Waraka kwa Dr. Slaa


Kama huna majibu ya maswali yangu, surrender umeshindwa huna hoja. Kwanza Nani alikuwambia ukawa ni Lipumba na Slaa? Nyerere na Karume walipokufa Tanzania ilikufa?

Subiri 25 October ndipo ujue UKAWA ni mziki mnene!.

Hakuna haja ya kupaniki. aSubiri tarehe 25
 
Namheshimu sana Dr. Slaa, lakini napata shinda kuelewa kwa nini anajiapiza kusema ukweli wakati baadhi ya maneno anayoyasema si kweli. Kwa mfano, Slaa anajua wazi namna serikali zote zinavyofanya kazi. Katika hotuba yake ya jana ametaja mara kadhaa "Baraza la Mawaziri" katika maamuzi ya Richmond. Ni wazi kabisa kwamba kwa suala kubwa kama hili, Waziri Mkuu peke yake hawezi kufanya maamuzi peke yake. Kama Lowassa amehusika, basi yeye atakuwa amesimamia utekelezaji wa maamuzi ya wengi (ya Baraza la Mawaziri). Huu ndio ukweli ambao haugawanyiki!. Swali langu hapa kwa Dr. Slaa, je ni kwa nini bado anafikiri ni Lowassa pekee ndiye fisadi? Je ni nani mwenyekiti wa BLM? ana hakika ni Waziri Mkuu?. Watanzania tuwe waungwana, na tujiweke katika viatu vya Lowassa. Ni ukweli kabisa kwamba mtu huyu amewajibika sana kwa makosa ya watu wengi. Amekubali kuwajibika na kutukanwa kwa ajili ya watu wengi (Kwa niaba ya BLM zima). Huo peke yake ni uungwana tosha. Hatuwezi kuendelea kumzushia na kumbebesha mizigo peke yake kama vile yeye aligeuka kuwa mwamuzi wa mwisho katika mambo yote mazito ya nchi hii. Mimi ni Mkristo kama Dr. Slaa na sitakubali kubeba dhambi za aina hiyo. Aidha, wapo watu katika nchi hii ambao walikaa mezani na Lowassa katika BLM kupitisha maamuzi ya kuupitisha na kidhinisha mradi wa Richmond. Wasifanye dhambi kwa kukaa kimya na kumwacha mwenzao akitukanwa. Wajitokeze waseme wazi kwamba yalikuwa ni maamuzi ya wengi, na mwenzao kawabebea misalaba yao. Siwezi kumhukumu Lowassa kwa sababu hiyo kwani siku zote maamuzi yanayofanywa na BLM ni maamuzi ya wote na mtu mmoja hawezi kuyapinga. Tumeshamwadhibu (kwa kujiuzulu uwaziri mkuu wake) imetosna. Hatuwezi kuendelea kumbebesha mizigo ya maamuzi ya serikali yetu wakati huo.
 
Huyu fisadi hakutubu, what he did is to transfer allegations.


What did you want him to say if that was his fact? I would expect your chair and his crew would come out immediately to clear the atmosphere. Silence means consensus. Now everybody knows he is guilty.

Ulitaka Lowasa afanye nini? Amesemwa kikwete ndiye mwizi, naye kakubaliana na hata kaogopa kukanusha, ukijumlisha na kwa nini serikali yake haikumshitaki kama Gwajima alipomtukana Pengo au Jerry Muro alipopokeleshwa milini kumi?

Ni nani binadamu mwenye kichwa asielewe tu ukweli ambao sasa uko dhahiri?

Dr. Slaa mwenyewe alisema "Wameongea naye, ametoa vielelezo, wamemwelewa. Na wengine watakaokuja tutawahoji, tukiwaelewa tutawapokea, tutawaambia wananchi" Wewe hili bango lako unalibeba kutoka wapi?

Kama mlitaka kujua nani firaumi halisi mngepeleka kesi zao mahakamani muone mziki wa chooni usivyochezeka. Sasa kaondoka na kuamua kuungana na wazalendo, mnamskama. Mbona walitajwa kwenye orodha ya mafisadi kuanzia na kikwete hamuwasemi?

Mafisadi wa EPA, Meremeta, kagoda, Escrow, Richmond, Kiwra, barabara, gas, rea. n.k mmewafanya nini na mnao huko ccm? Kwanza shetani atawahukumu kabla hamjaungua moto wa Mungu.

Jifunze kuwa na haiba ya ukweli na aibu kama binadamu.
 

Weka ushahidi wa boda boda kuhongwa na Lowasa na utakuwa umetusaidia. Vinginevyo hizo ngonjera zisizo na mashiko hatuna haja nazo! Yeye babu Slaa alipopokelewa alipofanywa kapi na ccm na kupewa nafasi chadema anaona ilikuwa sahihi, lakini kupokelewa kwa Lowasa imekuwa nongwa! Babu kachoka, babu ameishiwa, babu anatia huruma! Babu pumzika! Magamba wamekuingiza chaka! Fedheha ni yako peke yako! Kura zote zina thamani sawa! Hakuna tofauti ya kura ya boda boda na ile ya mbunge/mzito!
Yeye Slaa mwenyewe hana uzito wowote ameondoka na kura mbili tu! ya kwake na ya mke wake!
Babu nenda utakako umeshapitwa na wakati!!!
 

La kushangaza, pamoja na kumtaja Lowasa peke yake katika Richmond na kuaha kuthubutu kumgusia kikwete ambaye Lowasa kamtaja kuwa ndiye mwenye hiyo biashara, na ambaye si yeye wala serikali yake imekanusha taarifa zile zilizotolewa rasmi tena hadharani, bado hawaongelei maufisadi mengi mengine ambayo yameendelea kuwepo kama EPA, Meremeta, Kagoda, Kiwira, gas, rada, ndge ya raisi, rea, escrow n.k n.k. Je haya yote ni ya Lowasa?

Kama ni ya Lowasa kwa nini hajawahi kupelekwa mahakamani kwa ufirauni huu ili haki kwa taifa itendeke?

Kama si ya Lowasa kwa nini wahusika wake wako ccm na wanaendelea kufumbiwa macho hata mafili ya uchunguzi hawajafunguliwa? Au wanasubiriwa siku wakitangaza kuahma ccm ndiyo waana kusakamwa kijuha?

Tatu kushndwa kuwapeleka kwenye mahakama ili haki itendeke, na kuendelea kulalamika kwa wannachi haitoshi kuonyesh serikali dhaifu isiyofaa kusimamia taifa na wananchi wake hata dakika moja zaidi?


Bila shaka Mungu atabaki upande wa wanyonge, na tutashinda.

Ccm wana fedha, ccm wana kila silaha za uovu, lakini wananchi wanyonge wana Mungu na kila silaha za nuru!.

Na ijulikane leo kwamba Mungu aliyebaba wa maskini wanyonge wa tanzania, ni Mungu Mkuu mwenye Kuogofya na kwamba yko juu sana kuliko shetani wa ccm na ulaghai wake.

Leo Mungu Anakwenda kujionyesha ili dunia ijue kamba yeye anaishi Milele na hakiyake yakaa milele na wala hahongeki wala hahadaiki!.
 
tatizo ni Mshumbusi.....ufirst lady
Umri wa dr. na huyu fake first lady ni baba na mwana. Dr. alihonga u first lady akampata halafu unarudi jioni unaanza longolongo ooh tumeona tumwachie ooh! Ndo maana alitupiwa begi lenye mihogo akale na kulala kwenye gari.
Na wewe Lissu haya mambo mazito ungeyasitiri kidogo sasa kumdhalilisha Dr, tena kupitia VOA siyo fresh.
 
Sikufurahia jinsi Dr. Alivyoruhusu jazba imuongoze katika kutoa tuhuma dhidi ya CHADEMA. Alitakiwa kutofautisha kauli rasmi za Chama na zile za mitaani (pamoja na JF). Kwa mfano, sijawahi kusikia uongozi wa CHADEMA ukisema umepania kuiondoa CCM madarakani hata kwa kumtumia shetani. Nimesoma kauli hiyo kwenye michango ya manazi hapa JF.

Aidha, kuleta habari ya viongozi wa makanisa kununuliwa (kwa kauli za mtu kama Gwajima) huku akijua jinsi suala la udini linavyotumika vibaya nchini yeye binafsi akiwa mwathirika mkuu ni ukosefu mkubwa wa busara ambao sikuutegemea kwa mtu wa aina yake.

Pia sikumtarajia azungumzie tena kwa kejeli habari za watu kusombwa na malori mkutano wa UKAWA, za babu seya na za masheikh wa uamsho. Those were too low for him - kama kutoa mipasho ya kimtaani vile.

Kwa kifupi, alionekana kama mtu aliyekuwa kwenye misheni ya "kuwapasha na kuwasuta kabisa wabaya wake" badala ya kulisaidia taifa kwa ujumbe uliokamilika kwa busara (objective) kuhusu mustakabali wa taifa katika uchaguzi huu. Na kwa kufanya hivyo ameruhusu kutumiwa vizuri sana na mashetani wa upande wa pili! Na sitaki kuamini kuwa amefanya hivyo akiwa kipofu (naïve).

Mimi niliyekuwa namheshimu sana kama mtu binafsi aliyesimama katika misingi ya uadilifu hata kama kabaki pekee, sasa naamini Dr. hana (na hakuwa na sifa) za uongozi wa kisiasa. Na hapa, unafiki mbali, hakuna chama kinachoweza kuchukuana na Dr. katika harakati za kisiasa. Atafaa zaidi kwenye ulimwengu wa akina Mtikila. Siamini kama kanunuliwa kama wengi wanavyofikiri hapa. Kweli kabisa Dr. hana bei ya pesa; lakini anaingilika kirahisi kupitia jazba aliyo nayo. Hiyo ndiyo tofauti yake na akina Mtikila.
 
Wewe hivi maneno haya uliaandika kabla au baada ya kusikiliza hotuba ya Dt Slaa? ??
Ni lazima ujitambue mzee, maana utumbo wote mnaofanya pamoja na viongozi makamanda umeanikwa hadharani kweupeee. Jenga hoja njoo majukwaani kujibu hoja. Usikae kitapeli tapeli tu na kuishi kisanii sanii. Mafisadi wakubwa nyinyi. Na bado ngoja sasa Prof Lipumba naye atakapokuja kutapika yake muone. Tafuteni watu wa kuwaongoza lakini sio watanzania hawa wa leo
 

Nani alifadhili press conference ya Slaa? View attachment 283114
 
Mwacheni mzee wa watu aseme ukweli ili awe huru. Nafsi yake inamsuta na mimi ni mfuasi wake toka nitoke. Yeye ndie alinishawishi na ndie yeye ameshauri tujitafakari wote tena. Na tumesha jitafakari tayari. Hadanganywi mtu hapa.
Tulikuwa tunapumbazwa na hatuoni utadhani vipofu., wanajofanya ufisadi ooh sijui mfumo, yaani utapeli mtupu. Na kama alivyosema Dr Slaa uongozi wa kitapeli kama huu hauwezi kuingia ikulu kamwe. Namimi nasema ni bora tusiingie kwa manufaa mapana ya mama Tanzania. Hatudanhanyikiiiii tena naomba makamanda mrudi tena baada ya miaka ishirini labda mtakuwa mmenyooka
 
hatudanganyiki tenaaaa! Njooni na gia nyingine
 
Mods wa jf mmenunuliwa kuna threads huwazitaki hasa zinawahusu ccm na maovu yao, ila za ukawa wanaziacha hata kama ni mbaya
 
 
Huyo fisadi katubu lini na nini? Hebu zinduka! Alafu ilani yenu ya Chadema na Ukawa iko wapi? Mmekubaliana nini na huyo fisadi wenu? Hujui lolote unashabikia tu!
What a hollow statement and a sad state of mind!

akili za kuambiwa changanya na zako hivi chama kinawezaje kugombea urais bila ilani . we unamsikiliza tuu magufuli na kuchukulia serious si ufanye hata kautafiti kadogo kweli ccm imewafanya mabogas ukiambiwa ilani hawana unaamini tuu. shughulisha basi akili kidogo
 
Watanzania wengi tumeshaamua kuwa tutamchagua lowassa kuwa rais na amiri jeshi mkuu wa jmt.
 

Wewe ndiyo umesahau, waandishi waliuliza hili kisha akajibu kwamba yeye hana chama, ila watz wasije wakajuta lowassa hafai, ilikuwa bra bra bra bra tuu, yaani ukiangalia kwa makini mzee kachemka maana pale ni debe wazi kwa maccm. Kapotea kwa hili hitimisho lake, kapotea sana.

Ukawa songa mbele kwa spidi ya jet. Msijisumbue kumjadili wala kumtukana Slaa, aliwahi kuwa mtu muhimu, tuheshimu hilo, na sasa amepotoka kabisa, tuachane naye.
Naomba mjadala wa jinsi gani ya kulinda ushindi, tusiwape nafasi ccm ya kuiba hata kula moja. Tuungane kuelimisha watu huko mitaani, tusiache mjadala wowote upite iwapo tuna uwezo wa kutoa elimu ukawa, ingilia mijadala hata ya wanamama, au wazee au wanababa, huu ni muda wa ukombozi, daladala zote upandazo hakikisha zinajadili siasa na siasa yenye kuelimisha kwanini tuchague ukawa yaani lowasa na timu yake na si ccm na magufuli wao. Viva ukawa viva ukwa vivaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
 
Rafiki yangu,mzee wangu dr Slaa.Nimeyatafakari sana maneno yako.Nimeyachunguza na naendelea kuyachunguza yanayoendelea Tanzania.Mimi,kama ilivyo kwa watz wengi, napenda nchi yetu iwe na maendeleo.Maendeleo kama taifa,pia maendeleo kwa watu mmoja mmoja.Sote tunaistahili keki hii tuliyopewa na Muumba.Tumepewa sisi na vizazi vyetu.Hii ndio nia ya mpiga kura.Kuchagua viongozi watakaoleta haya maendeleo,lakini pia usawa katika kugawana hii keki.Inapotokea haridhiki,mpiga kura hutafuta watu wengine wa kuwaweka madarakani ambao anaona wana nia kama yake.Hiyo ndio kitu tunaita MABADILIKO.Kuna wakati hutokea jamii kukosa maadili sana,kiasi cha candidates wote wanaojitokeza kutokosa kasoro.Mara nyingi mpiga kura hutafuta penye nafuu.Hata kama pana kasoro lakini pana njia ya kuifikia ile nia yake hata kama ni baada ya muda mrefu.Hata hivyo hili linahitaji voter mwenye uelewa,anayejua anachokitaka ni kipi,anakipataje na gharama zake ni zipi.Hii ndio hatua tuliyofikia watz.Huko nyuma hatukuwa tunajitambua.Hivyo hakukuwa na mwamko wa kudai haki na maendeleo stahiki kama leo.Baadae mwamko ukaanza,watu wakatambua kuna kitu wanahitaji lakini hawajui namna ya kukipata.Hawa ndio wale waliosukuma gari ya Mrema pale Jangwani mwaka 95 bila kumpigia kura.Baadae wakaelewa namna ya kukipata,bila kujua gharama ya kukipata.Hawa ndio waliompa JK 80% mwaka 2005,lakini wakaangushwa mwaka 2010.Wakagundua kumbe kuna gharama kubwa.Sio tu kumchagua mtu unayemtaka,bali pia kupambana kumwekea mfumo salama utakaombana na kuhakikisha anatekeleza matarajio.Sasa hapo pana gharama.Gharama ambayo watz leo wako tayari kuilipa.Ndio maana wanataka kubadili mfumo.Hapo ndipo tofauti yako na watz ilipo mzee wangu Slaa.Unamzungumzia mtu mmoja Lowasa.Sisi voters tunao wawili,Lowasa na Magufuli,wanaonadi mifumo miwili tofauti.Mfumo anaoutumikia Magufuli tumeuchoka.Tunataka mfumo mpya wenye tija.Kile wanachokinadi UKAWA kinatuvutia zaidi.Ila kuna jambo linatatiza.UKAWA wameweka candidate kutoka mfumo wa zamani,bwana Lowasa.Huu ndio ugomvi wako mkubwa sana dokta.Binafsi nakubaliana nawe,sikupendezwa na hatua hiyo.Lakini katika ufinyu huu wa options uliopo,inahalalisha kubakiza mfumo wa zamani?Kwangu nasema hapana.Ni vema tukabadili.Why?Nina sababu mbili.Mosi,Upinzani bado kumejaa watu wengi waliokuwa groomed huko.Haiwezekani Lowasa kuwapelekesha,ni wao watakaompelekesha.Kama Lowasa angekuja na kundi la wabunge,wenyeviti na viongozi lukuki toka CCM kama ulivyotaka wewe mzee,basi Lowasa angekuwa "liability"(mzigo) maana hilo kundi la viongozi lingeteka nguvu ya maamuzi ndani ya UKAWA na tusingejua nini kitatokea,in fact ingekuwa gambling.Lakini Lowasa amekuja na viongozi wachache sana,ila ameleta wapiga kura.Wale mashabiki wake wanaomsapoti,hao unaowaita bodaboda,mama ntilie n.k,hao ndio kawaleta.Hao hawashiriki vikao vya kamati kuu.Wao kazi yao ni kupiga kura.Hawatachukua nafasi za kimaamuzi za akina Mnyika,wameletwa kutiishwa chini ya UKAWA.Hii ni "asset". Na sitaki kuamini eti UKAWA kuna gap la uongozi,no.UKAWA kulikuwa na gap la wapiga kura.Kwa sababu ni timu mpya,inayojenga ngome yake gradually,na hii ya Lowasa ni opportunity with moderate risk,kaleta voters,sio think tanks, na UKAWA inahitaji voters,haihitaji Kingunge wengi na mimi nashukuru hao wabunge 50 hawajaja,nasema wabaki huko huko,hawa bodaboda ndo wanahitajika,huu ndio "uwezo wa Lowasa kuiangusha CCM" aliosema Lissu.Kumbuka maneno yake:"hatujamchukua Lowasa kwa usafi wake,bali UWEZO WAKE WA KUIANGUSHA CCM".Baada ya hapo atatumikia mfumo mpya,nyuma yake wakiwepo akina Duni Haji,Mbowe,Mbatia,Lissu,Marando etc nao wakiwa under pressure ya voters wa both UKAWA,CCM,etc. Huo utakuwa mwanzo wa mabadiliko kwa kuwajibishana.La pili,mimi kama voter,bado naona ni heri kuwapa nchi UKAWA na Lowasa wao,kwa sababu hii ndio njia pekee ya kurudisha uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.Siku watz tukiiondoa CCM madarakani,tutaheshimiwa na wale watakaofuatia.Utakuwa mwanzo wa kurefine uongozi wa umma.Itatokea mitikisiko,ila mbele ya safari tutapata tunachokitaka.Tutaheshimiana tu.Utapata uongozi kwa sababu wenye nchi tunakutaka na sio babako anataka!Mabadiliko haya yataleta uwajibikaji wa viongozi,na pia voters wenyewe kuwajibika kwa kile wanachokichagua,hata UKAWA nao wakizingua tunapiga chini,tunaleta wengine while learning how to get the best out of our society.Ni gradual but hii ni formula nzuri kwa maendeleo na ustawi wa any democratic state.To us,this is just the beginning.Ni hayo tu mzee wangu.Nakutakia maisha mema ila ukirudi ni vema ukawajibu hawa wanaohoji gharama za ile press conference yako.
 


Ni kitu gani ambacho Dr. Slaa alikisema ambacho wewe kwako kimekuwa kipya na kibaya sana ambacho kimesababishwa na viongozi wa CHADEMA kinachokufanya uone CHADEMA ina uongozi wakitapeli? Be specific!.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…