Na Yule Mhariri wa Gazeti la serikali aliyeandika wakati wa uchagu yakwamba kamwe DR SLAA atokuwa RAISI anafikishwa lini mahakamani? na matusi wanayotukana baadhi ya watangaji wa clouds FM kuna hatua zimechuliwa? au hii ni CCM vs CHADEMA waje wazi wazi basi wanajificha nini?
Kama ni kweli na serikali inataka kumshukia Kibanda ili kuithibiti kasi ya EL, then imechelewa!. Hawatamweza EL, huwezi kuizima cheche ya moto wa nyikani kwa kuipulizia upepo kama kuzimavyo mshumaa au njiti ya kibiriti!.poor wahariri.....ukiacha mwananchi/citizen wengine wote hamna mnachokifanyia nchi hii...majungu tu, acheni mmalizane wenyewe..
Kibdana ni mtoto wa EL....hii vita haiko inavyodhaniwa
Wajameni kwa msiojua, huu ni utekelezaji wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo ni moja ya sheria kandamizi na imo kwenye ile list ya sheria 40 ambazo Tume ya Nyalali ilishauri zifutwe.Tayari habari zisizothibitishwa zinataja baadhi ya wahariri walio kwenye orodha ya kukamatwa na kushitakiwa katika mkakati wa serikali kutumia polisi kutisha waandishi wa habari na wakosoaji wengine wa serikali.
Hata kabla ya Jukwaa la Wahariri kutoa tamko lao, vyanzo kadhaa vya habari serikalini vililidokeza gazeti hili kwamba polisi wanatekeleza mpango huu kwa amri ya wakubwa wanaokerwa na ukosoaji unaofanya na baadhi ya waandishi, wanasiasa, wanaharakati na vyombo vya habari.
Wajameni kwa msiojua, huu ni utekelezaji wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo ni moja ya sheria kandamizi na imo kwenye ile list ya sheria 40 ambazo Tume ya Nyalali ilishauri zifutwe.
Ninachokiona sasa ni kwa serikali kifanya double standards kwa kuwalenga inaowatafuta na kuwaacha kujivinjari inao wasupport.
Tusimlilie Mwigamba na Kibanda, bali tupaze sauti zetu sheria hii isitishwe kitumika na badala yake sheria mpya ya habari yenye haki ya kupata habari ambayo serikali wameikalia tangu mwaka 2003, sasa iletwe bungeni na kuireplace hiyo Newspapers Act of 1976.
Tena tushukuru Mungu kwa miaka hiyo yote, serikali haikuwahi kuitumia sheria hii ipasavyo kwani kama ingetumika huko nyuma, magazeti kama Mwanahalisi, Raia Mwema and the like yaliyojikita kwenye ukosoaji wa serikali, yangekuwa ni hadhithi tuu kwani yangeshafungiwa zamani!.
Nionavyo mimi, lengo la serikali kwenye hiki kibano kwa Mwigamba na Kibanda tena watamuunganisha na printer, Mwananchi Communications, ni kutuma salamu kwa wahariri wote kuwa very carefull na contents za magazeti yao kwani sheria hiyo bado ipo!.
Kitendo cha kumuunganisha printer kama sheria inavyosema ni kuhakikisha wachapishaji wanakuwa resiponsible na contents hali itakayopelekea kususa kuchapisha baadhi ya magazeti yatakayo leta burning issues!.
Nimesema serikali inafanya double standards ili tuu kutishia nyau uandishi critique!.
Bado sijajua Mwigamba anatetewa na nani, ila wanasheria watetezi wa Kibanda, Nyaronyo Kicheere na Juma Thomas, wote ni wanahabari/wanasheria waliofikia level za editors Nyaronyo akiwa mhariri wa Citizen na Juma Thomas alikuwa mhariri wa the Guardian, natumaini waitumia kesi hii sio tuu kuonyesha jinsi sheria hiyo ilivyo mbaya, bali kumconvince jaji pia atoe order sheria hiyo iwe scrapped off from the books of law!.