Warioba Anamdhalilisha Nyerere!

Warioba Anamdhalilisha Nyerere!

K-Boko

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
697
Reaction score
218
Nimemsikia Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Mstaafu Warioba akidai kupitia ITV leo kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa na mawazo mgando, na kwa maana yake, anataka kuhalalisha kuwa kama angekuwepo, Mwalimu angeunga mkono mawazo yao ya kuibuka na serikali tatu.

Amedai kuwa endapo angekuwepo Mwalimu leo angekuwa amekasirika mno kutokana na Katiba iliyopo ilivyochezewa. Naweza kumuunga mkono kwa hilo lakini ni ukweli ulio wazi Mwalimu asingeunga mkono muungano wa serikali tatu kamwe!

Ni udhalilishaji mkubwa wa mtazamo wa Mwalimu kudai kuwa Mwalimu angeunga mkono serikali tatu!! Sote tulikuwa hai wakati Mwalimu alipoingilia kati, tena kwa nguvu zake zote, na kuziua juhudi za kikundi cha 45 cha kuanzisha harakati za kuunda muungano wa serikali tatu, harakati zilizokuwa tayari zimeshaungwa mkono na Mzee Malecela akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais chini ya utawala wa Mzee Mwinyi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba.

Huu anaoutangaza hivi sasa Warioba ni udhalilishaji mkubwa wa mawazo na msimamo wa Mwalimu kuhusu muungano. Ukweli ni kwamba muungano chini ya serikali tatu sio muungano.

Hauna mashiko na ni rahiusi mno kuuvunja akitokea kiongozi mkorofi kutoka upande wa Tanganyika au Zanzibar kuliko muungano katika mtindo uliopo sasa.

Na Warioba pamoja na heshima zake, asiwadhalilishe wananchi wanaopinga mawazo ya kuwa na serikali tatu kwa kuwaita ni "wenye mawazo mgando"--kama anavyoupigia yeye debe muungano wa serikali tatu pia hao wana haki ya msingi na ya kikatiba kuupinga muungano wa serikali tatu.

Akae akijua sio suala la gharama tu linalopigiwa kelele, ila ni suala la mashiko katika muungano wenyewe. Kwa mtazamo wangu anayeupigia upatu muungano wa serikali tatu, hautaki muungano!

Ukweli ni kwamba pamoja na juhudi zote hizo za kuutetea muungano wa serikali tatu, lakini Warioba hayuko wazi kuhusu ni wananchi wangapi wanaoutaka muungano huo.

In fact, katika wananchi wapatao laki 3 waliohojiwa na tume yake kutoka bara na Visiwani, ni watu wapatao 19,000 tu waliounga mkono muungano wa serikali tatu--hakuna uhalali wowote wa kimahesabu na kimantiki unaoweza kusema kwa kujiamini kuwa Watanzania sasa wanaulilia muungano wa serikali tatu.

Kwa kuanzisha muungano wa serikali tatu, ni wazi kabisa tutadhoofisha mno uzalendo wa Utanzania, ambao miaka ya hivi karibuni umeanza kuimarika sana ndani na nje ya nchi.

Hivi sasa bendera ya Tanzania inapepea katika madaladala, bodaboda, viwanjani na vitu vyenye alama ama bendera ya Tanzania vimeanza kutapakaa nje ya nchi!! Watanzania tuwe makini sana katika suala hilo--mvi sio hekima!!
 
Tupe uzuri na ubaya wa serikali mbili pamoja na changamoto zake pia rudi upande wa serikali tatu nazo weka faida na hasara zake ili tujue kama mzee warioba kapotoka,unajua kama sera za mwalimu zilishindwa pia? Unajua kwa nini wakati wa mwiyi aliruhusu soko huria?(ruksa) bs ujue pia kulingana na mda na changamoto za hapa na pale na wimbi la watu wengi kuzidi kuelimika,mwalimu asingekuwa na choice zaidi ya kukubaliana na mawazo ya wengi ya serikali3.
Wanaopinga serikali 3 ni ccm na sio wananchi wote kama unavyojitahidi kupotosha.
 
So, nani kakwambia na mimi ni CCM?

Mimi ni Mtanzania ndugu. Naitetea Tanzania yangu, na wala siijui Tanganyika na wala sina hamu ya kuijua. Nimezaliwa Tanzania!! Hayo ya faida na hasara--soma tena maandishi yangu! By the way, kuwa CCM ni dhambi ila kutokuwa CCM ndio ushujaa sio?
 
Nimemsikia Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Mstaafu Warioba akidai kupitia ITV leo kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa na mawazo mgando, na kwa maana yake, anataka kuhalalisha kuwa kama angekuwepo, Mwalimu angeunga mkono mawazo yao ya kuibuka na serikali tatu. Amedai kuwa endapo angekuwepo Mwalimu leo angekuwa amekasirika mno kutokana na Katiba iliyopo ilivyochezewa. Naweza kumuunga mkono kwa hilo lakini ni ukweli ulio wazi Mwalimu asingeunga mkono muungano wa serikali tatu kamwe! Ni udhalilishaji mkubwa wa mtazamo wa Mwalimu kudai kuwa Mwalimu angeunga mkono serikali tatu!! Sote tulikuwa hai wakati Mwalimu alipoingilia kati, tena kwa nguvu zake zote, na kuziua juhudi za kikundi cha 45 cha kuanzisha harakati za kuunda muungano wa serikali tatu, harakati zilizokuwa tayari zimeshaungwa mkono na Mzee Malecela akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais chini ya utawala wa Mzee Mwinyi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba. Huu anaoutangaza hivi sasa Warioba ni udhalilishaji mkubwa wa mawazo na msimamo wa Mwalimu kuhusu muungano. Ukweli ni kwamba muungano chini ya serikali tatu sio muungano. Hauna mashiko na ni rahiusi mno kuuvunja akitokea kiongozi mkorofi kutoka upande wa Tanganyika au Zanzibar kuliko muungano katika mtindo uliopo sasa. Na Warioba pamoja na heshima zake, asiwadhalilishe wananchi wanaopinga mawazo ya kuwa na serikali tatu kwa kuwaita ni "wenye mawazo mgando"--kama anavyoupigia yeye debe muungano wa serikali tatu pia hao wana haki ya msingi na ya kikatiba kuupinga muungano wa serikali tatu. Akae akijua sio suala la gharama tu linalopigiwa kelele, ila ni suala la mashiko katika muungano wenyewe. Kwa mtazamo wangu anayeupigia upatu muungano wa serikali tatu, hautaki muungano! Ukweli ni kwamba pamoja na juhudi zote hizo za kuutetea muungano wa serikali tatu, lakini Warioba hayuko wazi kuhusu ni wananchi wangapi wanaoutaka muungano huo. In fact, katika wananchi wapatao laki 3 waliohojiwa na tume yake kutoka bara na Visiwani, ni watu wapatao 19,000 tu waliounga mkono muungano wa serikali tatu--hakuna uhalali wowote wa kimahesabu na kimantiki unaoweza kusema kwa kujiamini kuwa Watanzania sasa wanaulilia muungano wa serikali tatu. Kwa kuanzisha muungano wa serikali tatu, ni wazi kabisa tutadhoofisha mno uzalendo wa Utanzania, ambao miaka ya hivi karibuni umeanza kuimarika sana ndani na nje ya nchi. Hivi sasa bendera ya Tanzania inapepea katika madaladala, bodaboda, viwanjani na vitu vyenye alama ama bendera ya Tanzania vimeanza kutapakaa nje ya nchi!! Watanzania tuwe makini sana katika suala hilo--mvi sio hekima!!
wewe jaribu sana kutumia akiri zako za kuzaliwa kuliko kumfanya Nyerere kama mungu wako. jiulize kwa nini Nyerere alipounganisha Tanu na Afro Shiraz hakuuiacha afro shiraz iwe huru visiwani. Ila alipounganisha Tanganyika na Zanzibar aliiacha zanzibar ijitawale? Muungano wa serikali tatu au mbili zote ni hisia za kipuuzi tupu. Muungano ni serikali moja tuu na raisi mmoja kwisha kazi.

Jaribu kujifunza kumkosoa nyerere ili uijenge nchi! usimfanye Nyerere ni mungu wetu wala eti fikira zake ni bora kupita watanganyika wote.
 
Nimemsikia Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Mstaafu Warioba akidai kupitia ITV leo kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa na mawazo mgando, na kwa maana yake, anataka kuhalalisha kuwa kama angekuwepo, Mwalimu angeunga mkono mawazo yao ya kuibuka na serikali tatu. Amedai kuwa endapo angekuwepo Mwalimu leo angekuwa amekasirika mno kutokana na Katiba iliyopo ilivyochezewa. Naweza kumuunga mkono kwa hilo lakini ni ukweli ulio wazi Mwalimu asingeunga mkono muungano wa serikali tatu kamwe! Ni udhalilishaji mkubwa wa mtazamo wa Mwalimu kudai kuwa Mwalimu angeunga mkono serikali tatu!! Sote tulikuwa hai wakati Mwalimu alipoingilia kati, tena kwa nguvu zake zote, na kuziua juhudi za kikundi cha 45 cha kuanzisha harakati za kuunda muungano wa serikali tatu, harakati zilizokuwa tayari zimeshaungwa mkono na Mzee Malecela akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais chini ya utawala wa Mzee Mwinyi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba. Huu anaoutangaza hivi sasa Warioba ni udhalilishaji mkubwa wa mawazo na msimamo wa Mwalimu kuhusu muungano. Ukweli ni kwamba muungano chini ya serikali tatu sio muungano. Hauna mashiko na ni rahiusi mno kuuvunja akitokea kiongozi mkorofi kutoka upande wa Tanganyika au Zanzibar kuliko muungano katika mtindo uliopo sasa. Na Warioba pamoja na heshima zake, asiwadhalilishe wananchi wanaopinga mawazo ya kuwa na serikali tatu kwa kuwaita ni "wenye mawazo mgando"--kama anavyoupigia yeye debe muungano wa serikali tatu pia hao wana haki ya msingi na ya kikatiba kuupinga muungano wa serikali tatu. Akae akijua sio suala la gharama tu linalopigiwa kelele, ila ni suala la mashiko katika muungano wenyewe. Kwa mtazamo wangu anayeupigia upatu muungano wa serikali tatu, hautaki muungano! Ukweli ni kwamba pamoja na juhudi zote hizo za kuutetea muungano wa serikali tatu, lakini Warioba hayuko wazi kuhusu ni wananchi wangapi wanaoutaka muungano huo. In fact, katika wananchi wapatao laki 3 waliohojiwa na tume yake kutoka bara na Visiwani, ni watu wapatao 19,000 tu waliounga mkono muungano wa serikali tatu--hakuna uhalali wowote wa kimahesabu na kimantiki unaoweza kusema kwa kujiamini kuwa Watanzania sasa wanaulilia muungano wa serikali tatu. Kwa kuanzisha muungano wa serikali tatu, ni wazi kabisa tutadhoofisha mno uzalendo wa Utanzania, ambao miaka ya hivi karibuni umeanza kuimarika sana ndani na nje ya nchi. Hivi sasa bendera ya Tanzania inapepea katika madaladala, bodaboda, viwanjani na vitu vyenye alama ama bendera ya Tanzania vimeanza kutapakaa nje ya nchi!! Watanzania tuwe makini sana katika suala hilo--mvi sio hekima!!
inaonekana umetoka chooni kuvuta ganja lako unaingia humu ukifikiri unaleta thread ya maana kumbe ----- mtupu!! kama uhendeshwi na ganja umetoa wapi hilo la kundi la watu 45 waliopinga muungano katika nchi hii? maviroba na mabangi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!
 
So, nani kakwambia na mimi ni CCM?

Mimi ni Mtanzania ndugu. Naitetea Tanzania yangu, na wala siijui Tanganyika na wala sina hamu ya kuijua. Nimezaliwa Tanzania!! Hayo ya faida na hasara--soma tena maandishi yangu! By the way, kuwa CCM ni dhambi ila kutokuwa CCM ndio ushujaa sio?

Hakuna sehemu yoyote niliyosema ww ni ccm bali nimesema wanaopinga serikali 3 ni ccm, na kwa jibu lako hapa huna haja ya kusema ww ni mtanzania wala mtanganyika bali ni ccm damu na kuwa ccm sio dhambi mkuu bali mmedumazwa na mfumo hamfikirii nje ya box.
Tume ya jaji warioba ilitumia kodi zetu kuzunguka karibia tz nzima na huo ndiyo msimamo wa watanzania wote bila kujali itikadi zetu,so hatuna budi kuyapokea mawazo ya watanzania wengi,na kama ilivyo ada wengi wasikilize wachche wape,mkicheza karata zenu vzr mnaweza fanikiwa hizo serikali 2
 
K-BoKO: naomba kujua ni watu gani waliomba muungano? Kama ni wazanzibari kwa sasa wanataka serikali tatu sasa ulipotoa mawazo yako ulikuwa unalijua hilo, muungano wa serikali tatu unawekwa kwa masilahi ya wazanzibari watu ambao tumekuwa tukilazimisha kuwanao kwa sababu wanazojua wachache, kikwete atakumbukwa kwa lile la serikali ya umoja wa kitaifa na hili kama litapita na.wazanzibari, azimio la arusha lilikufa wakati wa mwalimu wakati.akiwepo mbona hakusema kadhalilishwa?
 
Sijao pahali Mzee Warioba alipo mkosea heshima Mwl. Msingi wa alichokisema Warioba, ni kuwa Katiba imechezewa chezewa na malimbukeni na walafi wa madaraka kiasi kwamba kwa hatua tulionayo sasa (kutokana na kusiginywa kwa Katiba ya sasa) hata Mwl angefufuka sasa, hapana shaka asingekuwa "na mawazo mgando" wa kung'ania muundo wa serikali mbili.

Hao Majangili ya kisiasa ndo hao hao wanaompinga Warioba though ndo wametufikisha hapa tulipo!

Ni serikali tatu ndo yenye jibu la kurekebisha at least matatizo yaliyopo, haiwezi kutibu kabisa kwani kuna manyang'au yakisiasa ambayo at the core of their thought,wanahitaji utengano wa nchi mbili hzi ili waogelee kwenye bwawa la vyeo vya kisiasa na faida za kimadaraka!
 
Tupe uzuri na ubaya wa serikali mbili pamoja na changamoto zake pia rudi upande wa serikali tatu nazo weka faida na hasara zake ili tujue kama mzee warioba kapotoka,unajua kama sera za mwalimu zilishindwa pia? Unajua kwa nini wakati wa mwiyi aliruhusu soko huria?(ruksa) bs ujue pia kulingana na mda na changamoto za hapa na pale na wimbi la watu wengi kuzidi kuelimika,mwalimu asingekuwa na choice zaidi ya kukubaliana na mawazo ya wengi ya serikali3.
Wanaopinga serikali 3 ni ccm na sio wananchi wote kama unavyojitahidi kupotosha.

Siku zote kikwete hafanani na hao ccm katika maamuzi yake siunakumbuka ya serikali ya umoja wa kitaifa, kwa hili serikali tatu ndio litapita lakini naomba unijuze kwanini sisi wabara tunaing'an'gania zanzibar? Tunafaidika na nini na tuna the best army na strategic areas za kuweka kambi za jeshi
 
Nimemsikia Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Mstaafu Warioba akidai kupitia ITV leo kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa na mawazo mgando, na kwa maana yake, anataka kuhalalisha kuwa kama angekuwepo, Mwalimu angeunga mkono mawazo yao ya kuibuka na serikali tatu. Amedai kuwa endapo angekuwepo Mwalimu leo angekuwa amekasirika mno kutokana na Katiba iliyopo ilivyochezewa. Naweza kumuunga mkono kwa hilo lakini ni ukweli ulio wazi Mwalimu asingeunga mkono muungano wa serikali tatu kamwe! Ni udhalilishaji mkubwa wa mtazamo wa Mwalimu kudai kuwa Mwalimu angeunga mkono serikali tatu!! Sote tulikuwa hai wakati Mwalimu alipoingilia kati, tena kwa nguvu zake zote, na kuziua juhudi za kikundi cha 45 cha kuanzisha harakati za kuunda muungano wa serikali tatu, harakati zilizokuwa tayari zimeshaungwa mkono na Mzee Malecela akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais chini ya utawala wa Mzee Mwinyi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba. Huu anaoutangaza hivi sasa Warioba ni udhalilishaji mkubwa wa mawazo na msimamo wa Mwalimu kuhusu muungano. Ukweli ni kwamba muungano chini ya serikali tatu sio muungano. Hauna mashiko na ni rahiusi mno kuuvunja akitokea kiongozi mkorofi kutoka upande wa Tanganyika au Zanzibar kuliko muungano katika mtindo uliopo sasa. Na Warioba pamoja na heshima zake, asiwadhalilishe wananchi wanaopinga mawazo ya kuwa na serikali tatu kwa kuwaita ni "wenye mawazo mgando"--kama anavyoupigia yeye debe muungano wa serikali tatu pia hao wana haki ya msingi na ya kikatiba kuupinga muungano wa serikali tatu. Akae akijua sio suala la gharama tu linalopigiwa kelele, ila ni suala la mashiko katika muungano wenyewe. Kwa mtazamo wangu anayeupigia upatu muungano wa serikali tatu, hautaki muungano! Ukweli ni kwamba pamoja na juhudi zote hizo za kuutetea muungano wa serikali tatu, lakini Warioba hayuko wazi kuhusu ni wananchi wangapi wanaoutaka muungano huo. In fact, katika wananchi wapatao laki 3 waliohojiwa na tume yake kutoka bara na Visiwani, ni watu wapatao 19,000 tu waliounga mkono muungano wa serikali tatu--hakuna uhalali wowote wa kimahesabu na kimantiki unaoweza kusema kwa kujiamini kuwa Watanzania sasa wanaulilia muungano wa serikali tatu. Kwa kuanzisha muungano wa serikali tatu, ni wazi kabisa tutadhoofisha mno uzalendo wa Utanzania, ambao miaka ya hivi karibuni umeanza kuimarika sana ndani na nje ya nchi. Hivi sasa bendera ya Tanzania inapepea katika madaladala, bodaboda, viwanjani na vitu vyenye alama ama bendera ya Tanzania vimeanza kutapakaa nje ya nchi!! Watanzania tuwe makini sana katika suala hilo--mvi sio hekima!!
wewe ndo mwenye mawazo mgando-serikali 3 ni lazima-zanzibar kwetu ni mzigo usio na maana-ni bora kuutua tu
 
Democracy at its best!

Ila inakwaza sana watu wazima wanapojaribu kupotosha msimamo wa Nyerere hata kabla 'hajaoza' kaburini na baadhi yetu tuliomfahamu bado tukiwa hai! Wakasome kitabu chake "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania".
 
Usitokwe povu sana kwa kuetetea serikali 2, je na tunaotaka serikali 1, mbona hatutoi matamko? Muungano siyo mali ya wanasiasa kama wananchi wakiamu hawautaki hakuna mwanasiasa atakayelazimisha juo hilo.
Nakushauri uwashawishi viongozi wako wa CCM kuwa kwanini wasiitishe kura ya maoni kuhusu muungano kaka tunautaka au hatuutaki? na kama tunautaka je tunautaka wa serikali ngapi?
Note: Tusitetee serikali ngapi tunazotaka badala ya kuulizwa hayo maswali hapo juu.

Nimemsikia Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Mstaafu Warioba akidai kupitia ITV leo kuwa Mwalimu Nyerere hakuwa na mawazo mgando, na kwa maana yake, anataka kuhalalisha kuwa kama angekuwepo, Mwalimu angeunga mkono mawazo yao ya kuibuka na serikali tatu. Amedai kuwa endapo angekuwepo Mwalimu leo angekuwa amekasirika mno kutokana na Katiba iliyopo ilivyochezewa. Naweza kumuunga mkono kwa hilo lakini ni ukweli ulio wazi Mwalimu asingeunga mkono muungano wa serikali tatu kamwe! Ni udhalilishaji mkubwa wa mtazamo wa Mwalimu kudai kuwa Mwalimu angeunga mkono serikali tatu!! Sote tulikuwa hai wakati Mwalimu alipoingilia kati, tena kwa nguvu zake zote, na kuziua juhudi za kikundi cha 45 cha kuanzisha harakati za kuunda muungano wa serikali tatu, harakati zilizokuwa tayari zimeshaungwa mkono na Mzee Malecela akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais chini ya utawala wa Mzee Mwinyi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba. Huu anaoutangaza hivi sasa Warioba ni udhalilishaji mkubwa wa mawazo na msimamo wa Mwalimu kuhusu muungano. Ukweli ni kwamba muungano chini ya serikali tatu sio muungano. Hauna mashiko na ni rahiusi mno kuuvunja akitokea kiongozi mkorofi kutoka upande wa Tanganyika au Zanzibar kuliko muungano katika mtindo uliopo sasa. Na Warioba pamoja na heshima zake, asiwadhalilishe wananchi wanaopinga mawazo ya kuwa na serikali tatu kwa kuwaita ni "wenye mawazo mgando"--kama anavyoupigia yeye debe muungano wa serikali tatu pia hao wana haki ya msingi na ya kikatiba kuupinga muungano wa serikali tatu. Akae akijua sio suala la gharama tu linalopigiwa kelele, ila ni suala la mashiko katika muungano wenyewe. Kwa mtazamo wangu anayeupigia upatu muungano wa serikali tatu, hautaki muungano! Ukweli ni kwamba pamoja na juhudi zote hizo za kuutetea muungano wa serikali tatu, lakini Warioba hayuko wazi kuhusu ni wananchi wangapi wanaoutaka muungano huo. In fact, katika wananchi wapatao laki 3 waliohojiwa na tume yake kutoka bara na Visiwani, ni watu wapatao 19,000 tu waliounga mkono muungano wa serikali tatu--hakuna uhalali wowote wa kimahesabu na kimantiki unaoweza kusema kwa kujiamini kuwa Watanzania sasa wanaulilia muungano wa serikali tatu. Kwa kuanzisha muungano wa serikali tatu, ni wazi kabisa tutadhoofisha mno uzalendo wa Utanzania, ambao miaka ya hivi karibuni umeanza kuimarika sana ndani na nje ya nchi. Hivi sasa bendera ya Tanzania inapepea katika madaladala, bodaboda, viwanjani na vitu vyenye alama ama bendera ya Tanzania vimeanza kutapakaa nje ya nchi!! Watanzania tuwe makini sana katika suala hilo--mvi sio hekima!!
 
Wanaopinga mfumo serekali 3 ni CCM na wanaotaka mfumo wa serekali 2 uendelee ni CCM kutokana na sababu wanazozijua wenyewe.Walioleta muungano wa ajabu ajabu ambao haujawahi kutokea dunia ni CCM.Ni muungano wa ajabu kwa sababu huwezi ukaunganisha vitu viwili halafu vikapatikana vitu viwili.Vitu viwili vinapounganika ni lazima kitokee kitu kimoja.Kama TANU na ASP zilivyounganishwa ikapatikana CCM moja kwanini kwenye muungano wa serekali ya Tanganyika na ya Zanzibar zikazaliwa serekali 2 badala ya moja?kama CCM ilivyo moja.Wanao taka serekali 3 ni wananchi wala siyo Waryoba ili pawepo na usawa huwezi ukasema kuwa kunamuungano wa usawa wakati kuna nchi moja pamoja na serekali yake haipo halafu upande mmoja una sekali yake na nchi.Pia hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kuwa kile kilichofanywa na Nyerere hakiruhusiwi kubadilishwa hata kuboreshwa hakiruhusiwi hata Nyerere mwenyewe hajawahi kusema kuwa hiki ninacho kifanya kiendelee kuwa hivi hivi milele na milele.Wananchi nao wanataka kufanya chakwao endapo Nyerere angetokea akafufuka wawe na cha kumuonyesha kuwa wewe ulituachia hiki lakini sisi tumefanya hiki na kile.
 
So, nani kakwambia na mimi ni CCM?

Mimi ni Mtanzania ndugu. Naitetea Tanzania yangu, na wala siijui Tanganyika na wala sina hamu ya kuijua. Nimezaliwa Tanzania!! Hayo ya faida na hasara--soma tena maandishi yangu! By the way, kuwa CCM ni dhambi ila kutokuwa CCM ndio ushujaa sio?

Dah! natamani ningekua Sniper!!! ningekua najitolea bila kutumwa na mtu!
 
Mleta mada umepatia sana. Mungu akubariki. Jaji warioba nampenda, lakini kwa serikali tatu kaweka utashi wake. Njelu kasaka, muumini wa serikali tatu hakubaliani naye. Stay tune! Tanzania yangu maskini inakufa
. Tutaipigania hadi mwisho.
 
Sijao pahali Mzee Warioba alipo mkosea heshima Mwl. Msingi wa alichokisema Warioba, ni kuwa Katiba imechezewa chezewa na malimbukeni na walafi wa madaraka kiasi kwamba kwa hatua tulionayo sasa (kutokana na kusiginywa kwa Katiba ya sasa) hata Mwl angefufuka sasa, hapana shaka asingekuwa "na mawazo mgando" wa kung'ania muundo wa serikali mbili.

Hao Majangili ya kisiasa ndo hao hao wanaompinga Warioba though ndo wametufikisha hapa tulipo!

Ni serikali tatu ndo yenye jibu la kurekebisha at least matatizo yaliyopo, haiwezi kutibu kabisa kwani kuna manyang'au yakisiasa ambayo at the core of their thought,wanahitaji utengano wa nchi mbili hzi ili waogelee kwenye bwawa la vyeo vya kisiasa na faida za kimadaraka!

Endapo utaona vyema message yangu, nimeunga mkono la kuchezewa kwa katiba iliyopo--na hasa upande wa Zanzibar--ila kama ilivyokuwa kwa Mwalimu--siamini kabisa kwamba solution ni serikali tatu. Mbona suala hilo liliibuliwa wakati Mwalimu akiwa hai, tena kwa hoja hizo hizo za kuchezewa kwa katiba, hasa upande wa Zanzibar na kwa kutumia uwezo wake kama Jeshi la Mtu Mmoja akaiua hoja ya serikali tatu iliyokuwa ikiasisiwa na akina Njelu Kasaka na kundi lao la watu 45? Tuzungumze tatizo halisi hapa badala ya kulikwepa! Kama viongozi wetu wameshindwa kumfunga paka kengele, naamini Watanzania wa kweli watamfunga katika kura ya maoni ijayo!! Na pia naamini iko siku ataibuka kiongozi Mtanzania atakayemdhibiti vyema 'paka' asiichezee katiba ya TANZANIA.
 
Back
Top Bottom