Waraka Wa Jaji Warioba kwa Wassira

Waraka Wa Jaji Warioba kwa Wassira

Kuna wengi hawajatambua hekima na njia aloipitia Jakaya, ni kweli alilipa visasi vingine bila yeye kupenda, aligombanishwa na wengi kwa kuamini sana type ya huyu wasira, yeye alipobaini akavunja kambi strategically. ...JK wa 2005 siyo huyu anayeondoka....sasa yeye yuko tayari kwa swala ya hijja kwani nafsi yake imejiridhisha na ndio maana ukimuangalia usoni majibu unayaona wazi kuwa amechoshwa na wachumia tumbo waliomzunguka ktk tenure yake kwa kumpamba kinafiki ila rohoni anajua wazi "Ole wao wanafiki siku akiondoka Ikulu" JK ana mapatano kwa matendo pale pote alipogombanishwa na kufitinishwa, ole wenu msiomsoma Jakaya kwa hekima pevu usoni....

Baada ya JK kujua hekima yako akukupa nn sasa
 
huo waraka akiandika Warioba nitaona uzee umemfika kiwango cha juu sasa na ni utoto.

Huo waraka una Ubaya gani? Acha dharau, mie nimeona kamuasa wassira aseme ukweli. Kumwambia hivyo ndo uzee umemfikia mwisho? Wassira ndo anajitoa akili kama ambavyo sura yake ilivyo na akili ndo anakoipeleka. Kama na wewe unamsapoti Wassira basi una maslahi binafsi. Wassira alikosea kujinadi hadharani kupitia jina la mtu
 
Huo waraka una Ubaya gani? Acha dharau, mie nimeona kamuasa wassira aseme ukweli. Kumwambia hivyo ndo uzee umemfikia mwisho? Wassira ndo anajitoa akili kama ambavyo sura yake ilivyo na akili ndo anakoipeleka. Kama na wewe unamsapoti Wassira basi una maslahi binafsi. Wassira alikosea kujinadi hadharani kupitia jina la mtu

Aliekuumba ww ndo kamuumba yeye
 
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba ameandika waraka kumjibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira kwa kauli yake kuwa ndiye aliyemkimbiza CCM kwenda upinzani mwaka 1995.

Katika waraka wa maandishi alioutuma kwa gazeti hili, Jaji Warioba alisema maelezo ya Wasira dhidi yake katika mahojiano maalumu na gazeti hili hayakuwa sahihi na hivyo akamtaka ajifunze kusema ukweli kwa kuwa mambo anayosema yanaweza kumrudia baadaye.

Waraka wenyewe

Tarehe 22 Septemba 2014, Gazeti la Mwananchi lilitoa taarifa ya mahojiano kati yake na Mheshimiwa Steven Wasira. Katika mahojiano hayo, Mheshimiwa Wasira alisema mimi ndiye niliyemkimbiza CCM.

Tangu mchakato wa Katiba Mpya kuanza nilikuwa napata taarifa kwamba Mheshimiwa Wasira alikuwa amenifanya mtaji wake katika kutetea msimamo wake. Wakati mmoja kuna kiongozi mwenzake aliniuliza kama nina ugomvi binafsi na Mheshimiwa Wasira kwa sababu kila akipata nafasi kwenye vikao vyao ananishambulia. Wakati wa mabaraza ya Katiba nilipata taarifa za aina hiyo. Nilichofanya ni kuwaarifu viongozi wake wa CCM.

Mengi aliyosema Mheshimiwa Wasira siyo ya kweli. Napenda nitoe ufafanuzi kwa machache yafuatayo:-

Niligombea mara mbili na Mheshimiwa Wasira. Baada ya Uchaguzi wa 1990 ambao nilishinda kwa kura nyingi sana, uchaguzi huo ilitenguliwa kwa sababu nilifanya kampeni kwa kutumia gari la Waziri Mkuu.

Uchaguzi ulirudiwa mwaka 1992. Niliunda timu ya kampeni, Mheshimiwa Wasira akiwa kiongozi. Aliniomba atangulie jimboni kuandaa mazingira. Alipofika huko akaanza kampeni dhidi yangu na kutangaza kwamba anagombea. Wakati huo kura za maoni zilikuwa zinapigwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya. Wajumbe walikuwa kama 600. Nilipata kura 400 na Mheshimiwa Wasira alipata kura chache akiwa mtu wa tatu au nne. Baada ya matokeo akatangaza anajitoa kwenye mchakato na jina lake lisipelekwe NEC. Alikataliwa kwa sababu kufuatana na kanuni, muda wa mtu kujitoa ulikuwa umepita.

Mwaka 1995, kura za maoni zilikuwa zinapigwa kwenye kata. Tulianza na Kata ya Sarama ambayo iko upande wa mashariki, siku ya tatu tulifika Nyamuswa ambacho ndicho kijiji ninachotoka. Nyamuswa ilikuwa kituo cha tano kati ya vituo 12.

Baada ya hapo tulielekea magharibi ya jimbo anakotoka Mheshimiwa Wasira. Baada ya kura kupigwa katika Kata ya Guta, Mheshimiwa Wasira alijitoa kwa sababu aliona hawezi kunishinda hata kama angepata kura zote za kata mbili zilizobaki. Siyo kweli kwamba Nyamuswa ilikuwa ya mwisho kupiga kura na siyo kweli wananchi wa kata nzima walipiga kura. Kumbukumbu zote zinaweza kupatikana wilayani na makao makuu ya CCM.

Mheshimiwa Wasira anasema kwamba nilikuwa Jaji na kesi iliyopelekwa mahakamani ni kama kesi ya tumbili kupelekwa kwa nyani, kwa maana kwamba majaji walinipendelea. Kumbukumbu za kesi hiyo zipo. Wakati huo sikuwa jaji. Isitoshe huko nyuma uchaguzi nilioshinda 1992 ulitenguliwa. Kwa nini wakati huo sikupendelewa? Kumbukumbu za kesi zinaeleza kwa nini Mheshimiwa Wasira alifungiwa kugombea kwa kipindi.

Mheshimiwa Wasira ni kiongozi wa Taifa kwa kipindi kirefu. Ni mbunge wangu na namtambua hivyo. Tunaweza kuwa na mtazamo tofauti katika baadhi ya mambo lakini hiyo si sababu ya kusema mambo yasiyo ya kweli kwa nia ya kujijenga kisiasa.

Yeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM. Yeye ni Waziri mwandamizi. Yeye anafikiria kugombea urais. Ni vizuri basi akajifunza kusema kweli (ambayo ni ahadi mojawapo ya WanaCCM). Akumbuke anayosema yanaweza kumrudia mbele ya safari.

Waraka wa Warioba kwa Wasira - Kitaifa - mwananchi.co.tz




 
mtasema mengi sana ss tunawaangalia tu kwa kweli ccm sijaona kiongozi wa maana lowasa ndo mchafu hafai kabisa!!! yani labda wassira coz huyu mzee mimi namfahamu vizuri hana kashfa yoyote lakin sema tu huyu warioba anazeeka vibya kwa kumchafua mzee wa watu.. kwakweli chadema wasipimsimamisha mgombea wa maana mm kura yangu ipo kwa mzee wasira
 
wasira+akifuatilia.jpg
warioba+aonya.jpg
 
Waraka wa Warioba ni mzuri.
Bila shaka Mr Tyson anatafuta pa kutokea. Warioba ni mwanachama wa CCM si CCM! Kama kungekuwa na tatizo kipindi hicho, basi angepeleka malalamiko CCM na si kukimbia chama. Ni aibu kwa mtu anayehamahama kwenye vyama akagombea nafasi ya urais kama vile hamna waadilifu na wakereketwa ndani ya chama.
Bila shaka anaposisitiza kuwa UKAWA warudi kwenye vikao vya BMK angetakiwa kujua kuwa hiyo principle ilikuwepo ndani ya CCM tangu enzi hizo za Warioba. Na alichotakiwa kukifanya ni kujisalimisha kwenye chama na si kwenda NCCR.
Anjo

Wassira ni mpambanaji kwa hali zote halali na kinyume chake.Ni kweli amemsumbua sana Warioba jimbo la Bunda lakini aelewe kwa uraisi wa nchi hapana. Kitendo chake kukimbilia upinzani kipindi kile badala ya kupambana ndani ya chama chake na hata kama baadae alirudi kimempunguzia imani kwa wananchi kumpa madaraka makubwa.
 
huo waraka akiandika Warioba nitaona uzee umemfika kiwango cha juu sasa na ni utoto.

Kuweka kumbukumbu sawa ni utoto kwa hiyo, ni sifa ya utuuzima kuacha uongo uenezwe pasipo kuukanusha! Maajabu haya!
 
Anayekutumia amekuharibu ubongo wako, sasa unawaza kama yeye, pole.
Kamwambie Wassira hana kashfa hata moja, hayo yote mnajitahidi kutunga kumchafua Rais wa Watanzania mtarajiwa.

hahahahaaaaa eti rais mtarajiwa kaka mwambie kama Alivyoenda kwenye gazeti la dira, aende tena akasimulie kuhusu hii bilioni 1 alafu ni kwambie huwa si tumiwi mi najitmbua kuliko unavyoelewa kuna mambo ya wasira yatakuja humu hamtaamini endeleeni na tenda zenu kumbuka mi ni fundi na hamkutulipa inavyopaswa kuanzia SONGEA MPAKA SHINYANGA, MUNGU AMESAIDIA SASA NIKO GGM MTAUMBUKA mwambie MASATU kuwa atajutia mapunjo waliyoyafanya kwenye miradi yote, nabado PEMBEJEO
 
Hivi mnajua Jaji Warioba anaandamwa na ile organ ya Dkt Magufuli eti aondoke kwenye nyumba yao alikoweka ofisi zake Masaki! Hivi JK au JPM wanalijua hili jambo? Acheni kumchafua JK na Magufuli kwa usanii huu, kawakosea nini huyu Jaji?

Anatakiwa kulipa kodi kama mpangaji mwingine yule kama kupewa ofisi na serikali haimo kwenye marupurupu ua waziri mkuu mstaafu!!! katika ofisi zile si kuna kampuni yao ya uwakili kwanini wasipe kodi ya pango?
 
Warioba atabaki kuwa MWAMBA wa Taifa hili! Kwa kusema ukweli pasi na unafiki, amekuwa mtume mwema na mwaminifu. Wezi, wahafadhina, walafi, viwavi, wavivu na wapuuzi watamuona J S Warioba kama shubiri na mwiba juu ya ulafi wao! Asante Warioba. Taifa bado linakuhitaji iwe ndani ama nje ya ccm.

Labda Mwamba Wa familia yenu
 
Back
Top Bottom