Warembo tumieni "likes hits" vizuri zisiwapumbaze

Warembo tumieni "likes hits" vizuri zisiwapumbaze

tajirijasiri

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
2,863
Reaction score
3,854
Baadhi ya Kina Dada warembo (si wote) wenye sura na maumbo ya kuvutia wanapumbazika sana na likes hits wanazopata kwenye mitandao ya kijamii Mara tu wanaporusha picha. Ikumbukwe kuwa Uzuri wa Sura na mvuto wa kimaumbile hufikia mwisho.

Tumieni likes hits kujijengea mahusiano mema na kuweka mitandao ya kibiashara na kiuwekezaji zaidi ili mjenge maisha ya baadae.

Kwa mfano kama unapata likes 100 kwa picha moja uliyoposti basi ujue kuna raia 100 wamependezwa na haiba yako yaani personality, sasa badala ya kijisikia na kujenga kiburi, dharau na majivuno, basi unaweza ukaitumia opportunity hiyo kujiunganisha kibiashara, kimasomo, kimaendeleo, kiuwekezaji, kiajira n.k. kwa ajili ya maisha ya baadae.

Warembo kumbukeni kuwa Mvuto wa Sura na Umbo hufikia kikomo.

Hizo likes unazopata leo hutazipata tena baadae. Acha dharau, acha kujisikia, acha majivuno kisa "likes". Tumia nafasi hii kuijenga baadae.
 
waache wasifiwe...

they were born to be awarded the likes
 
Ukweli mtupu, walengwa wabadilike na wafikiri mbele zaidi.
 
Hivi mdada akikuletea nyodo za maringo unamfanyaje??
 
Facebook inaboa siku hizi

Haina mvuto hata kidogo
 
Ngoja nitumie likes zangi za jf kuwachuna! Sijui itawezekana?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom