Waraka kwako Abiria wangu (Binti) ninaekupaga Lifti asubuhi!!

bwn ww kuchanganganya watu!
tambua wengine wanapenda kusaidia watu, km ww hupendi mwambie atakuelewa kwani anao upeo wa kutosha kuelewa hilo
 
Kuna kitu kiko wrong hapo
Mpaka kufikia hapo uliposema kuna mengi alifanya ukamwachia nafasi na ameshaona ni haki yake na huna ujanja wa kujinasua
Mpaka kwenda kumgongea gate kisa unampa lifti na mume wake anasikia kabisa gate inagongwa na mwanamme mwingine kisa lifti na inaishia hivi hivi
Na mkeo anajua kabisa kuwa huwa unampa jirani yake wa jinsia yaka yake lifti kila siku mpaka unamsubiria getini
Na yuko na mume wake na wewe uko na mkeo na mnapigiana simu za usiku
mazoea hujenga tabia na tabia ikikomaa huleta majanga
Au mi ndo naona nyota nyota sijaelewa

nilimuheshim kama jirani mwema kusaidiana ila kavuka mipaka
 
bwn ww kuchanganganya watu!
tambua wengine wanapenda kusaidia watu, km ww hupendi mwambie atakuelewa kwani anao upeo wa kutosha kuelewa hilo

sio kwamba sipendi kumsaidia mi mwenyewe nimepanda daladala sana najua adha ya usafiri Dar ndio maana namsaidia kama jirani lakini msaada anautumia vibaya hilo ndo tatizo
 
Kwa yote hayo bado unampa lift? basi una lako jambo kwanini usibadilishe time ya kuondoka akute ushaondoka? atakupigia urudi kumfata? mnayataka wenyewe bwana, mume wa rafiki yangu hivohivo alikuwa anampa lift jirani, jirani akawataarifu na wenzie kama kuna lift huku, asubuhi moja kawakuta wamejazana watatu wanasubiri lift akawapita na kuwaambia samahani kuna watu nawapitia mbele hapo ikawa mwanzo na mwisho sasa wewe unamuendekeza huyo atabadili mpaka nguo katika gari yako



Habari zenu wana jf,

wewe dada ninaekupaga lifti kila siku naomba ujiregebishe upatapo ujumbe huu na iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama zako.



1.Sipendi tabia ya kunifanya mimi niwe nakugongea geti lako asubuhi,mimi sio dereva tax wako aisee wewe ndo mwenye shida unapashwa ujiandae mapema unisubirie nje.

2.Naomba tabia ya kunipigia sim usiku wakati nimelala na mke wangu ife elewa kwamba huna malaka yeyote yakunisumbua sumbua mimi.

3.Sipendi hayo mapafyum yako makali unayojipulizia nakereka ile mbaya kutokana na kukuheshim sana nashindwa kukuambia hata huko offisin kwako nadhani wanapata shida kutokana na hiyo pafyum yako.

4.Sipendi tabia ya kukaa kwenye gari alafu umebinua kiti unajilaza miguu unanyoosha kwenye dashbod,wewe ni nani kwenye gari yangu?

5.Sipendi tabia ya kujichania nywele na kukata kucha kwenye gari bila hata kujua hizo kucha zinarukia wapi alafu hata huangaiki kuzitafuta hivi wewe mwanamke unajua thamani ya hili gari langu?

6.Sipendi tabia ya kufungulia AC hadi mwisho asubuhi asubuhi unasikia joto unakunywaga gongo wewe,mimi huwa sipendi Ac napenda ubaridi wa mbali vioo vikiwa wazi.

7.Sipendi tabia ukiongea unanishika shati mara unipigepige mara unishike mikono naomba iwe mwanzo na mwisho tabia ya kunishikashika unanipapasa mikono sipendi.

8.Sipendi unajijua kabisa umevaa min-skert alafu unakaa unatanua miguu sina haja ya kuona hiyo chupi yako kaa kwa adabu.

9. sipendi tabia ya kuchokonoachokonoa vitu visivyokuhusu kwenye gari langu kama kubadilisha nyimbo,kuweka CD ikiscruch unagongagonga redio sipendi.

10.Sipendi tabia ya kuomba uendeshe gari wakati sikuwai kukuona hata siku moja ukiendesha unataka ujifunzie kwenye gari langu wewe kama nani ife hiyo tabia.

11.Sipendi tabia ya kunielekeza kuendesha gari wewe umekua mwalimu wangu?mimi nimejua kuendesha gari tangu nikiwa primary halafu wewe ujifanye unanielekeza unataka kunitawala kwenye gari langu?ukome hiyo tabia.

12.Sipendi tabia ya kunichekeleachekelea nikiwa na mke wangu na kunikonyeza ife mimi nina mke wangu wala sikutaki kimapenzi usione nanyamaza ukazani mi mjinga.

NAOMBA UKOME SITAKI KUKONTROLIWA KWENYE VITU VYANGU.
 
Wewe acha ujinga unapomchukua asubuhi mchane live ili kama ana swali au swala akulize
 
Back
Top Bottom