Ngambo Ngali
JF-Expert Member
- Apr 17, 2009
- 3,517
- 1,359
Prof Mark Mwandosya, waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mbunge wa Rungwe Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM, amefunguka na kutoa waraka murua na wa ukweli kuhusu demokrasia. kitabu hicho kinaitwa Sauti ya Umma ni sauti ya Demokrasia.
Katika waraka huo Professa anatuelezea kuhusu mchakato wa uchaguzi wa CCM mkoa wa Mbeya 2007.
Katika kitabu hicho anatufundisha:
1. Makundi yaliyojitokeza katika uchaguzi wa CCM Mbeya 2007 yalitokana na utupu wa kiitikadi,uliozaa makundi ambayo hayana msingi.
2. Kuna hatari kubwa ya wafanyabiashara kubadili umiliki wa chama, kutoka chama cha wakulima na wafanyakazi, kuwa chama cha wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara,wafanyabiashara ambao sasa inajitokeza kuwa watataka au watafanikiwa kukiongoza chama kutokana na uwezo mdogo wa wa vyama vya siasa.
3. chama kirudi katika misingi ya uongozi bora inayokataza matumizi ya fedha katika kuwashawishi wajumbe wa kikao cha uchaguzi kumchagua mgombea au anayewania kugombea nafasi katika chama.... Matumizi ya fedha kwa namna hiyo ni ishara tosha kwamba mgombea hafai kuwa Kiongozi.
4. Kitendo cha wasimamizi wa uchaguzi ( wa chama) kusahau, kuacha au kupuuza jukumu la usimamizi wa uchaguzi ni kielelzo cha kutokuwepo au uhafifu wa mafunzo ya uongozi na utawala kwa viongozi wetu.
Publisher: not disclosed
ISBN: not disclosed