Waraka mwingine wa Mwigamba kwa Rais JK

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
Na Samson Mwigamba

MHESHIMIWA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwanza nakupa hongera kwa kutimiza miaka sita ndani ya Ikulu ya Magogoni.

Lakini napenda kuwa muwazi kwamba nakupa hiyo hongera kwa desturi ya kitanzania tu lakini kiuhalisia hakuna bado una safari ndefu ya kuleta maisha bora kwa Mtanzania kwani kwa sasa hali ni mabaya sana.

Mheshimiwa rais naomba nikukumbushe kwamba ahadi kubwa mbili ulizoingia nazo kwenye madaraka mwaka 2005 yaani maisha bora kwa kila mtanzania na uongozi wa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya, zote zimeyeyuka.

Miaka sita ya wewe kuwa madarakani imeshuhudia maisha duni kwa kila mtanzania na kwa kweli

Serikali yako imekuwa legelege kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Wakati umeingia madarakani mwaka 2005 mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 5, leo tunapoongea uko kwenye asilimia 19 ambazo kimsingi mimi nasema ni asilimia za wataalam wa uchumi.

Kwangu mimi raia wa kawaida ambaye si mchumi ninauangalia mfumko wa bei katika jicho hili: Kwamba wakati unaingia madarakani mwaka 2005 tulikuwa tunanunua kilo ya mchele kwa shilingi 800 lakini leo tunaununua mchele huo huo kwa shilingi 2300.

Mfumko huu wa bei ni asilimia 150. Vivyo hivyo kama sukari ilikuwa shilingi 600 na leo tunainunua shilingi 2,500 na mahali pengine mpaka shilingi 2,700, mfumko wa bei hapo ni asilimia 230. Vivyo hivyo lita ya mafuta ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi zisizozidi 1,100.

Leo tunainunua lita hiyo hiyo kwa shilingi 2,050. Mfumko wa bei hapo ni asilimia 105. Masikini wa kupindukia wasio na uhakika wa mlo mmoja kwa siku walikuwa milioni 11 wakati Kikwete anaingia madarakani 2005, lakini leo wako takriban milioni 13. Hayo ni machache sana yaliyojiri wakati wa utawala wako wa miaka sita.

Hapo sijagusia akiba ya fedha za kigeni ilivyopukutika, sijazungumzia jinsi mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ilivyochakachuliwa, sijazungumzia jinsi uzembe ulivyopoteza maisha ya watanzania wenzetu kupitia mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto, sijazungumzia ombwe la uongozi uliosababishwa kushindwa kuchukua maamuzi, sijagusa ufisadi wa Richmond, Dowans, Stimulus package na mengineyo mengi.

Naomba nikuulize tena mheshimiwa rais, nikupongeze kwa lipi katika miaka yako sita? Mpaka sasa hatujaona barabara za juu ulizoziahidi mwaka 2005. Mheshimiwa, bado hatujaonyeshwa bayana ajira milioni moja zaidi ya kuona vijana wanaookota chupa za maji zilizotumika mitaani wakiongezeka mithili ya vichaa.

Hatujaona shule moja ya kitaifa katika kila wilaya ambayo itachukua wanafunzi kutoka pande mbalimbali za nchi yetu katika jitihada za kukuza uzalendo na umoja wa kitaifa. Katika hali hii najaribu kutafakari utakapoachia madaraka hapo 2015 ni nini utakumbukwa nacho!

Kwa maoni yangu huwezi kwa muda uliobaki kufanikiwa kununua meli tatu kubwa kuliko MV Bukoba kwenye maziwa matatu yaani Victoria, Tanganyika na Nyasa. Na sioni pia uwezekano wa wewe kuibadilisha Kigoma kuwa kama Dubai kama
ulivyoahidi mwaka jana.

Sioni pia uwezekano wa wewe kuweza kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa huko Mwanza na Bukoba katika muda uliobaki. Sioni uwezekano wa kuhakikisha kila mwanafunzi ana kompyuta yake kabla ya 2015 kama ulivyoahidi, sijaona
uwezekano wa kumnunulia bajaj kila mwanamke mjamzito wa nchi hii, na kadhalika. Naona anguko unalokiachia chama chako kama nilivyotabiri mwaka 2007, miaka miwili tu toka ulipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza.

Katika utabiri wangu nilisema, mwishoni mwa uongozi wake wa awamu ya nne wananchi watashtuka wataikataa CCM yote kwa kuwa waliaminishwa kwamba hakuna aliyebaki ndani ya CCM anayeweza kuikoa nchi hii zaidi ya Kikwete. Lakini wale tunaokupenda (ambao wewe unadhani ndio tunaokuchukia), hatukuachi hivi hivi.

Tunakupa ushauri ili ukichemsha ujilaumu mwenyewe.

Sasa nakupa ushauri wa mwisho.

Ushauri wangu kwako ni kwamba jiegemeze kwenye katiba mpya. Yule unayemwita Mzee Mkapa, alipoona anaondoka bila cha
maana cha kukumbukwa nacho, aliamua kujenga Uwanja mpya wa Taifa wa kisasa. Wewe tengeneza Katiba mpya. Ninaposema hivyo simaanishi kwamba hauko katika mchakato wa kuandaa katiba mpya.

Naelewa sana hilo lakini najua kwamba hiyo unayoitengeneza kwa sasa si katiba mpya bali itakuwa katiba ya zamani za kale katika jina jipya.

Ukitaka kuwa na katiba mpya fanya hivi. Katika bunge lijalo peleka bungeni muswaada wa marekebisho ya sheria ya mchakato wa katiba mpya.

Katika marekebisho hayo, jiondolee kabisa mamlaka ya kufanya uteuzi wa tume wewe mwenyewe, sekretarieti ya tume wewe
mwenyewe, bunge la katiba wewe mwenyewe, hadidu za rejea unawapa tume wewe mwenyewe, ripoti ya tume unaipokea wewe mwenyewe na mchakato wa katiba unafuata utaratibu wa kawaida wa kupeleka miswaada ya sheria bungeni kwa maana kwamba itapitia baraza la mawaziri na kadhalika. Hapa unataka kuleta vurugu isiyo na maana na pengine kuhatarisha amani.

Watu wataandamana kupinga mchakato huo na wewe kwa jeuri ya utawala utaagiza askari wako wakawapige. Badala ya kukumbukwa kama Mkapa anavyokumbukwa leo na kila mtanzania anayeingia ndani ya ule uwanja wa taifa wa kisasa, utajikuta unazungumzwa vibaya ndani na nje ya Tanzania. Kubali wananchi watengeneze katiba yao wenyewe.

Mimi si mtaalamu wa sheria lakini natambua kwamba kuna mapendekezo mazuri tu ya Jukwaa la Katiba na vyama vya siasa kama CHADEMA, CUF na NCCR ambao wanajiandaa kukuona.

Achana na jamaa zako kina Wassira, kina Nchimbi, na wenzao wa kwenye chama chako cha mapinduzi. Hao wanakudanganya na wanakutumia kwa maslahi yao ya binafsi. Hao ni kama wale waliokuwa karibu na rais wa zamani wa Ivory Coast, Laura Gbagbo.

Huyu bwana alikuwa anadanganywa na watu wa karibu naye akawa anakomaa na kung'ang'ania Ikulu matokeo yake leo yuko ICC peke yake na hakuna msaidizi wake hata mmoja aliyejitolea kushitakiwa naye. Hivi sasa una wasaidizi na washauri wengi sana walio karibu nawe kiasi kwamba sisi tulio huku nje unatuona hatuna maana bali ni wachochezi tusioitakia mema serikali "halali iliyoko madarakani".

Lakini wakati unakuja ambapo utatukumbuka wale uliotudharau kama utaendelea kutudharau na ushauri wetu. Hatuna la kufanya zaidi ya kukutakia kila la heri katika maandalizi yako ya kuja kuwa rais mstaafu atakayekuwa anazungumzwa vibaya. Utajikuta hakuna cha maana unachokumbukwa nacho na Watanzania katika utawala wako. Hukujenga uchumi, hukudhibiti ufisadi, hukufanya maamuzi ya mazito kama anavyoagiza, Edward Lowassa.

Kete pekee ambayo ulitak kujiibulia ujiko ni katiba mpya, lakini kama utakoroga mchakato wake na mchakato wa katiba mpya ukazusha vurugu, utakuwa umeharibu kila kitu. Hakuna atakayekumbuka hata vitu vizuri vichache ulivyovifanya kama kumleta kocha wa timu ya taifa ya mpira, ama kuongeza majengo pale kwenye jingo la Chimwaga na kutengeneza chuo kikuu cha Dodoma. Jaribu kutafakari lakini Waswahili walisema kama unaona elimu ni ghali jaribu ujinga.

Na wewe kama unaona ushauri wetu wachochezi ni mbaya sana, jaribu ushawishi wa wanaojikomba kwako halafu utaona matokeo yake. Kila la heri unaposherehekea miaka sita Ikulu.

Source:TANZANIA DAIMA
 
Kikwete ameoza sana,najua hii miaka mi4 iliyobaki tutashuhudia maumivu makubwa sana,lakini wa tz tulivyo wajinga tutamwacha tu huyu jamaa aende zake wakati tunamaumivu makali sana. Mungu tuhurumie sana ingawaje wengine hatukumchagua, Kweli Jk umetujeruhi sana. Asante mtu alie mchambua huyu mtu uko sahihi sana
 
Ndg yangu jk hashauriki huyu ni miongon mwa akina siambiliki nayeye mwenyewe alishadhihirisha hli pale alipoanguka akasema nimeshauriwa nipumzike nikapuuzia. Je unadhan atakusikiliza? Japo ushauri wako niwakisomi, waswahili walisema sikio lakufa halisikii dawa, mwache mwisho wa uongoz wake nimwsho wa chama chake na nimwanzo waukomboz wakwel kupitia CDM
 
Huyu JK anafanana na mti aina ya Ashok maarufu Dar es Salaam kama mu ashoki. Miti hii huwezi kufanya kuni za kupikia, huwezi kutengeneza mbao za fenicha, huwezi kutumia kama miti ya kujengea nyumba. Haiwezi hata kutumika kwa kivuli zaidi ya kuwa pambo la nyumba na kuwa makazi ya nyoka wa kijani. Hivyo ndivyo Raisi wenu muliyemchagua kwa kura nyingi alivyo, ni kama mti wa mu ashoki.
 
Huyu JK anafanana na mti aina ya Ashok maarufu Dar es Salaam kama mu ashoki. Miti hii huwezi kufanya kuni za kupikia, huwezi kutengeneza mbao za fenicha, huwezi kutumia kama miti ya kujengea nyumba. Haiwezi hata kutumika kwa kivuli zaidi ya kuwa pambo la nyumba na kuwa makazi ya nyoka wa kijani. Hivyo ndivyo Raisi wenu muliyemchagua kwa kura nyingi alivyo, ni kama mti wa mu ashoki.

ha ha ha ha kw kw kw kw
 
Kikwete ameoza sana,najua hii miaka mi4 iliyobaki tutashuhudia maumivu makubwa sana,lakini wa tz tulivyo wajinga tutamwacha tu huyu jamaa aende zake wakati tunamaumivu makali sana. Mungu tuhurumie sana ingawaje wengine hatukumchagua, Kweli Jk umetujeruhi sana. Asante mtu alie mchambua huyu mtu uko sahihi sana

"ameoza"
 
Huyu Mwigamba si ni Mccm mkubwa tu huko Tabora? kamchambua boss wake? kumbe wanakuwa wanamshabikia tu ili wale lakini hawapendi madudu yake? kweli watamkimbia kama gbabo alivyokimbiwa siku mambo yakiwa mabaya
 
labda haujafanyika utafiti tu,lakini nadhani ndiye Rais aliyeongoza kwa kutopendwa na wananchi wake tangu Uhuru!
 
Huyu Mwigamba si ni Mccm mkubwa tu huko Tabora? kamchambua boss wake? kumbe wanakuwa wanamshabikia tu ili wale lakini hawapendi madudu yake? kweli watamkimbia kama gbabo alivyokimbiwa siku mambo yakiwa mabaya

Unazungumzia mwigamba yupi?
 
Teh teh teh....'nitaigeuza Kigoma iwe kama Dubai', nadhan huwa anacheka sana kila anapoikumbuka ahadi hii!!! Mtu mzima hovyooooo.....!
 
Huyu Mwigamba si ni Mccm mkubwa tu huko Tabora? kamchambua boss wake? kumbe wanakuwa wanamshabikia tu ili wale lakini hawapendi madudu yake? kweli watamkimbia kama gbabo alivyokimbiwa siku mambo yakiwa mabaya

Issue si u-CCM wake;bali ni ubora wa hoja zake!
Nani aliyekwambia kazi ya kukosoa na kusahihisha viongozi wetu ni ya CHADEMA pekee?
Shivji ni chama gani?Warioba je?
Jambo la muhimu hapa ni kuwa Mwigamba yupo sahihi kihoja;chama chake si muhimu kwangu!
 
Kila mtu atakumbukwa kwa alichofanya. Hata ww utakumbukwa,hata mimi nitakumbukwa na yeye tutamkumbuka. Kwani wewe hukumbuki alitaka kujifananisha na VASCO DA GAMA au BATHROMEO DIAZ Wa zama hizi kwa kuizunguka dunia?

Tofauti wale walitumia melikebu yeye anatumia 'jet'. Hukumbuki kuwa yeye ndo rais anayeongoza ktk nchi zinazopakana na bahari ya hindi,nchi za SADC,EAC,Nchi zilizokuwa kimbelembele ktk ukomboz kusini mwa africa,nchi znazoongea lugha ya kiingereza,nchi zlzo kusin mwa jangwa la sahara,nchi za dunia ya tatu n.k

Kwa kuhudhuria misiba, kuwatembele waliolazwa na ndiye rais aliekwenda 'kulibusubusu' kombe la dunia mara nyingi pale diamond? Hata asipo timiza ahadi zake si tutamkumbuka kuwa ndo rais aliyewahi kutoa ahadi nyingi na za uongo kwa watu wake na katika kanda za kidunia hizo nilizo zitaja? Kila mtu atakumbukwa.

Mfano Mh.Mkapa alisema aliwahi kuwa mwanamichezo na mpenzi wa michezo lakini alikosa muda kutokana na marekebisho ya uchumi alokua akifanya.., nayeye tutamkumbuka na siku moja atasema.
 
Back
Top Bottom