Warioba Abashiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warioba Abashiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ochu, Sep 24, 2008.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Warioba abashiri mafisadi wa EPA kutikisa nchi


  Tanzania kama Taifa lenye dola kamili (sovereign) litatikisika na kudhalilika mno machoni pa wananchi wake na katika jumuiya ya kimataifa, iwapo matajiri waliogushi na kuiba fedha za katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) hawatafikishwa mahakamani.

  Onyo hilo limetolewa jana na waziri Mkuu wa zamani Jaji Joseph Sinde Warioba alipofanya mahojiano maalum na gazeti hili, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Jaji Warioba alisema kimsingi hatua za awali zilizochukuliwa na serikali kukabiliana na mafisadi zina mwelekeo mzuri.

  ``Tutakuwa tumefanya makosa makubwa na ya kihistoria, kutowafikisha wezi kortini eti kwa sababu ni matajiri. Kosa hili litakuwa limeitikisa Tanzania kama nchi sovereign (Dola).

  Watu wakijua kwamba katika nchi yao matajiri hawafikishwi mbele ya sheria (Mahakamani) hawatakuwa na imani na serikali yao, hawataiheshimu serikali,`` alisema na kuongeza:
  ``Kama matajiri wasipofikishwa mahakamani eti kwa ajili ya fedha walizo nazo, basi dola itakuwa imeweka rehani uwezo, madaraka na mamlaka yake kwa mafisadi.``

  Sakata la EPA liliibuka katika hesabu wa BoT za mwaka 2005/06 ambapo iligundilika kwamba kiasi cha Sh bilioni 133 zilichotwa na makampuni fisadi 22.

  Alisema hata kauli iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete juu ya umuhimu wa kurejeshwa kwa fedha hizo na wahusika kufikishwa mbele ya sheria, imetoa mwanga mzuri zaidi juu ya jambo hilo.

  Hata hivyo Mwanasiasa huyo alionya kwamba kurudisha pesa hizo pekee, hakutoshi na wala si njia ya kumaliza kashfa hiyo ambayo imewaudhi wananchi kwa kiasi kikubwa.

  Vilevile alisema kukaa kimya kutayafanya mataifa ya nje, na hata wahisani kuishangaa serikali na kuibeza.

  ``Lazima tujue na kuzingatia kwamba suala la EPA lilikuwa si lelemama, lile lilikuwa jambo kubwa, liliwahusisha watu wakubwa, na fedha zilizoibwa zilikuwa nyingi na mbinu zilizotumika zilikuwa za hali ya juu, kwa hiyo busara za hali ya juu ilibidi zitumike, na bado busara hizo zinahitajika japokuwa kilele cha yote ni mahakamani, hakuna uchochoro wa kukwepa korti,`` alisema.

  Hata hivyo alisema baada ya kusikiliza mlolongo wa tatizo hilo, ni wazi kwamba waliofanikiwa kuiba fedha za EPA walifanya hivyo baada ya kughushi.

  ``Na kughushi kwenyewe ni kosa la jinai, achilia mbali wizi walioufanya,`` alisema.

  Mbali na hivyo, Jaji Warioba alisema Watanzania wanayo haki ya kuwajua kwa majina watuhumiwa wa fedha za EPA na kujua kwa undani walitumia mbinu gani na kwa wakati upi, kutekeleza uovu huo.

  Alisema hekima za serikali, ambazo zimesaidia kurejeshwa kwa baadhi ya fedha, zinapaswa kupongezwa, lakini makosa kama hayo yanaweza kujitokeza tena siku za usoni, iwapo kosa hilo halitawekwa bayana.

  Jaji Warioba alisema kwa vile wahusika hao wamekubali kurejesha fedha hizo, na wengine wamepewa muda wa kuendelea kurudisha, ni wazi kwamba wamekiri kuhusika na kosa pamoja na kuiba.

  ``Hawa watu tunataka wajulikane na wakamatwe, itakuwa vigumu kubaini mbinu walizotumia kuiba na waliowasaidia, nje ya mahakama. Tukiacha hivi tutakuwa tumekalia tatizo ambalo linaweza kututafuna kama kansa siku zijazo,`` alisema.

  Alisema kwa vyovyote waliochukua fedha hizo, wasingeweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kiasi hicho, kama wasingepata masaada toka kwa maafisa wa juu.

  Hadi sasa baada ya kugundulika wizi huo kufuatia ukaguzi wa kampuni ya Ernst & Young, serikali ilimfukuza kazi aliyekuwa gavana wa BoT, Marehemu Daudi Balali, na makapuni husika yametakiwa kurejesha fedha hizo.

  Mwisho wa kurejesha fedha ni Oktoba 31, mwaka huu kabla ya Novemba mosi hatua za kisheria kuanza kuchukuliwa.


  * SOURCE: Nipashe
   
 2. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  usiwe na wasi wasi mkuu tutawafikisha mahakamani hao. ccm iko imara na inajua inachokifanya ni matter of time
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,882
  Likes Received: 83,364
  Trophy Points: 280
  :confused: Chama cha mafisadi kinajua inachokifanya!!!? Tangu lini!!!!?
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yeye mwenyewe yumo huyo
   
 5. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  yeye yumo kwenye kashfa ya mwananchi gold. na hii kampuni pia imechota hela BOT lakini siyo kwa mtindo wa EPA
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Sasa kama yeye yumo humo ndio wenzake waachwe? Hizo ni mbinu dhaifu za kulinda wahalifu. Kwa polisi makini mwizi akisema, "mbona mwenzangu Masatu hamumkamati, au akisema mbona wewe uliiba siku ile halafu leo unanikamata" anachekelea maana mwizi wake anakua amekiri kosa. Kuwa yeye anahusika si kinga kwa hao wengine na si kizuizi cha yeye kuwasema. Pengine anajiamini hana kosa na kama ana makosa apelekwe mahakamani atamwaga alichonacho.
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huko ndio kukurupuka... haya niaonyeshe niliposema waachiwe...
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,625
  Likes Received: 2,003
  Trophy Points: 280
  Naona mafisadi walikuwa wakijificha na the fact kuwa hata hapa marekani ufisadi umetokea na ndio umelifikisha Taifa hili hapa lilipo.
  Ila wenzetu wameshaanza kuchukuwa hatua na walishachukua hatua kama inavyojulikana kwenye Ken Lay na wenzake wa ENRON....
  Sasa kuna hao wengine waliopewa bail out nao wanachunguzwa na FBI sasa hivi...Mafisadi hawatakuwa na pa kujificha na ni kweli wananchi wanaweza kuanzisha mapinduzi kama wakiwa organized...Mabilioni ya dola zilizofujwa yatadaiwa na wananchi one day na hilo mafisadi wasisahahu.
   
Loading...