Waraka kwa Dr. Slaa

Waraka kwa Dr. Slaa

Criterion

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2008
Posts
11,797
Reaction score
11,899
Dr. Kwanza ninaomba nichukua nafasi hii kwa namna ya pekee nikushukuru kwa namna mlivyoshirikiana na viongzi wenzako kuinua upinzani na kutufikisha hapa tulipo. Umepigana vita vya hatari bega kwa bega na wana mabadiliko hata kutoa mwelekeo wa njia tunayoiendea sasa. Kila wakati yanapotajwa mabadiliko Tanzania, jinalako litatajwa.

Ninapenda nikushukuru kwa kuzungumza na Watanzania ambao wengi wao ni wapenzi na wafuasi wako wakubwa mimi nikiwa miongoni mwao.

Nimekusikiliza vizuri na kukuelewa kwa kiwango kikubwa. Hata hivyo nina masuala kadhaa ambayo ninaomba utusaidie kutupa maelezo kwa mtazamo wako ili tuendelee kuwa pamoja katika gurudumu la utetezi wa wanyonge uliotuthibitishia utaendelea kuwapigania bila kujali una chama ama hauna.

Kabla ya yote, ninaomba nionyeshe masikitiko yangu kwa uamuzi wako wa kuresign instantly baada ya kutofautiana na viongozi wenzako kwa sababu ninahakika tofauti zenu zilikuwa na ziko chini ya uwezo na hekima zenu za pamoja. Ninachokifahamu mimi, maamuzi yoyote yanayofanywa wakati wa hasira kali ama furaha kubwa sana, huwa hayazingatii maswala mengi ya muhimu na yenye tija kwa upana unaostahili.

Ninaomba nichukue nafasi hii kuomba ufafanuzi kwa masuala yafutayo.

1. Wakati mnapanga ujio wa Lowasa, ulitaka kujua kama ni asset kama atakuja na wenzake makini viongozi wazuri na kama ni liability ikiwa atakuja na vijana wa barabarani.

Mheshimiwa, huoni kama ingelikuwa ni vizuri zaidi kumpokea bila ulazima wa kuja na idadi fulani ya watu wenye sifa kadhaa, kama vile ambavyo CHADEMA mmekikuza kwa kumpokea mtu mmoja mmoja bila sharti la kuja na watu wengine kwa wakati huo? Kwa nini yeye Lowasa mlimwekea sharti hilo ambalo kwa watu wengine halipo?

Hoja yangu nyingine, hao unaowatambua kama vijana wa mitaani, ndio watanzania ambao walistahili kuwa sehemu za kazi lakini wamewekwa barabarani kwa utawala mbovu wa ccm. Huoni kama wana haki ya kuheshimiwa na kutambuliwa uwezo wao katika suala zima la maendeleo ikiwa kutakuwa na serikali mbadala inayowajali na kwamba wana umuhimu katika kupiga kura na kuiondoa ccm madarakani ili ije serikali sahihi?

Suala la kuhitaji watendaji wazuri kutoka ccm waje na Lowasa ili aqualify for membership, linanipa tabu. Dr. wewe ni msomi mzuri na umekuwa kiongozi wa CHADEMA kwa miaka mingi. Kama kulikuwa na knowledge gape, sikutegemea mtategemea ijazwe na watu wa Lowasa kutoka ccm mahali ambako tayari umepafananisha na choo. Kwa hali yoyote, hata kama wengelikuja, hawawezi kuwa ready made kufit kwenye utaratibu na kanuni za CHADEMA. Sasa kama ndivyo, hamkuona kabisa umuhimu wa kutengeneza watu wenu wawe kama mnavyotaka wawe kwa maslahi ya chama na taifa bila kujali wanakuja ktuoka wapi ama ni wenyeji wa mlemle CHADEMA?

2. Umeongelea suala la Demokrasia kwamba kama maamuzi ya wengi yanakuwa kinyume cha mawazo yako, unatakiwa uachie ngazi.. Ni kweli hili Dr? Siyo kwamba ni kukosa uvumilivu wa kuwachukulia wengine? Kama katika vikao watu wakitofautiana kwa ajli ya demokrasia Yule ambaye mawazo yake hajapitishwa anapaswa kuondoka, ni kwlei dunia ingelikuwa na amani au maendeleo? Watu wangapi wangelikuwa wanaondoka kwenye familia zao, maofisini na kila mahali kwa saa? Nilichokitegemea kwako Dr. ilikuwa ni uvumilivu wa kisiasa wa kuweza kuwachukulia wengine kwa kuamini kwamba, hata kama siku hiyo walikukatalia, siku nyingine au katika hatuanyingine wangehitaji hekima na maarifa yako.

Ninajua mchakato wa mabadiliko hauishii kwenye uchaguzi. Uchaguzi ni hatua za mwanzo sana lakini baada ya hapa kunahatua ya ujenzi wa taifa jipya ambapo ilikuwa ni nafasi yako nzuri kuongoza mabadiliko kwa kuhakikisha wanyonge uanaowatetea sasa wanakombolewa ki halisia.

Nili kutegemea kwamba wewe kama katibu mkuu wa CHADEMA, ulitakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha CHADEMA inapata wanachama wapya wengi bila kubagua na kuwakarabati ili makandokando wanayokuwa nayo kule wanakotoka, hayapati nafasi katika CHADEMA. Kama ulivyosema kubeba kinyesi toka chooni na kukiweka chumbani ama sebuleni, kweli ni tatizo lakini kinyesi hicho kinaweza kuwa purified na kufaa kwa matumizi mengine ya binadamu. Kilichotakiwa ni uwezo na maarifa ya kuhakikisha kinakuwa bidhaa nyingine, inayofaa kwa matumizi badaala ya kukiacha kiendelee kuwa kero. Na hizi haiba za watu si kutoka ccm tu bali hata wasio na vyama vya siasa wanapojiunga, wanahitaji kutengenezwa.

3. Umezungumzia ufasadi wa Lowasa, wakati huo huo ukihitaji aje na wenzake kutoka huko chooni. Kwenye list of shame, uliorodhesha majina ya mafisadi 11 Lowasa akiwemo. Ni kwei mchakato wa Richmond Lowasa amekiri kuhusika lakini hakueleza in details nini kilikuwa nini. Hata hivyo amewataja viongozi wa juu yake. Nilitegemea katika suala kama hili, ni vizuri Dr. ukalisaidia taifa, kwa kuzungumzia mchakato mzima, naman ccm ilivyofanya ufisadi na kuwalinda mafisadi ambao si lowasa peke yake bali genge zima la ccm akiwemo mkuu wao kama laivyotajwa na lowasa.

Wewe mtetezi wa wanyonge, tulitegemea upaze sauti ya juu ukemee ccm na serikali yake, kushindwa kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi ambao si Lowasa wala Richmond peke yake. Kitendo cha kuwasifia Sita na Mwakyembe kuongelea ufisadi bila kuonyesha kuguswa na kile alichokisema mwakyembe kwamba amekificha kwa kuogopa usalama wan chi, huoni kama umekuwa biased sana?

Tuanomba utamke report ya Mwakyembe yote bila kuacha aliyoyoaficha iwekwe hadharani, na wahusika wa wizi ule wachunguzwe na watakaobainika kuwa na hatia za kimahakama wapelekwe mahakamani. Lakini pia ili uonyeshe fairness, usiache kuzungumzia ufisadi wa meremeta, Kiwira, Kagoda, Escrow, miradi ya barabara, bomba la gas, mradi wa rea, nk. Nk. Kitendo cha kuishia Richmond tu na kuyaacha haya mengine yanayotisha zaidi yaliyoendelezwa na mafisadi ya ccm, inaweza kutafsiriwa kama chuki binafsi dhidi ya Lowasa. Makosa yote ya ufisadi yzungumziwe na yapewe uzito unaostahli bila upendeleo.

4. Dr. kitendo cha kuwashambulia CHADEMA kwa kumpokea Lowasa, fisadi mmoja aliyeamua kubadilika na kufuata sera za CHADEMA, huku ukiwalinda ccm ni kupigia kampeni ccm kwa kuwafichia makosa yao ambayo hasa ndiyo chimbuko la wewe kujibainisha kama mpigania haki za wanyonge (watu wa barabarani). Ninaomba upate muda mwingine, uzungumzie nini kilikufanya ujiunge na vyama vya upinzani, na nini sababu ya kuwa na wimbi kubwa la watu wanyonge Tanzania ambao unahitaji kuendelea kuwapigania dhidi ya nani adui yao na ametoka wapi.

5. La mwisho katika orodha lakini la kwanza kwa umuhimu, ninaungana na wewe kukemea maneno ya waropokaji kwamba wataitoa ccm hata kwa mkataba na shetani kwa sababu ni maneno yanayovuta laana katika nchi. Haiti walitamka maneno kama yale wakati wanapigania uhuru na shetani amekaa kwao akiwatesa vizaz na vizazi. Hatumhitaji shetani katika ukombozi wa taifa hili. Ninafuta kauli hizi na NINAUNGAMA DHAMBI HII MBAYA KWA NIABA YA WATANZANIA WOTE NA VIZAZI VYETU, MUNGU ATUSAMEHEE, ASITUHESABIE UOVU HUU, KATIKA JINA LA YESU KRISTO. Natamka atakayeendeleza kufufua maneno yanayompa shetani utukufu, kwa kiburi, afanye hivyo kwa gharama yake binafsi na si gharama ya watanzania.

Tulianza na Mungu, tunaendelea Mungu na Tutamalizia na Mungu ambayek sisi na vizazi vyetu tutamtumikia daima.

Vinginevyo sisi tunasonga mbele na ukombozi kama jeshi lenye nguvu na umoja. Tutapigana vita kwa kuheshimiana, kupendana na kushikamana. Wakati wote tutakapo tofautiana kim itazamo kwa kuwa ni binadamu, tutamaliza tofauti zetu kwa majadiliano bila kusalitiana na kuumizana. Atakayeonyesha kuchoka, hatutamtupa, tutamganga huku tukisonga mbele. Atakaye amua kurudi nyuma kwa sababu yoyote, tutalinda uhuru wake lakini tutaepuka madhara yake kwetu. Tumeshaamua kuiondoa ccm na kuweka utawala utakaojali Watanzania badala yakusita sita huku ccm ikipanga kutumalizia.

Ninategemea utaendelea kuwa upande wa ukombozi wakati wote tunapopigana vita na wakati tutakapokuwa tukianza kujenga Tanzanai mpya chini ya katiba mpya ya wananchi na mifumo mipya kwa maslahi ya Tanzania ya sasa ni vizazi vijavyo.
 
Hatuwezi kulilia Tanzania MPYA, SAFI na iliyokombolewa ikiwa tutaruhusu FISADI papa kukaa kwenye jumba letu la state house.

Hivyo basi, kama tunahitaji mema kwa nchi yetu, chaguo la pekee ni Magufuli tu.
 
Ni afadhali kuongozwa na fisadi mmoja aliyetubu na kubadilika, ambaye atawatetea Watanzania kwa kuongozwa na kundi la watu wasafi, kulilko mtu mwenye hila mmoja aliyewekwa chambo ili aongozwe na rundo la mafisadi nyangumi walioko ccm. Mbona hamsemi mafisadi wa meremeta, kagoda, barabara, escrow, epa, n.k walioko ccm mmewafaya nini?

Tumia akili yako vizuri.

Ni afadhili kukaa na donge moja la maji chumbani kuliko kuishi kwenye shimo la choo.

Tunamchagua Lowasa chini ya UKaWA, kwa Tanzania mpya!.
 
Unajidanganya na Magufuli, hivi kuna mtu ndani ya CCM aliyesafi? Hivi kwanini Watanzania wamekuwa na masikio ya kufa? Magufuli ni fisadi kama wanaCCM wenzake, na ufisadi ukiwa CCM ni ule wa utake usitake sababu mfumo wa CCM umekuwa hivyo miaka nenda rudi. Ni wazi kuwa Lowassa naye akiwa ndani ya CCM alikuwa ni fisadi by default LAKINI ukiwa ndani ya ukawa unakutana na mfumo mwingine ambao unakufanya unakuwa mwanamabadiliko by default.

Magufuli hawezi kufanya maajabu ndani ya li-mfumo lililooza kwa miaka zaidi ya hamsini, hawezi hata angefanyeje, JK yamemshinda na aliishia kuwaambia wezi warudishe pesa (na mpaka leo hatujui ni akina nani na walirudisha kiasi gani) wakati wezi wa kuku wanafungwa jela.

Sitampigia kura Lowassa sababu ya usafi wake bali nitampigia kura sababu yupo kwenye mfumo ambao unakiu ya kuleta mabadiliko. CCM wamekuahidi miaka yote hiyo lakini bado watu ni maskini -najua hata wewe unayesoma huu uzi ni maskini na sababu ya umaskini wako ni moja nayo ni CCM, naona ajabu sana kusikia mtu anaamini kuwa Magufuli na CCM yake wataleta mapinduzi ya maendeleo.
 
Ni afadhali kuongozwa na fisadi mmoja aliyetubu na kubadilika, ambaye atawatetea Watanzania kwa kuongozwa na kundi la watu wasafi, kulilko mtu mwenye hila mmoja aliyewekwa chambo ili aongozwe na rundo la mafisadi nyangumi walioko ccm. Mbona hamsemi mafisadi wa meremeta, kagoda, barabara, escrow, epa, n.k walioko ccm mmewafaya nini?

Tumia akili yako vizuri.

Ni afadhili kukaa na donge moja la maji chumbani kuliko kuishi kwenye shimo la choo.

Tunamchagua Lowasa chini ya UKaWA, kwa Tanzania mpya!.

Huyo fisadi katubu lini na nini? Hebu zinduka! Alafu ilani yenu ya Chadema na Ukawa iko wapi? Mmekubaliana nini na huyo fisadi wenu? Hujui lolote unashabikia tu!
What a hollow statement and a sad state of mind!
 
Atubu kwani yuko kanisani? Amtubie nani? Hizi ni siasa! Ameshasema na kusema na kusema mwenye ushahidi apeleke mahakamani
 
Naona baada ya Slaa kuwaeleza Watanzania ukweli vizuri, Team Lowasa wamekuja kwa nguvu nyingi hapa jamvini kujaribu kuokoa jahazi.

Kuna ushahidi Lowasa ni fisadi. Bila huo ushahidi wala hangejiuzulu Uwaziri Mkuu. Na anashirikiana na mafisadi papa ambao wanatumia rushwa na hongo kwenye kampeni zake. Hatutaki kutoa mafisadi kwa kutumia mafisadi na kuendelea kutawaliwa na mafisadi.

Nampa hongera sana Dr Slaa kwa kuwa na msimamo thabiti. Watu wa aina yake ndiyo wanatakiwa watawale Tanzania. Mwanzoni tulidhani washirika wake kama Lissu na Mnyika ni watu wenye msimamo pia, but now we know better. They caved in at the slightest indication that they could be co-opted into the ruling oligarchy. Shame on them. They have sold out!

Dr Slaa alikwishasikika akisema kuwa akiwa rais atamfikisha Magufuli mahakamani kwa kuuza nyumba za serikali kifisadi . Kisha amesema Lowasa naye ni mchafu hafai kuwa rais.

Lakini hajawaambia watanzania wampigie kura nani! Ni bahati mbaya kwamba waandshi wa habari walisahau kumuuliza hili swali: Sasa kura tumpe nani? Magufuli au Lowassa?
 
Hatuwezi kulilia Tanzania MPYA, SAFI na iliyokombolewa ikiwa tutaruhusu FISADI papa kukaa kwenye jumba letu la state house.

Hivyo basi, kama tunahitaji mema kwa nchi yetu, chaguo la pekee ni Magufuli tu.

Mlishindwa na hamjawahi kuthibitisha ufisadi wa Lowasa.
Tunarudia tena Magufuli hana weledi wa kusimamia mali za umma, tunayo kumbukumbu sahihi magufuli aliuza nyumba za serikali kwa ndugu na vimada wake.
 
Mlishindwa na hamjawahi kuthibitisha ufisadi wa Lowasa.
Tunarudia tena Magufuli hana weledi wa kusimamia mali za umma, tunayo kumbukumbu sahihi magufuli aliuza nyumba za serikali kwa ndugu na vimada wake.

Dr Slaa alikwishasikika akisema kuwa akiwa rais atamfikisha Magufuli mahakamani kwa kuuza nyumba za serikali kifisadi . Kisha amesema Lowasa naye ni mchafu hafai kuwa rais.

Lakini hajawaambia watanzania wampigie kura nani! Ni bahati mbaya kwamba waandshi wa habari walisahau kumuuliza hili swali: Sasa kura tumpe nani? Magufuli au Lowassa?

Dr. Slaa anauwezo wa kuongea anachojisikia lakini hana uwezo wa kuwalazimisha watanzania wachague chama wala mtu wasiyemtaka. Anabaki na kura zake mbili ambazo ni lazima zifanane. Watanzania wamechoshwa na mateso, dharau, hadaa, ubabe na hujuma za ccm na viongozi wao.

Atuambie uchafu wa lowasa mkubwa ni upi kati ya haya.

Tuhuma za ufisadi ambazo aliwajibishwa na ameshasema mwenye band ile ni Kikwete na kikwete pamoja na serikali yake wamenywea hata kukanusha wameshindwa, tuhuma ambazo wenye ushahidi wameshindwa kumfikisha mahakamani ili ahkumiwe? AU ni kushindwa kuja na viongozi wazuri kutoka ccm na badala yake kuja na kundi kubwa na watu wa barabarani wasiokuwa na kazi?

Shutuma za Dr. Slaa zingekuwa na uzito kama angelizielekeza kwa ccm kwa kushindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi ili ama wahukumiwe/wasafishwe ijulilkane mbichi na mbivu.

Mtu mwenye kujitambua, namwenyenia njema, hawezi kum attack Lowasa kwa ufisadi ambao srikali ilishindwa hata kumshtaki na ikanyamaza kwa miaka 8 na kisha chama chake kikampa na form za kugombea uraisi.

Halafu unaacha kuongelea rundo la mafisadi wa EPA, MEREMETA, KIWIRA, RICHMOND, RADA, NDEGE YA RAISI, KAGODA, ESCROW, UJENZI WA BARABARA, REA, BOMBA LA GAS ambao wamejazana ccm wakimezea mate miaka mitano ijayo ili waendelee kumalizia nchi yetu.

Kama unania ya dhati na nchi huwezi kumshupalia lowasa aliyeamua kuweka bayana kwamba richmond ni Kikwete, ukaacha kuongelea uhamishaji wa wanyama wetu, matumizi mabaya ya rasllimali za taifa na uharamia unaofanywa na ccm chini ya kikwete kiasi sasa haandamani ya magufuli na hadi kuficha NENO CCM ili kuwahadaa watanzania wasiowapenda.

TUNAHITAJI MFUMO MPYA CHINI YA UKAWA KUJENGA TAIFA JIPYA.
 
Sikutegemea kama Dr Slaa anaweza kuwadharau wananchi kiasi hiki, Eti tulitegemea Lowasa angekuja na watu wazito na sio waendesha boda boda" katika kauli za Dr zilizo nichefua ni hii.. Hawa waendesha boda boda si ndio walio mfikisha hapa Dr.. Walipigwa mabomu na wengine kupoteza maisha wakiwa mstari wa mbele kwenye harakati za mabadikiko.. Leo nani anampa kibri na kuona hawa watu hawana thaman.. Dr umekuja kama upepo na utapita kama upepo.. Mabadiliko yako pale pale

Ungekua na dhamira ya dhati yakutetea wanyonge ungebaki kuhakikisha hao waliokuja na uchafu kuharakisha mabadiliko, Unakua wakwanza kuhakikisha wanafuala mlongo walio ukuta. Na sii kukimbia
 
Dr Slaa hakuwadharau usitake kupindisha na kumfanya Lowassa ndo watetezi wa wanyonge. Lowassa alisema atakuja na wabunge 50 na ndiyo nguvu yake kubwa kwani ataipasua CCM
Sasa anapoonyesha kuwa nguvu yake ni waendesha bodaboda tena asilimia kubwa wamehongwa kuja hapo ni dhahiri huyu Lowassa ni msanii.
So hebu ondoa your false indignation na usitake kupindisha kilichosemwa!
 
Katika biblia kuna Mtu Mmoja aliitwa sauli, ambae ndio Mtume Paulo

Alikuwa muuaji na akiwatesa sana Wakristo, siku moja akakutana na Mungu akamwambia mbona unawatesa watu wangu, akambadili jina palepale akamwambia Tangu leo wewe ni Paulo, Uutangaze Ukristo

Tangu siku iyo huyu jamaa akabadilishwa ndio alitangaza ukristo haijawai tokea. Katika biblia ana vitabu Zaidi vitano kaandika. wagalatia, waefeso, wafilipi, watesalonike, wakolosai. nk nk

Muuaji aliekuja kuwa shujaa wa Ukristo.

Nakifananisha kisa hiki na story za kumuita Edward Lowasa fisadi, Sawa, yawezekana ni kweli, kama Paulo alivokuwa Muuaji, lakini Mungu amemuita Lowasa, asiwe tena Sauli Mtesaji na Muuaji bali (Paulo Mueneza ukristo).

Mungu hutumia wadhambi maana hajawai zaliwa malaika.

Lowasa, umetumwa na Mungu kutupeleka kaanani, TUTAFIKA.

Musa hakuiona kaanani lakn waisrael walirudi Nyumbani na walifika. Lowasa ameletwa kuturudisha Nyumbani. Tutafika.
Na haturud Misri.
 
Sikutegemea kama Dr Slaa anaweza kuwadharau wananchi kiasi hiki, Eti tulitegemea Lowasa angekuja na watu wazito na sio waendesha boda boda" katika kauli za Dr zilizo nichefua ni hii.. Hawa waendesha boda boda si ndio walio mfikisha hapa Dr.. Walipigwa mabomu na wengine kupoteza maisha wakiwa mstari wa mbele kwenye harakati za mabadikiko.. Leo nani anampa kibri na kuona hawa watu hawana thaman.. Dr umekuja kama upepo na utapita kama upepo.. Mabadiliko yako pale pale

Ungekua na dhamira ya dhati yakutetea wanyonge ungebaki kuhakikisha hao waliokuja na uchafu kuharakisha mabadiliko, Unakua wakwanza kuhakikisha wanafuala mlongo walio ukuta. Na sii kukimbia

Kiongozi,ninaumia sana ninapotafakari kauli ya Dr. Slaa, kuungana na Mkapa kuwatukana vijana ambao wamefanya vile walivyo na utawala dharimu wa ccm bila ridhaa yao.

Imenisikitisha sana kuona namna vijana hawa walivyojitambua na jinsi walivyotayari kujitoa kwa hali ya mali kiasi hata cha kumwaga damu yao ili kulikomboa taifa kutoka mkoloni ccm, na ambao yeye Dr. anajitambulisha kuwatetea, jinsi Dr. alivyowageuka na kuwadharau.

Kweli wanawake hugeuza mioyo ya wafalme!.

Ninaita wito kwa vijana wangu, msiogope wala msifadhaike. Tulianza na Mungu, tuko na Mungu na Tutamaliza na Mungu.

Kwa umoja wetu, tunakwenda kuikomboa nchi. Tusiwaangalie wanaoshindwa njiani na wala wasitukatishe tamaa.

Tunasonga mbele hadi ukombozi umepatikana. Tanzania ni yetu na sisi ndio wenye nchi. Hatutakubali tena kuwa watumwa wa ccm ndani ya nchi yetu.

Tanzania is and shall always belong to Tanzanians!.

Aluta kontinua, Mapambano yanaendelea.

PEOPLESSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSSS!.
 
Kama kweli Dr. Slaa anasimamia Ukweli kwa anachokisema, siku hiyo tr 28 angetueleza haya aliyoyasema jana. Yeye anashiriki dhambi kisiri harafu anakuja hadharani kukana. Angekataa toka mwanzo kumpokea mtu mchafu katika chama, anataka kututumia vijana kuikomoa chadema kwa kuwa haikufuata matakwa yake. Dr utakuwa umechelewa tumeshaamua ngoja kwanza tungo'e shina(ccm) ndipo tukate matawi. Nawaomba viongozi mlioko front line(team campain) msigeuke nyuma kujibu mashambulizi yanayotokea nyuma(dr) hii ni janja ya adui, hayana madhara songeni mbele. Mabadiliko yapo palepale. Ngoja tuendelee kumpumbaza, dr slaa naomba unijibu;. Ulisema ukishinda uraisi utampeleka magufuri mahakamani kwa ufisadi aliofanya, je leo hii amekuwa msafi kwa kuukoswa uraisi?... Nimesikia ukiilalamikia serikali kuzuia ndoa yako, na ukasema Mungu ameshaibariki. Rejea maandiko...Kitakachokatazwa duniani kimekataliwa na mbinguni... Usilazimishe. Dr ndoa yako imezuiliwa.
 
Chadema ni Kanisa na Uokovu? Kasisi Mkuu ni nani? Naona mnatangaza toba tu za watu, ingawa hatujawasikia hadharani wakisema wanajuta kwa waliyoyafanya. Hata Sumaye Jana songea anasema, CCM ilitakiwa itoke siku nyingi sana, akasahau Miezi miwili iliyopita aliomba ridhaa ya CCM awe Rais wa nchi hii. ( Umazwazwa ).
 
Back
Top Bottom