanaodai Muungano wa mkataba maana yake nini?

  Inashangaza kuona kwamba mtu kama Jaji Warioba kuwa haelewi kuhusu Muungano wa mkataba kama ule wa EU na mengine sio kweli,suala hapa ni kwamba Tanganyika wana ajenda yao kuhusu Zanzibar. Hawako tayari kuona Zanzibar inajikomboa kisiasa wa kiuchumi.

  Ilikuwa inaonekana wazi wazi kwamba kauli ya Muungano wa mkataba inawakera akina Warioba na tume yake huku akitishia kuvunjika kwa Muungano,kutokana na madai yanayotolewa na Wajumbe hao.

  Mimi nimuulize Jaji warioba kwa heshima na taadhima hivi Muungano ni Msaafu kwamba ukiupinga utakuwa huna salama kwa Mola wetu? Hakuna haja ya kuwatisha Wazanzibar kwa hilo. Zanzibar ilikuwepo tokea enzi na enzi na wala ilikuwa haitegemei Muungano.
  Lazima nyinyi kama tume mueleze kile ambacho Wazanzibar wanataka kwani hapa kila mtu anaangalia maslahi yake kama Taifa, ikiwa munahisi kwamba Wazanzibar wanachodai ni kero kwenu, kwa nini tusivunje huu Muungano kwa faida za pande zote mbili?

  Nahisi Jaji Warioba ni vyema kuziba ukuta kuliko kujenga ukuta, huko munakotaka kutupeleka sisi kama Wazanzibar tunasema kwa kinywa kipana kwamba hilo haliwezekani,Jamhuri ya watu Wazanzibar kwanza.
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Taja hasara unazopata wewe binafsi zinazosababishwa na muungano.
   
 3. MJENGA

  MJENGA JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2012
  Joined: Nov 18, 2012
  Messages: 577
  Likes Received: 275
  Trophy Points: 80
  Mizanzibar alwayz vichwa vya nazi. Hivi kisa mmeoza mibinti yenu Oman ndo mnakubali kununuliwa na maalshabab kwa hongo ya tende!? Kweli nyie mambugila kweli! Eti Muungano uvunjike, uvunjike kwani nini!! khaaa!!!!!!
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Nov 26, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Kakke,
  Wewe ni miongoni mwa waimba kwaya wasiojua tungo zake.
  Ni wajibu wa tume kufahamu kinachoongelewa, tume si makarani wa kukusanya habari wasizozijua.

  Ahmed Rajab,Seif Sharif, Jusa, Mansour kwa uchache wameshindwa kueleza nini maana ya muungano wa mkataba.
  Kwa taarifa yako huu tulio nao wa 1964 ni mkataba labda kama hujui wewe na Wazanzibar kama kawaida.
  Madai yenu siku zote si kurudi kwenye mambo 11 ya MKATABA 1964?

  Pili, uelewa wako kuhusu EU ni hafifu sana, unahitaji msaada mkubwa sana.

  Tatu ZNZ ijikomboe kiuchumi kwa lipi? Unaweza kusema Tanganyika inategemea nini kutoka ZNZ kiasi cha kuwashikilia?

  Nne, kama mnaona kuna tatizo la kujikomboa kiuchumi mbona mnashindwa kutumia njia ya maoni kusema vunja muungano. Neno vunja muungano limekuwa kama ''tusi'' kwani hakuna anayethubutu kulitamka.

  Tano, hivi hujui uchumi ndicho ZNZ inakitaka kuhusu mkataba, uswiss, ubelegiji, senegambia n.k.

  Sita, hiyo haki ya kuamua kuwa tuwe na ushirikiano ABC mnapewa na nani? Kwanini Tanganyika isiwe na haki hiyo?

  Go back to the drawing board! huna hoja! Sisi hatuimbi nyimbo za Ahmed kama mnavyoimba! tuna akili timamu.

  Wasalaam
   
 5. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by Stonetown (Kiongozi) // 27/11/2012 // Habari // 1 Comment

  [​IMG]
  Maoni leo asubuhi WELEZO: Waliotaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kuwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika ni 49; Waliotaka muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali Mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho ni 40; Waliotaka Serikali Moja ni 1; na ambao hawakufahamika ni 1.
  Maoni leo jioni MWANAKWEREKWE IJTIMAÂ’I: Waliotaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kuwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika ni 44; Waliotaka muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali Mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho ni 35; na ambao hawakufahamika ni 1.
  NYEPESI NYEPESI ZA LEO: Pamoja na maoni hayo, kuna matukio mawili yaliyojitokeza leo yanafaa ku-share na wengine.
  LA KWANZA: Hili limetokea asubuhi Welezo ambapo Mzee Warioba alikuja kujumuika na wana-Tume iliyopo Zanzibar. Mwana-Mkataba mmoja alihoji vipi Wazanzibari waendelee na mfumo uliopo wakati nafasi zote kubwa kubwa katika mihimili mbali mbali ya Dola zinashikwa na watu wa Tanganyika tu. Mzee Warioba kama kawaida yake huwa hawezi kustahamili mawazo yasiyokubaliana na yake, akamwambia hivi hajui Tume ya Katiba Makamu Mwenyekiti wake ni Mzanzibari? Mwana-Mkataba akamjibu hivi huyo Jaji Agostino Ramadhani hana sifa za kuwa Mwenyekiti na wewe ukawa chini yake? Mzee Warioba akagwaya. Kimya!
  LA PILI: Hili limetokea jioni Welezo. Mwana-Mkataba mmoja alipozungumzia Zanzibar kuwa na mamlaka kamili na Rais wa Zanzibar awe na hadhi kamili kama Mkuu wa Nchi ndani na nje. Mwenyekiti wa Timu iliyopo Zanzibar, Prof. Mwesiga Baregu akamwambia hivi sasa Rais Shein yupo Vietnam, kenda kama Rais. Mwana-Mkataba akamjibu kenda kama Rais lakini baada ya kupata kibali cha Waziri Benard Membe na kumuuliza na Rais wa nchi gani anayehitaji kibali cha Waziri ili apokelewe kama Rais? Prof. Baregu akabaki kimya!
   
 6. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,963
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Serikali tatu ndiyo suluhisha: ya Tanganyika, Unguja na Pemba, pia ya Muungano.
   
 7. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,932
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  Tatu za Nini?

  Muungano uvunjike! ... na kila mtu arudi kwenye nchi ya asili yake ... watakaobaki wachukue VISA

  Na Hatutaki Muungano wa Mkataba! - masuala ya mkataba tukutane East Africa Community

  Tunaitaka Jamhuri ya Tanganyika
   
 8. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #8
  Nov 27, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  mbona rahisi sana. mwambieni shein huko vietnama apeperushe bendera ya zanzibar,kwishney mnakuwa huru leo leo.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Nov 27, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,136
  Trophy Points: 280
  Kakke,

  ..hivi kinachowashinda wa-ZNZ kujitoa ktk muungano ni kitu gani??

  ..nyinyi jitoeni tu, maswali ya "muungano wa mkataba" yatategemea kudra za Mwenyezi MUNGU.

  ..hizi hoja za "tutaka mamlaka kamili halafu tuwe na muungano wa mkataba" ni kana kwamba kuna kitu mnachokihofia mkiwa na hayo madaraka kamili.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. kbm

  kbm JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4,963
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kwa Tanganyika hakuna wasiwasi, lakini awa ndugu zetu wapemba waliojazana bara nzima, kweli wakirudi kwao wataenea?
   
 11. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #11
  Nov 27, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,932
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 160
  kbm

  Kuhusu kama wataenea huko kwao au hawataenea hilo halituhusu ... wakishafika kwao ndio watajua kama wataenea au hawataenea ...Warudi tuu kwao .. sisi hatuwahitaji

  Warudi kwao wakajenge nchi yao ya Zanzibar ... kwa nini wanang'angania huku?! ..

  Na Muungano ukivunjika wale wasiokuwa na VIZA tutawachukulia kama wahamiaji haramu (kama wa Ethiopia na Somalia tunavyofanya) watarudishwa kwao! ... baada ya kutumikia kifungo Jela kwa kuishi nchini Tanganyika bila ya Kibali (VISA)

  Wanalazimisha mkataba?! - wa nini kwetu, hatuna shida nao wala hatuhutaki huo mkataba! - wakafanye mkataba na Kenya huko au Comoro ila sisi Tanganyika hatutaki mkataba nao.
   
 12. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #12
  Nov 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Huyu Warioba tangu tume ianze kazi zake keshafanya madudu mengi.Kikwete hana budi kuteua mtu mwengine haraka kuokoa kazi za tume.Vyenginevyo tume itakosa heshima katika majumuisho ya maoni itakayotoa mwishoni.
  Akimwonea haya au kumuogopa nahofia matokeo kama ya sensa ya mwaka huu.
   
 13. M

  Mandi JF-Expert Member

  #13
  Nov 27, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  natamani siku moja iwepo serekali ya jamhuri ya watu zanzibar na serikali ya jamhuri ya watu wa tanganyika.ndugu zanguni wabara kwanini neno tanganyika hatulipendi.inapelekea kutolipenda kwetu ndio wengi wetu tunakosea tunasema tanzania imepata uhuru 1961.what the hell!
   
 14. M

  Mandi JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  All togeza we have to say no union.hakuna kitu ninachokichukia duniani kama muungano watanganyika na zanzibar.1:unakero zisizomalizika,hadi zimepewa jina la kero za muungano.2:hakuna heshima kati ya nchi mbili zilizoungana ni kuzarauliana tu.tanganyika inajiona ina haki zaidi juu yamuungano sababu ina watu wasiopungua milioni 42 wakati zanzibar ina watu kidogo.1.2 mil.3.nyanzifa za juu za wizara ya muungano.mfano balozi wa nje.wazanzibar ni 3.waliobaki wote ni watanganyika.4.wazanzibar wanatawaliwa na katiba mbili ya zanzibar na ya muungano,jee inaingia akilini hii na tumeona wapi nchi moja kua na katiba mbili?wakati watanganyika wanaongozwa na katiba mmoja.5.watanganyika wamelifanya bunge la tanganyika kua la muungano na misaada inayoletwa nchini kwa serikali ya muungano inatumiwa na serikali ya tanganyika kupitia muungano,na wameifanya bendera ya tanganyika kuwa bendera yataifa.6.muungano huu,inawapa wazanzibar wachache nafasi nyeti ili kuulinda na kuwakandamiza wazanzibar wenyewe kwa wenyewe.mfano salmini amour komandoo ameambiwa aizinishe nafasi ya makamo wa rais tanzania asiwe rais wazanzibar amekubali na mwaka 1995 tumeliona hilo.7.ni muungano ambao imeinyima zanzibar kutokutambuliwa kimataifa kiasi yakwamba rais wazanzibar ni bora ya waziri wa tanganyika na tumeona hapo anapotaka kuondoka nchi hadi membe atoe baraka zake.it is tolaly foolis.i hate union forever.let tangaoyika go!!
   
 15. s

  salmar JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 782
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Si kwamba wazanzibari hawataki kujitenga wanataka leo leo ila viongozi wa ccm hawataki cuz watakosa u heshimiwa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Nov 27, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,136
  Trophy Points: 280
  salmar,

  ..sasa kama hamtaki kujitenga kwanini mtaka kuwe na "muungano wa mkataba"??

  ..mpaka sasa hivi hatujasikia kabisa habari ya kuuvunja muungano moja kwa moja.

  Mandi,

  ..kama hamtaki muungano timueni tu hakuna aliyewalazimisha.

  ..masuala ya Tanganyika kwamba itakuwepo au haitakuwepo tuachieni sisi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #17
  Nov 28, 2012
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hayo ni mawazo yako na si mabaya lakini inaonekana unayasema kama vile una hasira kutaka kuleta uhasma.
  Wewe hujui kwamba muungano ukivunjika mabadiliko yatakayotokea ni ya kawaida tu.Ambaye hataki huu muungano uvunjike na kuunda nongwa za wapemba ni mfumokristo Tanzania.Huyu ndiye peke yake ambaye atapata hasara lakini sisi wengine tutakuwa ndugu kama kawaida kama tulivyo na wenzetu wa Kenya na Uganda na Zambia na kadhalika.
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Nov 28, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,136
  Trophy Points: 280
  Ami,

  ..hivi kwanini hamuishi visingizio??

  ..uhasama wa nini haswa? kwa kitu gani ambacho Mtanganyika atakikosa ikiwa muungano utavunjika??

  ..Wapemba walioko Tanganyika watakuwa na uhuru wa kuchagua kubakia huku, au kurudi kwao.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Nov 28, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,670
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Na kinachowashinda Tanganyika kujitoa kwenye muungano ni nini? Au Tanganyika inautaka sana muungano kuliko Zanzibar inavyoutaka? Manake hata sisi Tanganyika tunaweza kujitoa vilevile.
   
 20. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #20
  Nov 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tume ina kazi pevu. Hii Tanganyika hii?
   
Loading...