Warioba afunguka, atoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja za taarifa yake

Wakuu, nimejitaidi kutafuta gazeti la MWANANCHI lakini sijalipata katika vijiwe kazaa huku Arusha.

Kwa atakae lipata tafadhali atujuze.
mkuu unatumia mtandao lkn hauwezi kukusaidia kupata taarifa zingine!? Ingia kwenye tovuti ya mwananchi lipo limewekwa tangu saa 1
 
Ni akili za maiti tu ndio zinaweza kupinga kuwa kwa sasa viongozi wa Tanganyika wanawaogopa viongozi wa serikali ya Zanzibar kama jinsi swala anavyo muogopa Simba mwitu mwenye njaa! Waliovunja katiba ya Muungano wakanyamaziwa leo bado wanabebwa kwa mbereko za mlenda! Jk na uluteni wake aliapa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT lakini mabadiliko ya 2010 yaliyoifanya ZnZ kuwa nchi kamili yalifanyika akiwa kajivalia zake kikoi huku kawekewa kashata za nazi na mkewe kipenzi akiwaza starehe anazopata akiwa mawingu kuelekea kwa Obama kumueleza namna Mbu wanavyo kuwa kikwazo cha maendeleo ya Wakwere.

Kaka inaelekea una kucha za chuma na meno yako hayang'oleki!
 
Yeyote anayembeza nyerere atakuwa na mapungufu ya hali ya juuu sana mwalimu alijenga taifa lenye umoja kamili.

....Ule Muungano wa magumashi aliouacha Nyerere sio huu wa leo, ule tayari CCM walishauchakachua vya kutosha ndo maana leo kuna serikali 2 wkati Nyerere aliacha serikali 1. SOma vizuri kwanza tarifa ya Warioba hapo juu kisha utaelewa ni akina nani haswa wanambeza na kumuona Nyerere kuwa punguani.

Nakubaliana na wewe kuwa anayembez Nyerere atakuwa na mapungufu ya hali ya juu, kwa mantiki hiyo hakuna Mwana CCM ambae yupo sawa maana hao ndo wanaombeza Nyerere kwa kung'ang'ania serikali 2 ambazo ni kinyume na matakwa na malengo ya huyo Nyerere.

Uwe unasoma dogo, sio kushabikia ujinga tu!
 
Mimi nitakuwa mtu wa mwisho kumwelewa huyu rais kwa sababu zifuatazo.

1.analalamikia idadi ya watu waliotoa maoni kuwa ni ndogo wakati tume aliunda yeye na muda na bajeti katoa yeye.
kwa hapa maswali ni haya.

.Kwa nini hakutoa mwaka mzima kama wa tume ya jaji kisanga?
.Kwa nini hakuongeza bajeti ili ikibido hata chopa zitumike?
.Yeye alichaguliwa na watanzania mil ngapi kati ya watu mil45?

2.Analalamikia mfumo wa serikali tatu na si mbili maswali hapa ni haya.
.Sio yeye alitoa hadidu za rejea?
.Kama ni yeye kwa nini yote aliyotunga juzi hakutunga wakati huo na kuyafanya hadidu za rejea?
.Kama serikali tatu ni mbaya kama alivyotuambia na kwa jinsi zanzibar ilivyovunja katiba ya jamhuri haoni ni wakati sasa wa kuwa na serikali moja?
.Je haoni kama aliyokuwa akitoa juzi ni maoni yake ambapo atakuwa amevunja sheria kwa kutoa maoni wakati kisheria muda ulishaisha?

3.Kwa mujibu wa sheria walizojiwekea jaji warioba alitakiwa kuwakilisha rasimu ya pili mbele ya bunge la katiba lakini kwa kupindisha sheria aliwakilisha rasimu mbele ya semina ya wajumbe ambao wangekuja kuwa wabunge wa bunge maalu la katiba,maswali hapa ni haya.
.Mh rais haoni kavunja sheria kwa kutoa maoni na msimamo badala ya kutimiza matakwa ya sheria yaliyomtaka kulizindua bunge>
.Rais haoni kuwa spika kakiuka sheria kwa warioba kuwakilisha rasimu kwa kitu ambacho shria yenyewe haikitambui?
.Nikienda mahakamani na kumshitaki kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria uliofanywa na yeye atatumia hela za uma kulipa gharama za kesi au atatumia mshahara wake?
.Kwa nini hakuyatoa hayo maoni anayoona kwa busara zake ni mazuri katika tume ya warioba/au ni ushauri aliokuja kuupata mbele?
.Kwa ukiukwaji huu mkubwa wa shria uliofanya na rais ambaye tulitegemea kuwa ni mfano katika kusimamia sheria haoni ametufundisha sisi wa chini kuvunja sheria?

Mwisho namalizia kwa kumwambia atake serikali 1,2,3,4,5,6,7,8,9 ahakikishe TANG​

Natumai una akili na wewe ni mtu mzima, ijapokuwa hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kuwa na hoja dhaifu kama za kwako;

Hapo kwenye Blue; Hakuna mahali Kikwete alilalamikia idadi ya watu waliotoa maoni kuwa ni ndogo, isipokuwa alihoji udogo wa namba ya watu waliozungumzia muundo wa muungano ikiwa kweli muundo uliopo unachukizwa/unanung'unikiwa na watu walio wengi kama ambavyo tume inataka kutuaminisha.

Hapo kwenye Red; Kitu kizima ni idadi ya watu waliotoa maoni na sio idadi ya watanzania wote kama ambavyo katika kura za urais kitu kizima kilikuwa ni idadi ya wapiga kura na sio idadi ya watanzania wote, kwa hiyo hoja yako haingii akilini kabisa.

Kwa hesabu za kitoto kabisa takwimu za tume hazionyeshi ukweli kuwa watanzania walio wengi wanataka muundo wa serikali 3, wanachofanya ni kugeuza uwingi kuwa uchache na uchache kuwa uwingi. Nashawishika kuwa maoni ya tume sio ya wanachi walio wengi, Rais ameliona hilo ndio maana kalisemea bila hiyana wala kificho, mkitaka kuamua vinginevyo amueni nyinyi ila yeye katimiza wajibu wake. Ni dhambi kubwa sana Tume kutumia mwamvuli wa maoni ya wananchi kupitisha maoni yao binafsi.
 
Magamba ni wanafiki wa kutupwa, kum beza Mwalimu wanambeza sana , lkn wanajitia kulia eti wanamuenzi.
Kama kweli hamum bezi Muungano ungekuwa bado na sura aliyoiacha, huu wa sasa wa kwao na upo ki maslahi yao zaidi.
Vp na kwenye Azimio la Arusha nako mnamuenzi?
 
1900066_652131428167507_989521899_n.jpg
 
Natumai una akili na wewe ni mtu mzima, ijapokuwa hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kuwa na hoja dhaifu kama za kwako;

Hapo kwenye Blue; Hakuna mahali Kikwete alilalamikia idadi ya watu waliotoa maoni kuwa ni ndogo, isipokuwa alihoji udogo wa namba ya watu waliozungumzia muundo wa muungano ikiwa kweli muundo uliopo unachukizwa/unanung'unikiwa na watu walio wengi kama ambavyo tume inataka kutuaminisha.

Hapo kwenye Red; Kitu kizima ni idadi ya watu waliotoa maoni na sio idadi ya watanzania wote kama ambavyo katika kura za urais kitu kizima kilikuwa ni idadi ya wapiga kura na sio idadi ya watanzania wote, kwa hiyo hoja yako haingii akilini kabisa.

Kwa hesabu za kitoto kabisa takwimu za tume hazionyeshi ukweli kuwa watanzania walio wengi wanataka muundo wa serikali 3, wanachofanya ni kugeuza uwingi kuwa uchache na uchache kuwa uwingi. Nashawishika kuwa maoni ya tume sio ya wanachi walio wengi, Rais ameliona hilo ndio maana kalisemea bila hiyana wala kificho, mkitaka kuamua vinginevyo amueni nyinyi ila yeye katimiza wajibu wake. Ni dhambi kubwa sana Tume kutumia mwamvuli wa maoni ya wananchi kupitisha maoni yao binafsi.
kwa hiyo kwa akili yako ya kuazima kwa jirani unaona ni busara kwa rais kuleta mipasho wakati alikuwa na muda wa kutosha hata kupendekeza rasimu kurudiwa upya toka amekabidhiwa?
au na wewe ni mtu wa pwani wa kusubiri kusutana hadharani?
 
Sasa imebainika kuwa kuna Rasimu 2; ya Kikwete na ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Lakini sijawahi kuwa na imani na busara za Kikwete hata siku moja!
 
Tumieni muda wenu vizuri kushauri namna ya kuichoma nchi watanzania mmechoka kuishi kwa amani
 
Mkuu wa nchi anayo haki ya kutoa indhari na tahadhari juu ya maamuzi ambayo lazima yazingatie maslahi mapana ya taifa
 
kwa hiyo kwa akili yako ya kuazima kwa jirani unaona ni busara kwa rais kuleta mipasho wakati alikuwa na muda wa kutosha hata kupendekeza rasimu kurudiwa upya toka amekabidhiwa?
au na wewe ni mtu wa pwani wa kusubiri kusutana hadharani?

Mimi nimekujibu kwa hoja, nadhani wewe ndo unaleta mipasho na kutaka kusutana hadharani,... otherwise na wewe ungenijibu kwa hoja.

Mimi sijaona mipasho ya mh. Rais, isipokuwa umenifahamisha kuwa kila usilolitaka wewe kulisikia masikioni mwako kwako ni mipasho.
 
Tume ya warioba iliundwa na warioba alikuwa m/kiti kusimamia zoezi zima la kukusanya maoni kwa watanzania wote juu ya katiba mpya.

Baada ya kuundwa tume ya warioba nimepata mashaka ccm waliunda tume ya kikwete na kikwete alikuwa m/kiti ili kusimamia zoezi la kukusanya maoni kwa wana ccm.

Hoja kwa nini kikwete alipingana na mawazo ya tume aliyoiamini akaiteua mwenyewe mbaya zaidi kikwete alisema mawazo ya tume yake ya ccm,pia wakafanya sherehe baada ya mawazo yao kuungwa mkono na wajumbe wasio wazalendo.

Karibu katika mjadala huu matusi hayabadili msimamo wangu.
 
Tume imeonyesha umakini kwa sbb watanzania bara wengi walitoa maoni ya kuendelea na serikali 2 kwa sbb walikuwa hawajui yanayoendelea Z'bar.Lkn kwa kupitia taarifa ya Tume waTanzania bara ndo wameanza kujua ss..Kwa nn CCM watumie ujinga wa wingi wa watanzania bara kutekeleza matakwa yao??
 
Mwenyekiti+wa+Tume+ya+Mabadiliko+ya+Katiba+-+Jaji+Joseph+Warioba.jpg

ILIYOKUWA Tume ya Mabadiliko ya Katiba, chini ya Jaji Joseph Warioba, imetoa ufafanuzi katika baadhi ya maeneo ya Rasimu ya Katiba yaliyokosolewa na Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge Maalumu la Katiba wiki iliyopita.

Taarifa ya Tume hiyo kwa umma wa Watanzania, iliyosambazwa jana kwenye vyombo vya habari, ilisema hatua hiyo ya kutoa ufafanuzi katika baadhi ya maeneo imetokana na kile kinachoelezwa na Tume hiyo kuwa shauku kubwa ya wananchi kutaka ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu Rasimu ya Katiba baada ya hotuba ya Rais Kikwete. (J.G)


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ufafanuzi huo umetokana na kikao cha tathmini kilichofanywa na wajumbe wa iliyokuwa Tume hiyo ya Warioba, kilichofanyika Jumatatu wiki hii ya Machi 24, mwaka huu jijini Dar es Salaam, baada Tume kuhitimisha kazi yake hiyo.

Maeneo ambayo Tume hiyo imeyafanyia ufafanuzi ni pamoja na Usanifu wa Katiba; Malengo muhimu na mwelekeo wa shughuli za Serikali na sera za kitaifa (Dira); Nchi mbili, Serikali mbili; Mamlaka ya Rais; Orodha ya mambo ya Muungano; Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mamlaka ya Mahakama ya Rufani na takwimu kuhusu maoni ya wananchi juu ya muundo wa Muungano.Ufafanuzi kamili ni kama ifuatavyo:-


UTANGULIZI


  1. Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika kutekeleza majukumu iliyopewa imetoa taarifa ya Tume yenye viambatisho vingi na vyenye maelezo ya kina kuhusu mchakato wa kuratibu, kukusanya, kuchambua maoni ya wananchi na kuandaa ripoti.
  2. Baada ya kukamilisha kazi hiyo, Tume iliwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalumu la Katiba Machi 18, mwaka huu. Pamoja na Rasimu hiyo, Tume iliwasilisha Randama ya Rasimu ya Katiba na Bango kitita la Randama ya Rasimu ya Katiba ambayo ilitoa maelezo ya kila Ibara ya Rasimu ikitoa maudhui, madhumuni na lengo pamoja na sababu za mapendekezo ya kila Ibara.
  3. Tangu kuwasilishwa kwa Rasimu na vyaraka zilizoambatana nayo katika Bunge Maalumu la Katiba, kumejitokeza tafsiri tofauti kuhusu baadhi ya mapendekezo yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba na baadhi ya taarifa zilizoambatana na Ripoti ya Tume. Katika maeneo ambayo kumekuwepo na tafsiri tofauti tofauti, ufafanuzi wa kina umetolewa kwenye Randama na bango kitita ya Randama ya Rasimu ya Katiba.
  4. Kutokana na hali hiyo, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, katika kikao chake cha tathmini ya kuhitimisha kazi kilichofanyika Machi 24, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, imeamua kutoa maelezo ya ziada ya ufafanuzi kama ifutavyo:-

NCHI MBILI SERIKALI MBILI
Tangu Mwaka 1984 hatua ambazo zimechukuliwa na serikali zote mbili za Muungano na Zanzibar zimeifanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kuwa Nchi Moja yenye Serikali mbili na kuwa Nchi mbili zenye Serikali mbili. Kwa maana nyingine Masharti yaliyomo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano yanaelekeza kwamba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi moja yenye Serikali mbili- Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kufuatia Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Zanzibar imetamka ni Nchi tofauti na ilivyokuwa imetamka kwamba ni sehemu ya Jamhuri ya
Muungano kabla ya Mabadiliko hayo.


Wakati Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni Nchi moja, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilikuwa na Mamlaka ya Kutunga Sheria juu ya Mambo ya Muungano kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yote, sasa uwezo huo umewekewa mipaka na Katiba ya Zanzibar Katika Ibara ya 132 ambayo inaelekeza kwamba Sheria iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya kuanza kutumika Zanzibar ipelekwe kwenye Baraza la Wawakilishi na kupata ridhaa ya kutumika Zanzibar .Zipo Sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilipokosa ridhaa ya Baraza la Wawakilishi zilirejeshwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kufanyiwa marekebisho ili kukidhi maelekezo ya Baraza la Wawakilishi, kwa mfano, Sheria ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (Commission for Human Rights and Good Governance Act) na Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority Act)

MAMLAKA YA RAIS
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 imempa Rais wa Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo ya kiutawala katika Mikoa na Wilaya. Hata hivyo, Marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 yanampa Rais wa Zanzibar Mamlaka kama hayo ya kuigawa Zanzibar bila kufanya marekebisho stahiki ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Mwaka 1977. Kwa mantiki hiyo mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano yamepungua na kubaki kwa Tanzania Bara tu.

MAMLAKA YA MAHAKAMA YA RUFANI

Katiba ya Muungano ya 1977 imetoa mamlaka ya kusikiliza rufaa nchi nzima. Lakini Zanzibar imezuia Mahakama hiyo kusikiliza rufaa kutoka Mahakama za Kadhi, kutafsiri Katiba ya Zanzibar na rufaa kuhusu mashauri ya haki za binadamu.
Kwa kifupi:

  1. Waasisi walituachia mambo 21 (ukiacha usajili wa vyama) kwenye orodha ya Muungano. Katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita yamepunguzwa. Mambo yote yaliwekwa kwa utaratibu uliowekwa na Katiba lakini yameondolewa kinyume na Katiba. Sehemu zote mbili ziliamua kuachia baadhi ya mambo yake kuwa chini ya Serikali ya Muungano, sasa sehemu moja inaondoa mambo yake. Kwa hiyo serikali ya Muungano itakuwa inashughulikia zaidi mambo ya upande mmoja.
  2. Waasisi walituachia Bunge lenye madaraka nchi nzima. Sasa ni lazima lipate idhini ya Baraza la Wawakilishi.
  3. Waasisi waliacha Rais akiwa na madaraka kamili. Madaraka hayo yamepunguzwa bila kufuata utaratibu wa Katiba.
  4. Waasisi walituachia Mahakama ya rufani yenye madaraka kamili. Madaraka haya yamepunguzwa.
  5. Waasisi waliunganisha nchi mbili ikawa moja. Sasa tunazo nchi mbili.
  6. Hii ndiyo inafanya wananchi wa Tanzania Bara waamini Zanzibar ni huru katika mambo yao. Wanaona ina mamlaka kamili kushughulikia mambo yake na imechukua rasilimali zake. Serikali ya Muungano imebaki na mamlaka na rasilimali za Tanzania Bara. Wabunge wa Zanzibar wanashiriki kuamua mambo ya Tanzania Bara lakini wabunge wa Tanzania Bara hawana nafasi ya kushiriki katika kuamua mambo ya Zanzibar.
  7. Tume iliona ni vigumu kwa Zanzibar kurudi kwa hiyari kwenye hali ya awali, yaani kurudisha mambo yote yaliyotolewa kwenye orodha ya Muungano, kurudisha madaraka ya Rais na kufuta kipingere cha nchi mbili kwenye Katiba yake. Tume iliona kwamba pamoja na mambo haya kufanywa kinyume na Katiba ya Muungano hali ibaki hivyo hivyo. Lakini kwa kufanya hivyo basi malalamiko ya Tanzania Bara nayo yasipuuzwe. Hivyo Tume nayo ikapendekeza Serikali ya Tanganyika iundwe.

HITIMISHO
Tume inapenda kuwashukuru wananchi wote kwa shauku kubwa ya kutaka ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu Rasimu ya Katiba.


 
Kebehi na matusi ya J.k kwa Warioba ni dhihaka kwa watanzania wote. Warioba ni sauti ya watanzania na is chama. Nashauri Warioba agombee urais either kwa Ccm au Cdm atapa. Wananchi wana imani sana na wewe na namna ya kumpa somo J.k ni wewe kuwa na Rais na kuhakikisha katiba ya wananchi ndiyo inakuwepo.
 
Back
Top Bottom