PreGE2025 Waraka wa wagombea 2020 na watia nia wa ubunge 55 wa CHADEMA. Wapinga chama kususia uchaguzi mkuu

PreGE2025 Waraka wa wagombea 2020 na watia nia wa ubunge 55 wa CHADEMA. Wapinga chama kususia uchaguzi mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

sonofobia

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
1,249
Reaction score
4,537
Miongoni mwa sababu walizozitoa G-55 katika waraka huo ni pamoja kwamba wanaona haiwezekani kuzuia uchaguzi ikiwa si washiriki, badala yake wanapaswa kushiriki na kuzuia kwenye vituo vitakavyoonekana kufanyika ubadhilifu.

Licha ya viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuweka msimamo wa kuzuia uchaguzi, watia nia 55 wa ubunge maarufu’G-55’ kupitia chama hicho, wamelipinga hilo wakitoa sababu tisa za uamuzi wao huo.

Watia nia hao 55, ndio wale ambao kuanzia juzi, jumbe zao katika kundi la WhatsApp zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikionyesha mipango yao ya kuwasilisha pingamizi la msimamo wa chama hicho.

1001073848.jpg

1001073849.jpg


1001073850.jpg


1001073851.jpg

1001073858.jpg


1001073859.jpg

g55.jpg
 
Daah hawa jamaa wameamua TU kua against na uongozi huu maana hata ukiwauliza hoja ziko wapi wanatoa macho tu.
Hawa hawajatumwa na CCM ila kwa kiburi chao wameamua kufanya KAZI ya CCM bila kulipwa ili kujarbu kuonyesha uongozi mpya wao ndio alfa na omega.


Wengine walitoa miez2 lakini wanaona mwezi wa3 huu Ngoma ndo kwanza inaanza kupaliliwa na harakati bila wao zinasonga Tena bila ya makando kando,wakaona wajikusanye kama Intarahamwe.

Nashauri wapuuzwi na kama watatokea wenye viburi zaid basi watawafata Covid-19.

Cdm haijawahi kua chini ya mtu,CDM ni chama chemye sura ya kitaifa sasa na kila mwenye kutaka mabadiliko anakimbilia CDM na ndo mana hawataki hata wanaharakati wajihusishe na CDM(😄😄).

LISU NA HECHE kazeni milio imeanza kuskika,hao waachieni kina Mnyika na Lema watadili nao
 
Katiba inatoa uhuru na haki. Kikundi cha watu wachache wanaminya uhuru huo..

Azimio la mafichoni aliipo ndg yetu Maria lilikuwa la no reforms, no election. Likiwa na ujumbe na mikakati yake, lakini kigenge cha watu wachache walio Anza kulewa madaraka mapema wamepindua dhima kuu na kubakia na sura ile ile ya kondoo kumbe ni mbwa mwitu

Muda ndio msema kweli. Je, uchaguzi utafanyika?
 
Tukiweka mahaba pembeni G55 wana hoja zenye mashiko.
Sasa tukishiriki alafu 90% wakaenguliwa na bado Tusipewe jimbo hata moja ndio ina maana gani?

Hata odinga alisusia uchaguzi wa marudio 2017 same to CUF walisusia uchaguzi 2016 na wala Seif hakupoteza chochote.

Kuna wakati lazima mjitoe ufahamu ili mabadiliko yaje otherwise tutaendelea kupelekeshwa.
 
Ndugu zangu, mikutano ya kisiasa ilikuwa imezuiliwa sivyo?

Je, ni nani aliyeandamana ama aliyekinukisha hadi ikaruhusiwa?

Je, ni kwanini akili ileile ishindikane sasa?

Nchi ina umasikini wa kutisha unapokinukisha, unaamini hiyo siyo njia ya milele ya kuondosha amani nchini?

Ninyi mnaosapoti mambo ya kutumia nguvu, fikirieni sana mara 2, 2.
 
Hawajakatazwa waende vyama vingine, huku kwetu "if no reform, no election" sentensi moja tu, mbona inaeleweka, wanataka kugombea CHADEMA waungane na wenzao ili kuhakikisha tume huru inaundwa, kama wao wanataka kugombea katika tume hii hii wawafuate akina Msigwa
 
Sasa inakuaje wanasema ni agenda ya lisu, aisee kukosa ulaji ni shida sana
Wajinga hao ni wa kupuuzwa Hoja yao haina kichwa wala miguu

NO REFORMS NO ELECTION ni Agenda na msimamo wa chama.

Kama wametumwa na Makala wakamwambie NGOME ya CHADEMA haipenyeki.
 
Back
Top Bottom