Waraka wa Wapagani - Draft | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa Wapagani - Draft

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zakumi, Aug 28, 2009.

 1. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Wengine sisi ni wapagani. Na kama inavyoonyesha kuwa interest groups mbalimbali zinajaribu kwa namna moja au nyingine kuandika jinsi ya kuongoza watu kwenye uchaguzi wa 2010.

  Ningeomba wale ambao hawana uwakilishi wa kidini au kwa wale wenye kutaka kutimiza wajibu wa kiraia bila kutumia makundi ya kidini tuandae draft na baadaye tutoe waraka wetu.

  Wenu Za10 MwanaMavungi.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hahahahahahaha,

  Za10,

  Wapagani bongo wanazidi 10% (all the animist and traditional religion upholders, tree worshipers etc)

  You almost got me started. Ila tatizo you are close but personally am not a pagan, more of an atheist, the two are not the same.

  Lakini kwa kuwa umealika wasio na uwakilishi wa kidini, nitaitikia wito wako vilivyo.

  Ila tusilaumiane tu.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mh!
  i mbombo ngafu!lakini zakumi ana point
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Sasa mbona mpagani mkubwa Kingunge yupo mstari wa mbele kupinga "waraka?".

  Mnahitaji muwekwe chumba kimoja msemezane....
   
 5. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Correction...a while back ulisema ww ni pagani...huamini dini yeyote naona leo umejing'ata ulimi....
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  LOL!

  Tatizo sio upagani au la, tatizo ni kuwa nchi kama ya Tanzania unashindwa kuelewa hata kama hizo dini zingine zipo, Churches and mosques are more like social clubs!

  Ndio maana ukifanya utafiti wa hizo nyaraka zo utajikuta wanaojiita wakristo na waislamu hawajasoma na wala HWANA MPANGO WA KUSOMA, BONGO TAMBARARE, KANISA NA MISIKITINI WATU WANAENDA KWA KUOGOPA WAZAZI AU JAMII INAYOWAZUNGUKA!

  Huo waraka wa wakatoliki ni wa wakatoliki na sio wa wawakristo wooote, hawajaanza KKKT, walokole, wasabato, huko kw waislamu hawajaanza huyu wa shia huyu wa shai!!!!!
   
 7. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #7
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi nikiwa mpagani mwandamizi naunga mkono.Napendekeza machache ya kuweka humo.

  Napendekeza kuwa tutoe waraka wa kipagani wa kuwaomba wananchi wawachague watu wasiokuwa na dini uchaguzi ujao.

  Tuwaeleze kuwa ,kwa kuwa Serikali haina dini mtu asiye na dini ndiye anafaa zaidi kuchaguliwa kuongoza serikali isiyo na dini.Wenye dini hawawezi kuongoza serikali isiyo na dini sababu fikra zao zimekaa kidini dini ndiyo maana wana muda wa kupoteza kwa kujadili mambo ya kadhi na nyaraka za katoliki badala ya kujikita kutafuta mbinu za kujikwamua kutoka katika umaskini.Tungekuwa na viongozi na wabunge wasio na kidini dini kama mambo ya kadhi ,hijabu mashuleni,nyaraka za katoliki n.k yasingethubutu kukanyaga serikalini ,kwenye ilani za chama wala bungeni kuzua mjadala.

  Tuwashawishi kuwa wakichagua wapagani watakuwa na uhuru wa kuabudu watakavyo na kutoa nyaraka watakavyo bila serikali kuwaingilia wala kuwaomba wajisajili au kupeleka hotuba au nyaraka zao serikalini kwani dini na siasa vitatenganishwa na hata kuapa mtu hatatumia biblia au kuruani.Dini zitawekwa mbali kabisa na serikali.Viongozi wa dini hawataalikwa kwenye shughuli za kiserikali na viongozi wa serikali hawataalikwa kwenye shughuli za kidini.

  Katika waraka huo inabidi tutamke wazi kuwa Kingunge Ngombale Mwilu hatumtambui kuwa ni mpagani kwa sababu hakukemea hoja za kidini zilipoingia kwenye ilani ya CCM,Serikalini na bungeni .

  Wapagani hoyeeeee.


   
 8. T

  T_Tonga Member

  #8
  Aug 29, 2009
  Joined: Jul 24, 2007
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa wapagani hawana kitabu wataongea nini wao naona wabakie kimya kwani wakristo wanacho kitabu biblia na waislam nao wana Quran sasa wapangani wana nini
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,582
  Likes Received: 1,949
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu kwasababu atheist tofauti na wapagani hawabelieve either in God or even miungu kama miti milima ama hata mizimu.Uhuru wa kutoa maoni under free speach unampa Za10 nafasi ya kuleta hoja hii,hatahivyo tunakuwa bias kama badala ya kufuata katiba na principles za uadilifu wa uongozi tunaweka issue za kutugawanya mbele,nchi haiongozwi na koran ama bible,ni katiba iliyowekwa ambayo imeridhiwa na wananchi na ambayo ndio muongozo wa nchi. Waraka uliotolewa na catholics ni guding principles tu wakati huu ambapo ufisadi ni kama fashion na mafisadi ndo wenye nguvu, sema tu siasa za divisions zinapenyezwa kwa maslahi ya itikadi flani ama hata binafsi tu kwa kutumia migongo ya imani nk. Ufisadi hauangalii wewe ni dini gani,jinsia gani ama kabila gani etc,ni tabia ambayo ni kama section ya dini nyingine ya tofauti kwasababu walio mafisadi ni wa dini tofauti ila they share something in common,lakini sio principle za uadilifu.Na kwa hivyo basi nampa zakumi changamoto na yeye aseme kuwa wapagani hawawezi kuwa mafisadi na ni kwa misingi ipi hiyo hawawezi kuwa mafisadi.Kingunge ni mpagani,lakini anatetea mafisadi,so instituon ya catholics imetoa changamoto na wanaojibu either wanawachukia wakatoliki,ama ni mafisadi na wanatetea zaidi maslahi ya chama na mafisadi wakiwemo na bila ya wao kuonyesha kuchukizwa ama hata kuchukua hatu...Wakatoliki wametoa hoja ambazo zinatakiwa zifuatwe na viongozi bila kujali dini kwani waliyoyasema hayana uhusiano na kutaka biblia ama dini yao ifuatwe ama hata muongozo wa kidini kwene Taifa,kama vile ufisadi unavyowaunganisha watu wa dini tofauti,kwanini uadilifu usiwaunganishe viongozi ambao ni wazalendo wanaoweka maslahi ya Taifa mbele?
  Tonga message hii pia iko aimed to answer or comment ur posting,we should judge the content and not veerering towards religious conflicts kwani ufisadi hauna dini,hilo liko wazi.
   
  Last edited: Aug 29, 2009
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Kingunge sio ndo kiongozi wa watanzania wapagani?????
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  And where is pundit?????????i think he is one of them........
   
 12. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  BluRay:

  Lugha yetu bado unaupungufu wa misamiati kuelezea makundi mengine na ndio maana usipokuwa mkristo au mwislamu unaweza kuitwa pagani au kafiri. Lakini Tanzania kuna bahai, hindu, Zorostrian, imani za kikabila, spiritual..............

  Hivyo point kubwa ni kuandika waraka kwa kutumia uraia na haki za kiraia na historia ya nchi.
   
 13. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mfano huu ni sawa na kusema kuwa wakatoliki wote wamekubaliana na waraka wa wakatoliki.
   
 14. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Waberoya:

  Unajua nchi yetu ni nchi ambayo imejengwa kwa utamaduni wa oral traditions. Ni miaka ya hivi karibuni literacy traditions zimeanza kuingia. Hivyo katika maisha yetu makubaliano au mazungumzo ya mdomoni yana nguvu sana kuliko mambo yaliko kwenye makaratasi.
   
 15. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  sio lazima kuwa na kitabu,watakopi na kupesti[kama wengine wanavyofanya] na labda kubadili baadhi ya maneno yaendane na upagani
   
 16. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kingunge anapinga waraka sababu yeyete ni mpagani, na muda si mrefu atakuja na waraka wake binafsi kuwakilisha wapagani na wale wasiofungamana na dini... lol
   
 17. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tunangojea waraka wa MAFISADI tuone wametayarisha pesa kiasi gani kununulia kura 2010
   
 18. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2009
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani hii itakua hatua nzuri na waprotestanti,wasabato,walokole nao watoe mwongozo.Pia sio vibaya wavuvi,wakulima,wafugaji,machinga, wanamuziki na makundi mengine kwenye jamii nao wakatoa vipaumbele vyao.
   
 19. Z

  Zurich Member

  #19
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Lakini na mimi kama mwana JF nitoe mawazo yangu, nafikiri watanzania tusiogope kuona yale yanayokwenda kutokea katika nchi muda si mrefu,(kupatikana kwa UKOMBOZI au UHURU), ingawa nasikitika kusema kuwa lazima tutapitia wakati mugumu kidogo, na pengine wako ambao wanaweza poteza maisha kama ambavyo tayari tulivyokwisha poteza baadhi ya ndugu zetu waliosimama kwa ujasiri kutetea maslahi ya watanzania sina haja ya kuwataja maana badhi yao tunawakumbuka. Ila damu zao zitaendelea kuwapa ujasiri watu wengine kupinga ufisadi au fikra za kidini kama ambavyo serikali hii ya kikwete ilivyojitahidi kupalilia haya mambo.

  Ni historia pekee ndio itatufanya aidha tupate ukombozi kwa amani au kwa gharama ya juu(watu kupoteza maisha), Amerika ina misingi yake hivyo hatuwezi kujilinganisha nayo na pia South Afrika nao wanahistoria yao na tunapoona leo hii wanafurahia matunda kuna gharama iliyowahi kulipwa huko nyuma.

  Viongozi wetu wa sasa katika serikali hii, nawashukuru sana maana kwa upofu walionao, ndio utakuwa mwanzo wa Tanzania, au Tanganyika mpya kwa yale waliopalilia na sasa yamekomaa. Mimi naona hayo yote yanayotokea katika nchi yetu, zikiwemo nyalaka za wakatoliki au waislamu, au na mambo mengine mengi tu ambayo yametokea katika nchi yetu na tutashuudia mengi yakitokea ni harakati za ukombozi. Ila naomba niweke angalizo kwa wanaotetea dini zao, Mungu hana dini, watu wote wana thamani mbele zake, tena kifo cha mwenye dhambi Mungu hafurahii kabisa, lakini kama mtapenda kuendeleza mijadala ya dini, na nyie pie mjue mnafanya gharama ya kupata uhuru kuzidi kuwa kubwa kwa yale yatakayo tokea hapo mbele. Siwalaumu lakini, ingawa mnachochea mafuta na kuongeza ukali na ugumu wa njia tutakayoipitia na mwisho wa yote, watanzania walio wengi watashinda vita hii.
   
 20. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Kila watu watoe waraka wao,mabaa medi,vyangudoa,mashangingi ya mjini,wasanii wa bongo flavour,watangazaji wa vipindi vya taarab,mateja,wapiga debe,n.k
   
Loading...