Waraka wasambazwa

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,791
4,679
Waraka mchafu wasambazwa
Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed, amewataka Waislamu nchini kutopumbazwa na ujumbe wa simu unaosambazwa na watu ukilenga kuwachonganisha na chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Iringa, Issa Mohamed alisema kuna kundi la watu kwa sababu wanazozijua wenyewe wameamua kusambaza ujumbe wenye lengo la kuichafua CHADEMA, huku wakijua huo ni uchochezi wa kidini.

Ujumbe huo ambao Tanzania Daima imeuona umeandikwa; "Wapendwa katika bwana tumejipanga vyema kuchukua nchi 2015, Haleluyaa. Operesheni vua gamba vaa gwanda itasaidia kuwatia mkononi Waislam. Uingereza na Ujerumani zimeahidi kuwapa vijana wetu mafunzo ya uongozi na ya kivita, tusiache maandamano kwani yanajenga chama zaidi, mawakala wetu waliomo ndani ya CCM na CUF wanafanya kazi vyema tuliyowatuma, vyombo vya habari vimeahidi kutubeba hadi kieleweke, watangazie waumini wetu kuwa ule mpango wa KICHUNGAJI unaendelea vyema kafiri kakosea namba sambaza ujumbe huu kwa Waislamu tujipange."

Issa alisema kwa sababu ya tishio, Serikali ya CCM na wapambe wake wameogopeshwa na nguvu ya CHADEMA katika mikoa wanayopita, hivyo wameamua kubuni mbinu za kuwachonganisha na wananchi pasipo kujua hali hiyo inaliangamiza taifa.
Alivitaka vyombo vya usalama kuacha ushabiki wa kisiasa na badala yake vifuatilie hiyo meseji kwa kuwa ni sawa na uchochezi mwingine.

Kiongozi huyo aliwataka Waislamu kuzifanyia utafiti kila taarifa watazopewa ili wasije wakajuta baadae. Wakati huo huo, Mkuu wa Operesheni Sangara katika ziara ya CHADEMA maarufu kama M4C inayoendelea, Benson Kigaila amesema kitendo cha serikali kuwaomba wasimame kupisha zoezi la sensa kimekuwa na manufaa kwao kwa kuwa wameweza kufanya kazi kubwa ambayo wasingeweza kama wangeendelea na ratiba yao.

Alisema wamefika katika kata 46 za majimbo ya Iringa mjini, Mufindi Kusini na Kaskazini na kutembelea zaidi ya vijiji 200 kwa ajili ya mikutano ya ndani na kukutana na wanachama.

"Hawa polisi na CCM ni makatibu uenezi wetu wametusaidia sana katika kutuomba tusimame kazi tuliyofanya, hakika watajuta kwanini walibuni mchezo wao huo," alisema Kigaila.
 
TCRA wanafurahia tu, ungekuwa ujumbe wa kumkashfu rais lazima watu wangekuwa kolokoroni
 
Currently our prayers is for GOD to really steady this radarless sinking ship.

Actually it's by HIS grace that it hasn't sink or explode by now, given the ceaselessly barrage from Kikwete and his party aimed to tore this country apart in order to buy a false security & dominance.

Folks, we are here for a reason. We are here to stay and prosper in free, developed and just country. Tanzania is for all Tanzanians.
 
baba yangu alinitumia sms yenye ujumbe huu,kiukweli ni mdini sana nikamwambia nakushukuru kwa kunipeleka shule nielimike

kwa ueleewa mdogo tu ni mbinu ya magamba unaytumiwa na magamba. kwa kuhofia MVC sidanganyiiki
 
mbona redio imani juzi kwenye kipindi cha kidokezo imewaasa waislamu kwamba meseji ni za uwongo kuna mtu anatumia kwa ajili ya manufaa yake.zipo kama tatu walizisoma.
 
Yaani Magamba hayajifunza chochote kupitia sensa juu ya mbegu ya udini waliokwishaupanda tayari? Kweli akili zao ni mfu.
 
Mtambo wa mwigulu alonunua yerusalemu umeanza kazi zake.

..itakuwa walipumzika pale chadema waliposhikilia bango sasa wameona kimya wameanza tena hata tcra hawana mpango wa kuutafuta pamoja pamoja na kujivunia kuwa wanaweza kuingilia mawasiliano yoyote.
 
Huko ni kama kumpiga chura teke, Watanzania wa sasa si wale wa 1947. Ngoja walete stori za mwandishi kujilipua halafu zile za Igunga kuchoma nyumba kisha kusema CDM sisi wajanja.
 
Naungana mköno na wanaosema haya ni mawazo ya Nepi,NCHEMBA na Kibajaji hawa kwa utashi wao linawahusu.
 
Tatizo Waislam wamekuwa watu wakutumiwa sana...kama Toilet paper vile ndo maana kila kitu huwa kinaelekezwa kwao.

baadhi yao sio wote wamekuwa wakitumiwa kama kondom ambapo mtu akitaka kuzini huitumia lakini akiisha maliza haja zake huitupa na huona kinyaa hata kuigusa,waislamu safi tusikubali kutumiwa kwa maslahi ya wachache.
 
hahaha siasa za majitaka bhanaa...wakati mwingine huwa najikuta nacheka alone
 
Waraka mchafu wasambazwa
Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Issa Mohamed, amewataka Waislamu nchini kutopumbazwa na ujumbe wa simu unaosambazwa na watu ukilenga kuwachonganisha na chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Iringa, Issa Mohamed alisema kuna kundi la watu kwa sababu wanazozijua wenyewe wameamua kusambaza ujumbe wenye lengo la kuichafua CHADEMA, huku wakijua huo ni uchochezi wa kidini.

Ujumbe huo ambao Tanzania Daima imeuona umeandikwa; "Wapendwa katika bwana tumejipanga vyema kuchukua nchi 2015, Haleluyaa. Operesheni vua gamba vaa gwanda itasaidia kuwatia mkononi Waislam. Uingereza na Ujerumani zimeahidi kuwapa vijana wetu mafunzo ya uongozi na ya kivita, tusiache maandamano kwani yanajenga chama zaidi, mawakala wetu waliomo ndani ya CCM na CUF wanafanya kazi vyema tuliyowatuma, vyombo vya habari vimeahidi kutubeba hadi kieleweke, watangazie waumini wetu kuwa ule mpango wa KICHUNGAJI unaendelea vyema kafiri kakosea namba sambaza ujumbe huu kwa Waislamu tujipange."

Issa alisema kwa sababu ya tishio, Serikali ya CCM na wapambe wake wameogopeshwa na nguvu ya CHADEMA katika mikoa wanayopita, hivyo wameamua kubuni mbinu za kuwachonganisha na wananchi pasipo kujua hali hiyo inaliangamiza taifa.
Alivitaka vyombo vya usalama kuacha ushabiki wa kisiasa na badala yake vifuatilie hiyo meseji kwa kuwa ni sawa na uchochezi mwingine.

Kiongozi huyo aliwataka Waislamu kuzifanyia utafiti kila taarifa watazopewa ili wasije wakajuta baadae. Wakati huo huo, Mkuu wa Operesheni Sangara katika ziara ya CHADEMA maarufu kama M4C inayoendelea, Benson Kigaila amesema kitendo cha serikali kuwaomba wasimame kupisha zoezi la sensa kimekuwa na manufaa kwao kwa kuwa wameweza kufanya kazi kubwa ambayo wasingeweza kama wangeendelea na ratiba yao.

Alisema wamefika katika kata 46 za majimbo ya Iringa mjini, Mufindi Kusini na Kaskazini na kutembelea zaidi ya vijiji 200 kwa ajili ya mikutano ya ndani na kukutana na wanachama.

"Hawa polisi na CCM ni makatibu uenezi wetu wametusaidia sana katika kutuomba tusimame kazi tuliyofanya, hakika watajuta kwanini walibuni mchezo wao huo," alisema Kigaila.

CCM ni mababa ya kutunga bhana, yale yale ya mwaka 2010 kwamba Slaa akiingia ikulu damu itamwagika! kwa hali hii na woga wa watz, sijui kama tutafika!
 
Classmate (Benson Singo Kigaila) hakika juhudi zako zinaonekana ndani ya CDM. Ongeza bidii kaka, CCM wanasahau ya kuwa.....mlango mmoja ufungwapo mwingine unafunguka.....
 
Back
Top Bottom