Tatizo hapa si muisilamu au Mkristo, cha muhimu ni kupata uongozi utakao kua responsible, visionary, creative, understanding n.k regardless ya dini yake.
Sasa tutapataje kama kunakuwa na kura za kundi maslahi la kidini?
Mwaka huu mtajiuliza sana.
Sasa tutapataje kama kunakuwa na kura za kundi maslahi la kidini?
Changa akili yako rafiki.
kwa hiyo wewe unafurahia hili? kama ndiyo, huna mapenzi na nchi yako na umetanguliza dini na ubinafsi.
Baija Bolobi!
Yanapokuja malumbano ya kidini naomba nisichangie kwani katika makuzi nilifundishwa kuheshimu kila mtu linapokuja swala la imani kwani tulio wengi hatujawahi kuchagua tuwe waislaam au wakristo inategemea tu ulipozaliwa wazazi wako walikuwa dini gani.
Huo waraka sijausoma ila nimeguswa na bei inayouzwa Shilingi 2000 nakala moja? isije kuwa kuna wajanja wameanzisha DECI kwani kila penye mauzo yatakiwa risiti na kodi ya KAISARI ikusanywe au nakosea!
Hivi ule waraka wa WARUMI(Wakatoliki) ulikuwa unauzwa bei gani au ulikuwa bure. Sitaki kulumbana na Mashehe nisije somewa dua mbaya.
Hivi ni waislamu wangapi wanaweza kulipa elfu mbili kununua waraka badala ya kuongezea na kununua futari. Nisameheni tena huu ni mwezi wa toba kuna haja ya mpambano au kuganga njaa ili wajanja fulani wapate vijisenti vya kuserebuka kwenye sikukuu za Eid Mubarak !!! Huo waraka si ungetolewa baadae au uchaguzi ni Oktoba 2009.
Kuuliza sio ujinga ila ni kutaka kuelimishwa.
Mkereme
Waraka wa WARUMI haukuuzwa, ulitolewa bure na ulilenga waumini wao.
Hii habari ya wajanja hata mimi naona kuna hatari ya kuwa tunatumiana ili kuganga njaa ya watu. Lakini nisiseme mengi, maana sisi tulio bara tumeambiwa tutaletewa na hatukuambiwa tuandae fedha.
I say jamani, naona wengi mnafanya masikhara. Hili sio jambo la kutaniana. This is the beginning of the end of Tanzania!!!! Nauza nyumba yangu iliopo DSM ili nihame mapema. Najua damu itamwagika tu nchini kama kufa. It's too late for JK. Yote kwasababu kawakumbatia mafisadi. Uganda yanaendelea, Kenya yashatokea, Unguja ndio yamebakia mpaka leo. Sasa ni zamu yetu wadanganyika nasi kuchinjana!!!
Mwenye akili ahame kama mimi ninavyohama nchi hii hii leo!!!
Huo ni waraka au Mwongozo au fatwa? Hao akina Ponda, Kundecha et al kwa upande mmoja wanaamua kulumbana na Wakatoliki halafu upande mwingine BAKWATA haikubaliani na akina Ponda na wenzie. Halafu Wakatoliki wanalumbana na Kingunge ambaye kwa nia ya hoja tuseme anaiwakilisha NEC ya CCM. Hii equation imekaa vipi?
P vis a vis K vis a vis CCM + K vis a vis CCM+B vis a vis P= Political environment in Tanzania. Where as P=Ponda at al; K=Katoliki;CCM=Kinguge and NEC;B=BAKWATA.
Niambieni hii imekaeje? Nani atakaekuwa mshindi au kubakia na nani atakuwa cancelled out. Mimi naona hii ni kama sinema ya Ze Komedi. Mnasemaje wachambuzi?
Kwa hiyo Serikali inatakiwa ifuate MWONGOZO la sivyo hawatapewa kura au namna gani? Au tuseme kama atatokea mwanasiasa mwenye kuukubali MWONGOZO ndiye atakayepewa kura? Tunamsubiri mzee 'no comment' kikongwe wa kikomunisti Kingunge, mzee wa 'hapa patamu' Makwaia wa Kuhenga na 'bwana madevu' maalim Seif kuupinga waraka huo kama walivyoupinga ule wa Kanisa Katoliki otherwise tutakuwa tumewajua janja yao ililenga kwenye nini!
Ushauri wangu kwa maaskofu na wakristu ni kufanya kampeni za waziwazi makanisani kwamba tuchague wakristu wenzetu tuu.
Tueneze kampeni zaidi na kwa wapagani, hindu,n.k(exclude wajahidina).
Hii move ita work sana tuu.
Liwalo na liwe, kama ni noma na iwe noma.
Sasa tutapataje kama kunakuwa na kura za kundi maslahi la kidini?
Simoni hujui nani atashinda?
CCM itashinda, cha kushangaza zaidi watarudi mafisadi walewale.
Pia utakuwa mwisho wa CUF Tanganyika.