Uchaguzi 2020 Uchaguzi mdogo Buhigwe; Felix Kavejuru wa Chama cha Mapinduzi (CCM) atangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA BUHIGWE
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buhigwe Felix Kavejuru amepata ushindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo baada ya kupata kura nyingi zaidi ya wagombea wengine.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Buhigwe Bi. Marycelina Mbehoma amemtangaza Bw. Kavejuru kuwa mshindi baada ya kupata kura 25,274 ksti ya kura 30320 halali zilizopigwa. .

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Bi. Marycelina Mbehoma alisema Bw. Kavejuru aliwashinda wagombea wenzake kutoka vyama 12 vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi huo.

Baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe, Bi. Marycelina Mbehoma alimkabidhi cheti cha ushindi Bw. Kavejuru kama inavyoelekezwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Buhigwe ulifanyika Mei 16 mwaka 2021 pamoja na Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kifoma na Uchaguzi wa Madiwani katika Kata Tano za Tanzania Bara.

Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Buhigwe ulifanyika baada ya mbunge wa jimbo hilo (Dkt. Philip Mpango kupoteza sifa za kuwa mbunge baada ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


IMG-20210517-WA0004.jpg

MATOKEO YA UDIWANI
1. Katika Kata ya MIUTA Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara
Mgombea wa CCM Ndg. Mahamoud Chiwembi amepata kura 670 dhidi ya Mgombea wa ACT - Wazalendo Ndg. Saidi aliyepata kura 507 na kutangazwa kuwa Diwani mpya wa Kata ya MIUTA.

2. Katika Kata ya Igunga Wilayani Igunga, Mkoani Tabora
Mgombea wa CCM Ndg. Athuman Hussein Mdoe amepata kura 14,379 dhidi ya Mgombea wa ACT - Wazalendo Ndg. Kelvin Mikora aliyepata kura 759 na kutangazwa kuwa Diwani mpya wa Kata ya IGUNGA.


PIA SOMA
- Uchaguzi 2020 - Makamu wa Rais Dkt. Mpango ashiriki zoezi la upigaji kura Buhigwe

 
Hongera sana kwake mshindi wa uchaguzi Kavejuru - itumie vizuri fursa hiyo ili wananchi wako watuwe ndoo
 
Back
Top Bottom