Waraka mwingine wa Mwigamba kwa Rais JK

Waraka mwingine wa Mwigamba kwa Rais JK

kwa mwenye akili atajua kuwa kikwete kafanya mengi mazuri yanayoonekana lakini kwa mwenye chuki moyoni ataona mapungufu pekee.machache mazuri ni haya;
1.shule za sekondari kila kata.
2.ongezeko la vyuo vikuu nchini sambamba na ongezeko la graduates kila mwaka.
3.uhuru wa kutoa maoni mf.kutukana hapa JF kama sisi tunavotukana pamoja na mwigamba.
4.kuendeleza kujenga barabara za lami kuunganisha makao makuu ya mikoa hata wilaya kote nchini.
5.kutoa kipaumbele katika uongozi kwa vijana na wanawake katika maeneo nyeti serikalini.

AU MNATAKA AWALETEE CHAKULA MAJUMBANI KWENU NDIO MTARIDHIKA?hiyo haiwezekani,tufanye kazi tuache kulalamika.
 
tangu lini chadema na gazeti lake la tanzania daima wakaandika mema ya kikwete na serikali yake?
 
Tatitizo la uongozi na siasa chafu kwa Tanzania yetu ni mfumo mbaya wa uchaguzi, na ndo mana Taifa hili kila mtu ana kitambulisho chake, Kama serikali ya ccm iyopo madarakani ni wakweli waharakishe upatikanaji wa national ID kwa kila raia na daftari la kupiga kura liwe electronically accessed, naamini haya yatamaliza kama si kupunguza uchakachuaji.
 
mh hiyo 2015 sijui CCM watatokea wapi! Na wakirudia kale kamchezo chao cha kuchakachua wacha tu Tz igeuke kama Misri na Tunisia kipindi kile eboo.
 
Maego hujatulia man wangu." Hivi unajua hata mbinguni huwa wanamshangaa jk " inabidi aingizwe kenye rekodi ya dunia kwa ...... wake.
 
huyu nae wa wapi!!!??? hebu tukumbushe mema ya kikwete na serikali yake ya chukua chako mapema na kauli mbiu yao ya tumbo mbele maendelo nyuma.
 
wakuu, comments mlizotoa humu jf,hakika ni sahihi mimi sina neno tena! Kwa kawaida mtu atakaye pona ugonjwa alio nao ni yule anaye sikia ushauri wa doct, na kisha kuufanyia kazi mara moja ya kutumia dawa alizopewa.tatizo ni kwamba Jk, ana kiburi sana na dharau,na hiyo itamgharimu, na mwaka huu ni mwaka wa shida na njaa kali
 
tangu lini chadema na gazeti lake la tanzania daima wakaandika mema ya kikwete na serikali yake?[huyu nae wa wapi!!!??? hebu tukumbushe mema ya kikwete na serikali yake ya chukua chako mapema na kauli mbiu yao ya tumbo mbele maendelo nyuma. ]
 
Bw. Mwigamba ujumbe mzuri! Ila nakuhakikishia JK ameweka pamba kwenye masikio na kulala usingizi wa pono pale magogoni!! Kelele zetu waaaaala hamzimzuii kulala usingizi wake!!

Sana sana utaambiwa unamuonea gere na kuleta makala zako za uchonganishi.
 
Tuliona Mbwebwe nyingi miaka 50 ya Uhuru kwa kutuonesha silaha nzito Za kivita na Wakati wa Mafuriko kumbe hata Boat hawana
Mkuu wa mkoa alisema kuwa helicopters zetu zilizokuwa zinazunguka angani wakati wa mafuriko hazikutengenezwa kwa ajili ya uokoaji, hapa alikuwa anamaanisha nchi haina vifaa vya uokoaji. Vivyo hivyo hata vile vifaa vya kivita ni kwa ajili ya mapambo ya sherehe mbali mbali za kitaifa!!!!
 
Mwigamba, wewe kweli ni mwamme wa Shoka. Tungekuwa na wanaume kama wewe 10 tu Tanzania ingefika mbali. Ubovu mashoga kibao hata sisi wanawake tuna ma.kende zaidi yao. Kazi kujikomba kwa huyo bab Riz1. Mwigamba, mungu akupe uhai na maisha marefu, Tanznaia inakuhitaji sana
Dada umeanza vizuuuuuri dah mwisho umeishia kutukana wanaume.Jamaa gani huyo aliyeshindwa kukudhibiti na kukufanya ushindwe kuheshmu wanaume wote??Vijana jitumeni, hii sasa dharau.
 
kwa mwenye akili atajua kuwa kikwete kafanya mengi mazuri yanayoonekana lakini kwa mwenye chuki moyoni ataona mapungufu pekee.machache mazuri ni haya;
1.shule za sekondari kila kata.
2.ongezeko la vyuo vikuu nchini sambamba na ongezeko la graduates kila mwaka.
3.uhuru wa kutoa maoni mf.kutukana hapa JF kama sisi tunavotukana pamoja na mwigamba.
4.kuendeleza kujenga barabara za lami kuunganisha makao makuu ya mikoa hata wilaya kote nchini.
5.kutoa kipaumbele katika uongozi kwa vijana na wanawake katika maeneo nyeti serikalini.

AU MNATAKA AWALETEE CHAKULA MAJUMBANI KWENU NDIO MTARIDHIKA?hiyo haiwezekani,tufanye kazi tuache kulalamika.

Shule za kata ubora ukoje?
Chuo cha dodoma hata mwigamba kakitaja.
Uhuru wa kuongea mara nyingine ni ishara kwamba hakuna kiongozi hivyo yeyote anaongea.
Barabara gani mpya anazojenga mbali na alizoanzisha mtangulizi wake?
Vijana na wanawake wameleta nini tofauti na wazee? Ngeleja, Masha, Nyarandu, Nchimbi, Makinda etc

Ahadi ni deni....aliahidi mwenyewe atimize.... Hata katiba haikuwa kwenye ajenda zake lakini madam alidandia treni hana budi kutimiza kikamilifu.

Ushauri alopewa ni mwanana......
 
tangu lini chadema na gazeti lake la tanzania daima wakaandika mema ya kikwete na serikali yake?
Mema si ndio haya yakuambiwa ukweli au wewe unataka adanganywe ndio uone wema???wewe unaishi wapi ambaye huyaoni haya yakitokea???tatizo maisha ya kinafki yameshakuwa part ya wanaccm, badala ya mtu kuambiwa ukweli ili ajirekebishe kama anataka, wanaccm wanataka mtu asifiwe alhali hakuna anachofanya......upuuzi huo ndio uliomfikisha JK hapo alipo.
 
kwa mwenye akili atajua kuwa kikwete kafanya mengi mazuri yanayoonekana lakini kwa mwenye chuki moyoni ataona mapungufu pekee.machache mazuri ni haya;
1.shule za sekondari kila kata.
2.ongezeko la vyuo vikuu nchini sambamba na ongezeko la graduates kila mwaka.
3.uhuru wa kutoa maoni mf.kutukana hapa JF kama sisi tunavotukana pamoja na mwigamba.
4.kuendeleza kujenga barabara za lami kuunganisha makao makuu ya mikoa hata wilaya kote nchini.
5.kutoa kipaumbele katika uongozi kwa vijana na wanawake katika maeneo nyeti serikalini.

AU MNATAKA AWALETEE CHAKULA MAJUMBANI KWENU NDIO MTARIDHIKA?hiyo haiwezekani,tufanye kazi tuache kulalamika.

Naona unaongea wimbo ule ule unaoimbwa na wa wanufaika wakubwa wa fedha za ufisadi. Kwanza ujue maendeleo ya nchi hii hayatokani na fedha za Rais, ni fedha zetu za kodi hivyo yapo mambo ambayo ni lazima atake asitake as long as anakusanya kodi zetu sharti ayafanye. Najua wewe ni mkazi wa Masaki/Oysterbay/Mbezi Beach ndo mana unaongelea shule za Kata kama success story kwa JK, tema mate chini tafadhari.

Hizo shule ndo zimezidisha ujinga humu nchi. Tembelea huko Mbekenyela, Kazuramimba, Samvulachole, Lusewa, Naminywili na Kakonko ukajionee hizo unazoziita sekondari za kata, then ndio uargue case hapa. Acha kabisa, ndugu zetu wamepoteza uelekeo wa elimu huko, mtu anamaliza form four hajui kusoma wala kuhesabu na la saba alifauru. Shule sio majengo, shule ni walimu, vifaa vya kufundishia na kutumia, mitaala mizuri na maabara. Au wewe hujapita shule?????Shule za kata ni za kuongelea mbele za watu kweli???

Hivi wakati anagombea Urais angekuja na sera kuwa mkinichagua kuwa Rais ntawapa uhuru wa kutoa maoni wewe ungempa kura yako, kututeulia wahuni, mafisadi na wastaafu na ma bimdogo zake kuwa wakuu wa wilaya wewe ungetoa kura yako???labda kama na wewe ni bi mdogo wake. Wewe usitutie hasira, hebu acha hii ngoma ichezwe na wenye nayo na wale wanaoujua wimbo.
 
[h=1]Kupanda kwa bei ya Umeme wa Tanesco, ndio mema ambayo tumendewa na Serikali hii ya CCM. Hivi kweli tunahitaji kusoma Phd ndio tujue au tuelewe kuwa Nchi hii imefikishwa mahali pabaya? Umeme leo umepanda, Mafuta nayo ndio usiseme, Elimu ndio hio wanafunzi wanafukuzwa wakati wakidai haki zao za msingi. Mishahara ndio hio tulioambiwa hata Mkiidai haitaongezwa Ng'ooo!! Hivi kweli viongozi wanaotuongoza wameweka pamba masikioni? au wana kauli mbiu ya TUMBO mbele Uzalendo nyuma? .Hivi kama Wenye Viwanda wakipandishiwa bei ya Umeme,Mzigo anaubeba mwenye kiwanda au Mlaji wa Ile Bidhaa inayotoka kwenye kile kiwanda? Halafu tunasema tumendewa mema, yapi hayoo? Mtu anayesema ametendewa mema kuna kitu anafaidika nacho toka kwa hao tunaoona hawawa tendei mema wananchi wa Tanzania.[/h]
 
Kupanda kwa bei ya Umeme wa Tanesco, ndio mema ambayo tumendewa na Serikali hii ya CCM. Hivi kweli tunahitaji kusoma Phd ndio tujue au tuelewe kuwa Nchi hii imefikishwa mahali pabaya? Umeme leo umepanda, Mafuta nayo ndio usiseme, Elimu ndio hio wanafunzi wanafukuzwa wakati wakidai haki zao za msingi. Mishahara ndio hio tulioambiwa hata Mkiidai haitaongezwa Ng'ooo!! Hivi kweli viongozi wanaotuongoza wameweka pamba masikioni? au wana kauli mbiu ya TUMBO mbele Uzalendo nyuma? .Hivi kama Wenye Viwanda wakipandishiwa bei ya Umeme,Mzigo anaubeba mwenye kiwanda au Mlaji wa Ile Bidhaa inayotoka kwenye kile kiwanda? Halafu tunasema tumendewa mema, yapi hayoo? Mtu anayesema ametendewa mema kuna kitu anafaidika nacho toka kwa hao tunaoona hawawa tendei mema wananchi wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom