sonofobia
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 1,249
- 4,537
Miongoni mwa sababu walizozitoa G-55 katika waraka huo ni pamoja kwamba wanaona haiwezekani kuzuia uchaguzi ikiwa si washiriki, badala yake wanapaswa kushiriki na kuzuia kwenye vituo vitakavyoonekana kufanyika ubadhilifu.
Licha ya viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuweka msimamo wa kuzuia uchaguzi, watia nia 55 wa ubunge maarufu’G-55’ kupitia chama hicho, wamelipinga hilo wakitoa sababu tisa za uamuzi wao huo.
Watia nia hao 55, ndio wale ambao kuanzia juzi, jumbe zao katika kundi la WhatsApp zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikionyesha mipango yao ya kuwasilisha pingamizi la msimamo wa chama hicho.