Waraka wa Kibanda kabla ya kufikishwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka wa Kibanda kabla ya kufikishwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mnyakatari, Dec 18, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Mhariri mtendaji wa Tanzania daima bw.Absalom Kibanda ataripoti tena polisi kesho na ikiwezekana ataburuzwa mahakamani. Huu ni muendelezo wa kesi inayoitwa ya"Uchochezi" kufuatia ile makala ya Samsoni Mwigamba kwa jeshi la polisi. Ikiwa imebaki masaa machache kabla ya kuripoti polisi Kibanda ameandika yafuatayo kwenye ukurasa wake wa facebook:

  "Kesho saa 3:00 asubuhi natarajia kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam tayari kwa lolote, kubwa likiwa ni kuburuzwa kortini Kisutu kusomewa shitaka la uchochezi. Hatua hii inakuja siku tatu tangu niliposhikiliwa , nikahojiwa, nikatoa maelezo yangu na kisha nikawekewa dhamana na rafiki na mdogo wangu, Saed Kubenea.

  Taarifa tulizozipata kutoka kwa viongozi waandamizi serikalini ambao wanatutakia mema zinaeleza kwamba limekuwapo shinikizo kubwa kutoka kwa wakuu wa dola la kutaka mimi ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima nifunguliwe mashitaka ya Jinai kama njia ya kujibu hasira za wakubwa dhidi yangu binafsi na dhidi ya gazeti la Tanzania Daima ninaloliongoza.

  Habari kwamba nilikuwa miongoni mwa wahariri waliokuwa wamewekwa katika orodha ya kufikishwa mahakamani kwa makosa ya jinai na siyo ya madai kama ilivyo ada tulielezwa miezi kati ya mitatu na minne iliyopita. Taarifa hizi zilitolewa na mmoja wa mawaziri kwa mmoja wa wahariri ambaye ni rafiki yake mkubwa.

  Baya katika uamuzi huu si kwamba anayeshitakiwa ni Absalom Kibanda, ambaye ni Mhariri wa Tanzania Daima na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri la hasha, bali ni uamuziwa hatari wa baadhi ya viongozi wa serikali ambao wameamua kuminya uhuru wa kikatiba wa watu kutoa maoni yao.

  Uamuzi huu wa sasa wa kuanzakuwashitaki wahariri kwa makosa ya jinai yanatukumbusha maneno ya Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye aliyetabiri kwamba kiongozi anayesaka umaarufu na ikulu kwa njia ya vyombo vyahabari akiingia madarakani atalinda himaya yake kwa risasi.

  Ni wazi kwamba dhamira ya kupambana na watu wanaokukosoa wewe binafsi au serikali yako kwa njia ya kuwakomoa au kuwaumiza si tu ni udikteta unaofanana kimantiki na wa zama za Adolf Hitler bali unadhihirisha namna tulivyo na madikteta wanaofichwa na uhuru wa kidemokrasia waliokuta ungalipo hata kabla hawajaingia madarakani.

  Hatua ya kulitumia Jeshi la Polisi kukandamizi uhuru wa habari kwa kuwakamata waandishi wa maoni kama walivyofanya kwa Samson Mwigamba wiki iliyopita na wahariri wa magazeti kama inavyofanyika kwangu haina budi kupingwa kwa matamko na kwa njia nyingine za kudai haki iliyowekwa rehani.

  Hakika kama taifa tupo njia panda. Nimeamua kwa dhati kulitumia tukio hili kama somo kwa madikteta wa Tanzania na wengine wa Bara la Afrika. Nimehamasishwa kujitoa mhanga kuleta mabadiliko ya kweli ya uhuru wa habari na wawatu kutoa maoni yao pasipo kuvunja sheria. Ukisoma makala ambayo imewapotezea polisi, mahakama, magereza na wapendwa wetu muda adhimu huwezi ukaamini kwamba tuna viongozi wanaofikiri sawasawa.

  Ni hatari kuwa na kiongozi mkuu aliye tayari kuumiza watu wadogo kama sehemu ya kupumua au kupunguza hasira na machungu yake moyoni ambayo yamesababishwa na kupwaya kwake au kushindwa kwake mwenyewe. Ni aibu kuwa na viongozi dhaifu ambaokwao kuumiza wengine ndiyo kipimo cha nguvu za kikatiba walizopata tena kwa njia ya sanduku la kura.

  Kama kweli tunalitakia mema taifa hili hatuna budi kuanzisha mapambano makali ya kupigania uhuru ambao sasa umewekwa rehani. Wanahabari na wanahabari tunapaswa kujitoa mhanga kuyaongoza mapambano haya mapya".


  +++++++++++++++++
  Habari zilizopatikana kutoka Mahakama ya Kisutu zinasema tayari Kibanda ameshafikishwa mahakamani hapo tayari kwa kuunganishwa katika shitaka alilofunguliwa mwenzake Samson Mwigamba.
   
 2. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Kiukweli ukisoma na kutafakari maneno haya ya Kibanda unapata picha halisi ya watawala wetu wa sasa..!
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kibanda,to be honest nyie waandish ni vibaraka wa politicianz,huwa mnanunulika kwa bei rahis sana na wanasiasa,kwani salva yuko wapi?sasa hili ni somo kuwa wanasiasa si marafiki
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mnyakatari,hata kibanda asemeje?ukwel uko palepale journalist wa tanzania wanajal matumbo yao tu!
   
 5. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Truth well said,the Ex soldier is mentally corrupted and only external forces(nguvu ya umma) will do than fake democracy of barrot boxes.
   
 6. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Viongozi wengi hupenda pale wanapopambwa kwa maneno matamu yenye kuwatukuza na kupambwa kwamba wao ni zaidi hata ya mitume,hupenda kuonyeshwa kwa mema tuu, pole ndugu zangu wahariri hao ndo wale mliosema ni chaguo la Mungu
   
 7. d

  dada jane JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini yana mwisho kama alivyosema Rashidi.
   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mwisho ni pale waaneish watakapokataa ushoga na wanasiasa
   
 9. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Nyie ndio mnao-define vibaya uhuru wa habari.

  Toeni/pokeeni habari ila msivuke mipaka.
   
 10. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  mipaka ipi? au nini maana ya habari?
   
 11. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Hizi ni dalili za anguko kuu la serikali legelege ya ccm
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mpaka upi uliovukwa,?mwaka huu hata gazet la mwananch lilitishiwa,MCT wakaja wakasema halina makosa,dola hupenda kusifiwasifiwa tuu,
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  waandishi wamepanda mbegu amabyo sasa inawatafuna
   
 14. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Huyo anatumiwa na Chadema hana lolote. Hatupo tayari kuvumilia uchochezi wa aina yoyote ile.
   
 15. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Kila kona ni malalamiko, uonevu na mateso. Muda sio mrefu tutapambana bila hata ya kuagizwa na yeyote..
   
 16. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hilo ndo naloliona,kila mwandish ana mwanasiasa wake,hawatak tena kuwaandikia wananchi!
   
 17. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kibanda~tulia usipanic! Hao wote wanaokubughudhi siku yao yaja nayo sasa ipo! Ambapo kila mmoja atajutia maamuzi kandamizi aliyowahi kuyafanya ndani ya sayari hii iitwayo dunia. Na hii itakuwa kuanzia kwa mkuu wa kaya hadi kwa mwokota makapo barabarani. Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha! Nao mwisho wao mabeberu, wasandiki, mafisadi, waonevu, wakandamizaji na wasiyo jali uko mlangoni!!!
   
 18. k

  katatuu JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Waandishi wachache wanaharibu sifa za wenzao
  .Aacha kulalama sasa aende akavune alichopanda.sheria za nchi lazima zilindwe.huo ndio ukweli wenyewe.
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kila mtu analaumiwa,
  kama walimlaumu tido watashndwa kwa Kibanda?
   
 20. d

  dada jane JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  leo wenzio hawapo
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...