Warioba,maneno haya ya Nyerere hata ungekesha serikali tatu ni ndoto za ali-nacha

Kwa nini tusivunje Muungano wa serikali mbili na kuwa na Muungano kamili, wa serikali moja? Raisi mmoja, akitokea Bara, Makamu wake anatokea Visiwani, Raisi akae vipindi maximum viwili (miaka 10), Kuwe na Mawaziri wakuu viongozi wawili kutoka kila upande, kusiwe na wabunge wa kuteuliwa, wawepo wabunge wa kuchaguliwa.
 
Mbona hata Mungu, watu hawamtii kwa mambo yote. Kama hatukuwezi kumtii Nyerere tuliye muona kwa macho tutawezaja kumtii Mung tusiyemuona. Asiyemtii Nyerere hata Mungu hawezi kumtii
Hivi nyie watu mna nn na huyo Nyerere? Yeye alikuwa Mungu?
 
Serikali tatu ni laana kwa watakaoibariki, dhambi hiyo itawapukutisha kama ambavyo mti hupukutisha majani wakati wa kiangazi.

Tulia ndugu yangu serikali tatu ni baraka kwa watakao ibariki.
Njoo kundini serikali 3 ipite.
 
Serikali tatu ni laana kwa watakaoibariki, dhambi hiyo itawapukutisha kama ambavyo mti hupukutisha majani wakati wa kiangazi.

Na walaaniwe CCM wote wenye kuunga mkono mfumo dharimu wa serikali mbili
 

Attachments

  • eee.jpg
    eee.jpg
    2.2 KB · Views: 79
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania" - Ukurasa wa 61.
1010332_678415008867133_1699515160_n.jpg


Mkuu kwa mwelekeo uliopo sasa hivi hilo la serikali moja lishazikwa siku nyingi, halitatokea kamwe labda tu yafanyike mapinduzi mengine Zanzibar. Kwa hiyo tuking'ang'ania serikali mbili tunamaanisha:
  1. Serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanzania (ambayo ndiyo Tanganyika, kwa hiyo muungano hapa ni geresha tu la kuwezesha wazanzibari kugeuza Tanganyika kuwa 'shamba la bibi', chetu chao lakini chao chao! Hiki ndicho kilichowachosha watanganyika)
  2. Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanganyika (hapa hakuna muungano)

Kwa hiyo serikali mbili ndizo zinazovunja na zitakazomalizia kabisa kuvunja muungano. Tungefanikisha vema muungano kama tungenuia kweli kuwa na serikali moja tu ya jamhuri ya muungano, lakini sheria iliyounda tume ya mabadiliko ya katiba iliweka masharti kuwa uwepo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar usiguswe, kwa hiyo suala la serikali moja automatically lisingewezwa kupendekezwa na tume.

Serikali moja ndiyo ingeufaa muungano zaidi, lakini kisheria imezuiliwa. Iliyobaki ni serikali tatu, kwamba hiyo ya tatu ndiyo inayoziunganisha hizo serikali mbili za nchi mbili. Hivi hamjiulizi muungano wa America (USA) una serikali ngapi? Na wana katiba moja tu (angalau najua kuna katiba moja ya USA, wanaojua zaidi wataniambia kama yale majimbo nayo yana katiba zao). Lakini tofauti ya wazi hapa ni kuwa Zanzibar imekataa kuwa jimbo, yenyewe ni nchi ndivyo katiba yake inavyosema, kwa hiyo suala la katiba moja kwa nchi mbili naona ugumu wake lakini tushachelewa. Sasa hivi tuangalie maslahi ya tanganyika kama wazanzibari wanavyoangalia ya kwao: Tunahitaji serikali ya Tanganyika. Na ili muungano uwepo, tutahitaji pia serikali ya Muungano.
 
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania" - Ukurasa wa 61.
1010332_678415008867133_1699515160_n.jpg


Huo ni msimamo wa CCM......msimamo wa wananchi ni serkali tatu au moja na sio mbili. Tutawaelewa CCM mkitimiza hiyo ndoto ya Nyerere ya seikali moja!
 
Nyerere kakamata akili za watu,watu wanafikra za nyerere kuliko hata kumjua Mungu.siku ya mwisho watu watalia na kusaga meno kwa kuona kila kitu alichofanya yule mzee kuwa sahihi.
 
Serikali tatu ni laana kwa watakaoibariki, dhambi hiyo itawapukutisha kama ambavyo mti hupukutisha majani wakati wa kiangazi.

acha upumbavu na kutofikiria mshenzi mkubwa utanipigisha bun,. Serik 2 ni mawazo ya wafu na wote walishakufa hatuna haja ya kuenzi kitu ambacho hatuoni faida yake
 
Ongeeni yote maamuzi yeenu sio msaafu wananchi hawataki hizo serikali mbili na wao ndio waliwaweka madarakani msisahau hilo
 
Mimi hawa jamaa wananichekesha sana, Linapofika suala la Muungano Nyerere anakuwa mungu, Ila kwenye Rushwa, Ufisadi na umasikini Nyerere ni Shetani.
Sio hilo to mkuu bali isome hiyo attachment vizuri alafu angalia hapo nilipo highlight na uniambie watu wana aina hiyo wamebakia wangapi ccm ukimtoa Mzee Warioba na wenzake wachache!? dda.jpg
 

Attachments

  • dd.jpg
    dd.jpg
    55 KB · Views: 26
Mimi hawa jamaa wananichekesha sana, Linapofika suala la Muungano Nyerere anakuwa mungu, Ila kwenye Rushwa, Ufisadi na umasikini Nyerere ni Shetani.

Full unafiki hawa jamaa. Siku za nyuma ulikuwa ukimtaja Nyerere na malengo yake ile Lumumba team ikiongozwa na Faiza Fox ilikuwa inamwaga matusi humu na kumkejeli Marehemu Nyerere mpaka basi. Mara eti ndiye kaleta umasikini mara hakujali hiki na kile basi mradi ni kejeli kwenda mbele. Hata mkulu akawa hamuiti baba wa Taifa bali mzee Nyerere.
Iweje leo kwenye muungano ambao watu wanautaka na mfumo ambao unatishia uhai wa chama kilichopo ki mbinu mbinu akumbukwe Nyerere na kutumia jina lake kujinasua?
Serikali moja ilishindikana miaka ya mwanzo ya muungano. Serikali mbili zimeshindikana kwa muda wa miaka 50 mpaka zimezua nchi mbili sasa ni wakati wa serikali tatu nchi mbili. Basi.
Kama hawana hoja na wanataka kulazimisha mambo wata ona yatakayo tokea.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Back
Top Bottom