Waraka no 4 wa CCM: Chakula cha njaa kilitupa ushindi Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waraka no 4 wa CCM: Chakula cha njaa kilitupa ushindi Igunga

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mikael P Aweda, Dec 6, 2011.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Gazeti la Mtanzania leo limeripoti kuwa ccm imekiri kuwa Chakula cha njaa iliwasaidia kushinda Igunga. Gazeti hilo limenukuu waraka no 4 wa idara ya oganizesheni uliowasilishwa ktk mkutano wa NEC ulioisha hivi karibuni Dodoma.

  Waraka wenyewe unasema, kama ulivyonukuliwa na gazeti
  Ktk Muda huo wa kampeni, Serikali ilipeleka mahindi ya msaada tani 1000 kiasi ambacho ni kidogo sana kulinganisha na mahitaji. Jambo hili kwa upande moja liliweza kupunguza kura za ccm kwenye maeneo ambako chakula hakikufika.

  Waraka pia unasema kutotekelezwa kwa ilani ya ccm na ahadi za viongozi kwa upande mwingine pia ilichangia kushuka kwa kura za ccm, mfano kutojengwa daraja la Mto Mbutu.

  My take,
  Kwa kuwa kura zilipungua mahali ambako chakula hakikufika, kwa hiyo ccm iongeza chakula penye njaa ili kura iongezeke? Ndiyo mbinu bora ya ushindi?
  Kwa kuwa hiki ni Chama dola, nini hatma ya nchi yetu?
  Je, hii itakuwa ni kuhalalisha hoja kwamba CCM ilishinda kifisadi?
  Kama jitihada zote hizi tofauti ya kura kati ya ccm na Chadema ni 3000 na kidogo nadhani 2015 hapatatosha.
   
 2. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Nawapa pole sana wanaigunga CCM inawadhririsha,Watu wa Igunga badilikeni jamani ona CCM inavyowadharau,eti mkipewa chakula tu mnawapa kura BADILIKA IGUNGA.
   
 3. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Hivi nyie viongozi wetu CHADEMA mmelogwa na nani?
  Tunataka nyie mtoe hoja kuhusu mipango ya CDM siyo kuleta hoja kuhusu CCM.kuna mambo mengi ambayo nyie inabidi mjitahidi ku-adress badala ya mambo ya wapinzani wenu kila wakati.

  Nachukia hii tabia. Unaweza kukutana mkutano wa chadema ukiwa na agenda 4 lakini mpangilo ukawa hivi
  Agenda no 1 kufungua.
  Agenda no 2 .Waraka wa CCM Igunga
  Agenda No 3.Maamuzi ya NEC ya CCM Dodoma
  Agenda No 4.Chadema kuonana na Kikwete Ikulu
  Agenda No 5 Kufunga

  Ipo siku mtajua nina maana ipi:lol:
   
 4. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wewe unatusema sisi Chadema,
  Soma gazeti la Mtanzania la Leo au Tafuta waraka wenyewe wametaja Chadema mara kumi kidogo pamoja na kuwa wao ni Chama dola. Sembuse sisi wapinzani?

  Ushauri wako ni mzuri mkuu, lakini ccm kama Chama dola mmoja ya mapendekezo yake ktk waraka huo huo wanapojadili jinsi ya kujadili mfumo wa chaguzi za marudio ambao unatuhusu, kwa hiyo hatuwezi kuacha kujadili hilo.
   
 5. N

  Nyota Njema Senior Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona hizi ni ngumi za juu juu, hakuna kushikana shikana; hata hivyo naomba mrudi kwenye hoja. Hoja ya kuwa CHADEMA wanajadili hoja za CCM haina mashiko kulingana na hoja halisi iliyopo hapa jamvini. Hoja hapa ni huo waraka wa CCM, maana chama hicho kina dhamana kwa Watanzania, lazima watueleze wanaongoza vipi nchi hii, kama kweli ni kwa njia ya kugawa vipipi badala ya kuleta maendeleo basi tujue ili tufanye maamuzi sahihi 2015!
   
 6. D

  Dopas JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wajitahidi kuweka akiba ya chakula gn 1000 kila jimbo la uchaguzi 2015 ili walau wapate ushindi mwembamba. Kinyume chake hawana lao Igunga 2015 na kwingine kwenye uelewa wa hitaji la mageuzi.
   
 7. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 841
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Masikitiko!
   
 8. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Sasa hasira yako nini. Kumshinda adui inabidi ufahamu pia mbinu zake. Hata hivyo hapa Aweda amesema kama mwana JF wa kawaida na sio kama kiongozi wa Chadema.
   
 9. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Usiwe kichaa wewe,hiyo taarifa imetolewa na Chadema?Gazeti la Mtanzania linamilikiwa na nani.?
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Bado ule ubwabwa harage njaa mbaya.
   
 11. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hiyo dhahiri ni Rushwa na iliishalalamikiwa,kwamba kwanini chakula kipelekwe wakati wa kampeni na njaa ilianza kabla.TAKUKURU walilifumbia macho kwa sababu wao wanaongozwa na CCM ,na ndio maana rushwa ilitawala waziwazi mpaka kuibua ule mgogoro wa mabalozi waliopunjwa rushwa.JIbu la matatizo yote haya ni CCM kung'oka madarakani kwa hali yoyote ile ndio mifumi hii ya kidhalimu itakapokufa.Vinginevyo yataendelea kuja mapya mengine na hatutakua na la kufanya,tutabaki na makelele yetu humu.
   
 12. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mwaka 2015 Watapeleka chakula kilichopikwa kabisa ili kuwaondolea wapiga kura gharama za mkaa, maji(Maana ni tabu kupatikana).

  Kweli Magamba ni Wabunifu!
   
 13. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
   
 14. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Hilo gazeti linaongoza kwa uzushi! Mchadema anayebisha abishe nimpe evidensi
   
 15. s

  shukia Member

  #15
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa tatizo ni kubwa kuliko wengi tunavyofikiria. Kwanza kumpa mtu chakula ili akupe kura. Kwa maana hiyo unatumia dhiki aliyo nayo ili kujinufaisha. Kama chama ambacho kipo madarakani kwa muda mrefu, kwa nini wananchi wake wategemee chakula cha msaada. Kama jitihada za makusudi zikifanyika, Tanzania si nchi ya kutegemea chakula cha msaada. Kwa maana hiyo ugawaji wa chakula unadhihirisha ubovu wa serikali.

  Pili, kwa wanaopokea chakula na kutoa kura. Kwanza poleni kwa njaa. Lakini jiulizeni zaidi, mtapokea chakula mpaka lini? Bila uchaguzi mdogo kuwepo hali yenu ingekuwaje? Serikali yenu inawawekea mipango gani ya kujitosheleza kwa chakula pasipo kutegemea msaada, tena kipindi cha kampeni? Kutegemea misaada ni kujiweka katika hatari ya kuwa mtumwa kimawazo. Kunahitajika mabadiliko ya kifikra.
   
 16. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Ndugu kaa ukijua kuwa CCM sio Chama cha siasa peke yake, ndio CHAMA KINACHOSHIRIA DOLA. Hatuwezi kuacha kujidali kwani matendo yake yana far reaching consequences sio katika politics pekee bali nchi nzima.

  Vitendo vya serikali kupeleka vyakula vya misaada wakati wa uchaguzi ni ubakaji wa demokrasia, wanafanya haya kwa maelekezo ya CCM na kumbuka hizi ni rasilimali za taifa, kesho watachukua mishahara ya walimu wakanunue Tshirt ndo utapoona umuhimu wa kuyajadili haya regardless uko chama gani.
   
 17. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hizo ni mbinu za mwisho kabisa karibu wanaachia saizi hali yao ni mbaya mno CCM!
   
 18. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kakwambia nani kuwa mleta hoja ni kiongozi tena wa cdm? Mbona umepata mchecheto kuna nini hapo? Hivi hujui wamiliki wa Mtanzania ni kati ya waliopiga debe Igunga, mbona hukuwaambia walete mambo ya msingi (kama hili sio la msingi) waachane na ccm?

  Sasa kwa taarifa yako habari hii ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu hasa kuelekea 2015, na ili uamini kuwa ni kati ya habari muhimu hata ccm wameijadili kwenye vikao vyao vya chama na ndio chanzo cha kutufikia sisi, acha woga siasa siku zote ni kosa la mwenzako faida kwako na agenda kwa wananchi kama ccm inavyoshupalia swala la udini kwa cdm japo halina mashiko
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Na hili la ugawaji wa ubwabwa maharage wamelijadili kwenye waraka namba ngapi??

  [​IMG]
   
 20. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Punguza povu umeambiwa gazeti la Mtanzania ndilo limetoa hiyo habari wewe unakurupuka na ajenda za mikutano ya Chadema. Au kwa vile aliyeleta ni kiongozi wa Chadema tofautisha source na mwanzisha thread.
   
Loading...