Fede Masolwa
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 528
- 123
warioba anazidi kupanda chati siku hadi siku !
Mkuu chati sawa, usalama wake je? ndio la msingi hili kwanza.
warioba anazidi kupanda chati siku hadi siku !
ukweli ni kuwa warioba hakua convincing kabsa kama nilivyotarajia,ameshindwa hata kupangua hoja ya kuwa watu 17,000 waliotoa maoni ya serikali tatu wanakua vipi majority.Huyu mzee anajua sana aiseee
Kile kipande cha hotuba ya mwalimu itv kinachosema.TUNATAKA RAIS ANAYEWEZA KUISIMAMIA KATIBA NA KUILINDA ASIYEWEZA AKASIMAMIE SHAMBA LAKE KULE,mi naona kama anamsema ba riz.
Kuwaita Uvmajanga waje wajibu hoja za Warioba ni sawa na kumuita mkutano wa hadhara Joseph Kone aje ajibu tuhuma zake.Hao ni wahuni ni kichaka na pango la wanyang`anyi hawana umoja wala makao rasmi unategemea watokee upande gani?Wana jamvi kama kweli vijana wa uvccm wana hoja na data za kupangua mawe aliyo toa jaji warioba leo itv tuna wataka watokee hadharani wamjibu mzalendo wetu jaji warioba kada wa ccm nguli na mweledi tangu enzi za mwl nyerere;waje jf watoe majibu msimamo wa serikali mbili wanaupata wapi?kwa data zipi walizo kusanya?
Halafu warioba alipaswa kujiweka pembeni na huo ushabiki coz kama hayo yalikua maoni ya wananchi anahangaika nini sasa? nani kamtuma awasemee? kazi yake ilikua kukusanya maoni na si kuwa mshabiki...
sasa si umeweka thread tujadiri ama unataka nichangiaje?.Kasema nani?
Hayo ni mawazo yako binafsi
Sioni sababu ya kuyaheshimu kama mawazo ya wananchi.
Kupitia dk 45 ITV usiku huu, Jaji J. Warioba asema katiba mpya itaondoa kero ya nchi kuwa na maamiri jeshi wakuu 2 wanaopigiwa mizinga 21.
Asema wanaopinga serikali 3 ndiyo wasaliti wa Mwalimu Nyerere aliyeacha nchi hii ikiwa 1, Amiri Jeshi Mkuu 1, Bunge na Mahakama vyenye nguvu
Asema kauli za wabunge kuwa Jeshi litachukua nchi kama serikali 3 zitapita ni uchochezi unaolenga kuwafanya wananchi walichukie Jeshi lao.
Mods naomba sana uzi huu msiunganishe wa s2 waje wajibu haya aliyoyasema jaji warioba
Halafu warioba alipaswa kujiweka pembeni na huo ushabiki coz kama hayo yalikua maoni ya wananchi anahangaika nini sasa? nani kamtuma awasemee? kazi yake ilikua kukusanya maoni na si kuwa mshabiki...
Mkuu hutakiwi kushangaa, ndivyo ilivyo, wanaCCM wenyewe wanataka serikali tatu, ndio maana viongozi wao wakaweka mbinu ya kupiga kura ya wazi ili kuwalazimisha wapigie serikali mbili,Hata siamini macho yangu ni wewe Ritz au naota? Hongera kwa kupona ugonjwa uitwao CCM
Mkuu unaweza kutuambia warioba leo kaongea nini cha maana.Wadu,
Jaji Warioba kaendelea kutiririka. Mungu baba mpe ulinzi wako pande zote,ili aje kuishuhudia S3 tunayoitaka!!!
Warioba anatetea maoni yake mzee karibu atapagawa eti kapika maoni mwenyewe halafu leo anayatetea sijui ataishia wapi.