PostGE2025 Waraka wa Martin Maranja kwa serikali ya Tanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Think2

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2025
Posts
2,193
Reaction score
3,957
Katika orodha ya watu wote waliokamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za makosa ya uhaini na makosa mengine kutokana na maandamano ya 29/10/25 hakuna raia wa kigeni hata mmoja katika hati ya mashtaka

Hii dhana kwamba walioandamana walikuwa wageni inatoka wapi? Wageni gani ambao wamekamatwa na kushatakiwa kwa mambo ambayo yanatokana na maandamano yaliyofanyika tarehe 29/10/25?

Kwamba walioshiriki maandano hawakuwa wanazungumza kiswahili. Hao waliokamatwa na kushtakiwa wote wanazungumza kiswahili. Hao wasioweza kuzungumza kiswahili wapo wapi?

Je, waandamanaji hao ambao hawazungumzi kiswahili ni kati ya hawa waliokamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini au wale waliouwawa kwa kupigwa risasi na wengine miili yao haijulikani ilipo hadi sasa?

Kwamba waandamanaji walikuwa na silaha za moto? Kwamba waandamanaji wameuana wenyewe kwa wenyewe? Hii mnataka kumdanganya nani? Washirika na wadau wa maendeleo kutoka nje au Watanzania?

Katika waandamanaji waliokamatwa na kushtakiwa katika mahakama mbalimbali hakuna hata mmoja amekamatwa na bunduki. Hizo silaha za moto walizokuwa nazo ninyi mmezitunza wapi sasa?

Bila kujua, mnalidogodesha Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambao tangu siku ya kwanza ya maandamano askari wake walikuwa barabarani. Kwamba wakiwa barabarani walishindwa kudhibiti watu wenye silaha za kivita?

Mnataka kusema kwamba, hao watu waliokuwa na silaha za moto walikuwa wanavuka vizuizi vya JWTZ wakiwa na silaha hata baada ya kutangazwa amri ya kutokutoka ndani? Hivi mnajisikiliza kweli?

Unasema hakukuwa na maandamano kwa kuwa waandamanaji walikuwa na silaha za kivita. Halafu unasema wengine wamepoteza maisha bila kushiriki. Kwanini mmewaua ambao hawakuwa na silaha?

Hata hivyo, mnajaribu kutuonesha wananchi kwamba mipaka ya nchi yetu haipo salama hadi kuruhusu watu kutoka nchi jirani kuvuka na kuingia na silaha za moto? Idara ya uhamiaji ivunjwe na kufutwa mara moja.

Kwamba watu hao waliingia nchini wakiwa na silaha za moto na kusababisha madhara kwa binadamu, walitumia mipaka na Airports? Serikali ipo? Intelejensia yenu ya kuzuia mikutano ya kisiasa mliuza wapi?

Kujaribu kutupa hizi lawama kwa majirani ni kutafuta mgogoro wa kidiplomasia usiokuwa na lazima. Lipo tatizo, litatuliwe. Wasikilizeni wananchi, hususani kundi hilo la vijana. Msiendelee kukaa kwenye denial.

-AMEANDIKA MARTIN MARANJA MASESE
 
Ni ujinga fulani hivi sijui tuuiteje hata kuna vitu mtu anaongea unajiuliza huyu anaongea Nini ?!
 
Cyprian Nyakundi huko X kawaaambia ukiona umechimba shimo na kuingia jizuie kujichimbia zaidi shimoni! sasa sijui hii serikali ya Form Four Failure kama hata inaelewa
 
Viongozi wetu sio kwamba hawajui kuongoza ni kwamba hata akili ya kufikiria na kujenga hoja hawana , Nchi haiwezi kuendelea Kwa kuongozwa na akili kama hizi , kama hii ndio akili ya ya PM vp kuhsu RC,DC,diwani, wenyeviti mpka mabalozi .Nchi yetu imeoza we need to change the whole government structure from president to stret chairman's.
 
Attachments

  • Screenshot_20251108-110457.png
    Screenshot_20251108-110457.png
    93.9 KB · Views: 8
Viongozi wetu sio kwamba hawajui kuongoza ni kwamba hata akili ya kufikiria na kujenga hoja hawana , Nchi haiwezi kuendelea Kwa kuongozwa na akili kama hizi , kama hii ndio akili ya ya PM vp kuhsu RC,DC,diwani, wenyeviti mpka mabalozi .Nchi yetu imeoza we need to change the whole government structure from president to stret chairman's.
Chalamila huyu hanaga ubongo kbs 😂
 
Hivi Kenya walishawahi kutusingzia kwenda kuunga mkono maandamano nchin kwao?
 
Kikao cha Jumuiya wakati ujao kitakuwa cha moto sana.

Lazjma hiyo ajenda ijadiliwe na watu waotoe ushahidi.
 
Back
Top Bottom