Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,574
- 19,457
Zamani sana kulikuwa na rafiki yangu alikuwa anakwenda Bukoba kikazi. Alikata ticket ya basi kutoka Mwanza siku mbili kabla ya safari, na kupata kiti. Siku ya safari jamaa akawahi akapandisha mizigo yake na kukaa kwenye kiti chake akisubiri safari ianze. Muda mfupi kabla ya safari kuanza, akaja mzee mmoja wa kihaya naye anataka kusafiri wakti huo huyo; ikabidi kondakta amfuate jamaa yule na kumurudishia hela yake ya nauli huku akimshurutisha atelemke, na mizigo yake pia ikatelemshwa. Jamaa akakosa safari aliyokuwa ameipanga kwa siku mbili, ila tatizo lake aliingia basi la wahaya wakati yeye siyo mhaya.Kwa nyumba nzuri vijijini hawana mpinzani kuna mahekalu kwenye migomba mengine hata masaki yanastahili ,tatizo mjini tu,ukifungua duka kama hujui kihaya utakoma,anakuja mteja. Iwe ndetela akananka aiko,kama hujaelewa kesho haji hapo anajua huyu mnyamahanga