Waraka wangu wa kufunga mwaka kwa wanaume wa JF

Mara nyingi kunuka uke ni magonjwa, kama kuna mwanamke ambae hawezi kujisafi mpaka atoe harufu huyo ni changamoto. Uke wake mwenyewe bado utoe harufu kuhudumia familia ataweza?????

Tafakari, chukua hatua!!!
Asante sana shemeji
 
ni matumaini yangu hamjambo wapenzi wetu wa humu .kwanza nawashukuruni sana maana mitongozo yenu inatufanya tujione tunaishi .
waraka wangu wa leo ni kupenda kuwajibu kwa niaba ya wanawake wengi kuhusu malalamiko yenu ambayo nimeona kila siku mnaleta hapa kuhusu wanawake wenu kunuka sehemu zao za siri.
basi naombeni ni wa jibu kwa niaba ya wahenga wenzangu na nyie mkawaoneshe wapenzi wenu ili muendelee kufaidi mahusiano yenu
yafuatayo yafanyike ili kuepuka uke wa mwanamke kutoa harufu mbaya
1.acha kuvaa chupi/underwear,
kama huwezi kuacha kuvaa,basi fanya yafuatayo
epuka kuvaa underwear mpya bila kufua,pia jitahidi kuvaa underwear za cotton ,na hakikisha unazifua vizuri,na kuanika vizuri zikauke vizuri.acha kabisa kufulia maji yaliyobaki wakati wa kuoga kwanza hayo maji yanakuwa na sabuni zenye machemical maana masabuni ya wadada ya kuogea yanajulikana ni makali . chupi zifuliwe kwa maji safi na salama

2.epuka kuvaa vaa underwear kila saa asubuhi/mchana /jioni
toa muda mwili upumue
usiku unavaa ya nini? au wkend kama leo huendi mahali ,unavaa ya nini?

3.ukiwa period
hakikisha unabadilisha pedi kila mara ,kwa siku hata mara tano.pia chagua pedi quality .achana na mchina rahisi inaua.

4.ukiona dalili yoyote mbaya ukeni itibu mara moja .usisubiri ikolee

5.usijioshe kwa kuingiza vidole huko.,labda mara moja moja uingize ili kucheki kama kupo shwari. pia usipake sabuni au vipodozi vyovyote

6.epuka kuwa na wapenzi wengi.sufuria moja mara lipikie wali mara ugali mara kande lazima lipate kutu

7 epuka kutumia choo usichokijua
unaenda bar kujisaidia unajikalisha kama hicho choo ni cha baba yako sio? bora ukojoe mlangoni ila uwasafishie choo chao acha kujikalisha kalisha na kuinama kwenye mavyoo usioyajua.

8 hii namba nane italeta mjadala mwingine na mimi sitaki kuonekana muhuni ila kwa hayo saba ni rahisi tu kuzingatia na papuchi zenu zikawa salama
Mkuu, huu waraka ndio umeamua kutuandikia wanaume? Wallahi umemaliza mwaka vibaya Miss Natafuta
 
Back
Top Bottom