Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Ukitaka balaa na kuleta chokochoko na hata kusemwa mabaya yako basi wee kosana na KANISA KATOLIKI.

ALIANZA MEMBE NA HOJA YA OIC. KANISA WALISEMA APEE RED CARD.

SASA TUSUBIRI TAMKO LA PENGO DHIDI YA KINGUNGE. ( NAFIKIRI LIMESHAANDALIWA SASA LINAPITISHWA KWA BALOZI WA VATICAN NA KISHA POPE LIPATE BARAKA KABLA YA KUTOLEWA.

HAKIKA WAKATOLIKI WANAJIONA KAMA WANAONGOZA TANZANIA KWA REMOTE CONTROL
 
Guys usomeni vizuri na muhimu ni kujua lengo la Ilani ya Wakatoliki. Tukumbuke,......"The Great Civilization Cannot Be Conquered From Without Until It Has Destroyed Itself From Within........."
 
Hakika mimi naona kama wao maaskofu wanajiona wasafi na waadilifu vya kutosha. KWANINI WASIVUE NGUO ZAO NA KUVAA KAMA ZA DR SLAA YAANI WAACHANE NA DINI WAINGIE KUGOMBEA UONGOZI KUPITIA KURA ZA WANANCHI ILI WAENDE BUNGENI KUWEKA MAMBO SAWA.

TUNAONA MFANO MZURI WA DR SLAA. SASA NA VIONGOZI WENGINE WA KIROHO WAIGE MFANO WAKE KWANI KUKIWA NA AKINA SLAA KAMA 30 BUNGENI BASI NCHI ITAENDELEA
 
Nimetuma Ilani kama attachment kwenye moja ya michango yangu, jaribu kuushusha upate nakala
 
Last edited:
Kama Kingunge anadhani Maaskofu na mapadre ni kama wale aliowadangaya alipoitisha mkutano wa waandishi wa habari pale maelezo, basi atakuwa anachemsha. Atakuwa anajimaliza kabisa, walau hata sasa anaweza kujaribu kuongea.

Ni kweli makanisa na misikiti yako organised, hoja ikipangwa vizuri juu basi inaweza kufika chini na ikatekelezwa. Huenda ukombozi wa nchi ukaanzia hapo.

Kinginge na hana dini sidhani kama anajua busara za yaliyomo kwenye dini, much better akiongelea yale ya wasio na dini kama yeye.
 
KIngunge mbona hata kipengele kimoja kinachogawa nchi hujatuonyesha? unaongea kiujumla jumla tu? au matatizo ya kutokwenda shule. Wenzio makini akina DR.Slaa wanakuja na nyaraka na kusoma kipengele au kunukuu penye utata. Waraka umeuita wa kuelimisha wapiga kura, tatitizo nini madhehebu mengine wakielimisha watu wao?isitoshe wagombea watateuliwa na vyama vya siasa na siyo madhehebu.Umechoka tuachie nchi yetu kafie mbali huko
 
Ukitaka balaa na kuleta chokochoko na hata kusemwa mabaya yako basi wee kosana na KANISA KATOLIKI.

ALIANZA MEMBE NA HOJA YA OIC. KANISA WALISEMA APEE RED CARD.

SASA TUSUBIRI TAMKO LA PENGO DHIDI YA KINGUNGE. ( NAFIKIRI LIMESHAANDALIWA SASA LINAPITISHWA KWA BALOZI WA VATICAN NA KISHA POPE LIPATE BARAKA KABLA YA KUTOLEWA.

HAKIKA WAKATOLIKI WANAJIONA KAMA WANAONGOZA TANZANIA KWA REMOTE CONTROL

Hivi jamani,mbona huu waraka ukiusoma hauoneshi ubaya wowote au mkubwa hivyo kama unavyotangazwa? aidha hakuna sehemu yoyote inayowaagiza wakatoliki wamchangue kiongozi fulani au wa kikatoliki? viongozi tunaoombwa tuwachague kulingana na huo wa waraka niwa sifa zilezile zinazokubalika katika jamii. Nadhani kila mtu hapa anapaswa kuusoma vizuri sana huu waraka ndo tujadili sasa
 
HIVI SASA KINGUNGE AMEANDAMWA ,matusi yote dhidi ya kingunge ni baada ya kutofautiana na waraka wa kanis katoliki. HONGERA KINGUNGE. TUPO PAMOJA KINGUNGE HANA DINI NA SIO MKIRISTO NDIO MAAN KAANIKAKANISA HADHARANI
hata membe yalimkuta kama haya wakati wa hoja ya oic
 
Kingunge na kanisa wote wana issues.

Kanisa kwa kujiingiza katika issue delicate ya kisiasa, Kingunge kwa kuingilia uhuru wa kujieleza. And there is no contradiction.
 
Kanisa Katoliki lagoma
Imeandikwa na Mwandishi Wetu Habari Leo; Tarehe: 16th July 2009 @ 17:33

KANISA Katoliki limekataa kuuondoa waraka wake kuhusu elimu ya uchaguzi na limewashangaa wanaouogopa.

Kanisa hilo limesema, limefunga mjadala kuhusu waraka huo, unafaa, na halitamjibu yeyote atakayehoji uhalali wake.

Limesema, waraka huo ni nguvu ya hoja na si ya kiimani, kila mtu anaruhusiwa kuwa nao bila kujali dini, kabila au rangi.

Kwa nyakati tofauti, Kanisa Katoliki limewahi kusema kuwa waraka wa elimu ya uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani na ule wa mwaka 2015 unafaa na hauna tatizo lolote.

Kwa mujibu wa uongozi wa kanisa hilo, halihitaji mjadala na mtu yeyote kuhusu waraka huo hivyo, watu wenye mapenzi mema wausome na kuuelewa kabla ya kuujadili.

Askosu Mkuu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini amesema, Kanisa hilo limetoa baraka kila mtu mwenye mapenzi mema autumie waraka huo kama jukumu mojawapo la kanisa kuelimisha jamii kimwili na kiroho.

Askofu Kilaini amesema, si mara ya kwanza kwa kanisa hilo kutoa waraka kama huo ila anadhani umewagusa sana watu kwa sababu umegusia suala la ufisadi.

Kanisa hilo limesema, halitamjibu chochote Mbunge wa Kuteuliwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru kwa kuwa linamheshimu.

Kanisa hilo limemshauri Ngombale mwiru aainishe eneo lenye utata katika waraka huo ili kanisa nalo lifahamu kasoro za waraka huo badala ya kutoa hoja juu juu.

"Nina muheshimu sana yule mzee, kachangia sana kujenga taifa hivyo heshima yangu kwake ni kubwa na nisingependa kumjibu ila faida ya wengine ni kwamba nchi hii si ya chama kimoja bali kila mtu ana uhuru wa kusema, na hao wanataaluma wametumia haki hiyo kutoa maoni yao, watu wautafute waraka maana unapatikana na wausome ili wapate mantiki yake kwa kina," amesema Kilaini.

Kilaini amesema leo kuwa, kama kuna mtu anaona unahatarisha amani abainishe wazi kipengele husika kwa hoja, na kwamba, suala si kuuondoa au kuuacha.

"Tumeshazungumza sana suala hili, kanisa limejaliwa neema za kuwa na taasisi nyingi ndani yake na hii ya Wanataaluma Wakatoliki ni moja wapo, hivyo hao wametoa maoni yao ambayo kanisa imeyapa baraka kutumika kwa kila mtu mwenye mapenzi mema kama jukumu moja wapo la kanisa kuielimisha jamii kimwili na kiroho" ameisema Kilaini.

"Hao wanaoogopa sijui ni kwa nini? kama nilivyosema awali wabainishe kipengele chenye shida na ikumbukwe si mara ya kwanza kutoa waraka kama huu, unatoka mara nyingi, wa kwanza waliutoa mwaka 1989 na wameendelea kutoa nyaraka nyingi, naona kipindi hiki inawagusa watu sana kwa kuwa ufisadi umeguswa humo, waraka huo ni nguvu ya hoja na si nguvu ya kiimani na kila mtu anaruhusiwa kuwa nao bila kujali dini, kabila wala rangi."


Kilaini amesema, taasisi za dini zipo huru kuchangia mawazo endapo zikiona suala hilo lina maslahi kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Kilaini, kilichofanywa na Kanisa Katoliki si kitu kipya, ni utaratibu wa kawaida.

Naye Katibu wa Habari wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Modesti Katonto amesema,kanisa liimefunga mjadala kuhusu waraka huo.

Amesema, kanisa halimjibu Kingunge au yeyote atakayetaka malumbano kwa kuwa limetimiza wajibu wake.

Padri Katonto amewaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam kuwa, kanisa halina nia mbaya na liliubariki baada ya kuusoma kwa kina na kuona unafaa.

Ngombale Mwiru jana aliliomba Kanisa Katoliki liuondoe waraka huo kwa madai kuwa unahatarisha mshikamano wa taifa.

Mbunge huyo alisema bungeni mjini dodoma kuwa, kutolewa kwa waraka huo ni dalili za nchi kuanza kubabaika juu ya mshikamano wa udugu ambao ndiyo utamaduni wa nchi.

"Nasema hivi, kwa heshima zote, nawaomba viongozi wa Kanisa Katoliki warudishe mwongozo wao. sisi tunataka nchi moja, watu wameshikamana, hatutaki kugawanyika kama Lebanon" alisema Mbunge huyo.
 
Kingunge na kanisa wote wana issues.

Kanisa kwa kujiingiza katika issue delicate ya kisiasa, Kingunge kwa kuingilia uhuru wa kujieleza. And there is no contradiction.
Nakubaliana na wewe hakuna tofauti tena si tu viongozi wa kanisa ni viongozi wa dini zote. Ndio hao huwasadia kupiga kampeni in return wakitarajia na wao kuwaita kwenye harambee au kupewa upembeleo. CCM wanahofu kupoteza na viongozi wa dini wanahofu kupoteza. Si wengine tunanyoosha vidole kwa wote I have nothing to loose maana CCM haijanisaidia wala dini haijanifaa. Tutapambana na wote hakuna wakufurukuta this tym. Kuna nch nyingi zilizoendelea hawa viongozi wa dini hawana influence kama Tz. Dini zimebaki pembeni na serikali zinakwenda. In no way mpaka kieleweke
 
KIngunge mbona hata kipengele kimoja kinachogawa nchi hujatuonyesha? unaongea kiujumla jumla tu? au matatizo ya kutokwenda shule. Wenzio makini akina DR.Slaa wanakuja na nyaraka na kusoma kipengele au kunukuu penye utata. Waraka umeuita wa kuelimisha wapiga kura, tatitizo nini madhehebu mengine wakielimisha watu wao?isitoshe wagombea watateuliwa na vyama vya siasa na siyo madhehebu.Umechoka tuachie nchi yetu kafie mbali huko


Jamani, haka kababu ketu nadhani tukasamehe, tena tukasemehe bure, unajua saa hizi ndo kapo katika ile negative growth, thinking capacity yake inapungua kwa kasi sana, Labda tumshauri Kinje amsaidie huyu babu, akamchukulie vidonge vyenye zinc, na pia kuna dawa za GNLD zinasaidia sana kurutubisha ubongo kwa watu kama hawa, hizo dawa ni ghali kidogo, but anyway kale kafisadi kanazo pesa za ubungo terminal, kwahiyo kanunulieni, kameze, pia kaambie kapumzike kaachane na haya mambo hakayawezi tena!
Sasa hivi siyo zama za kuja na bla bla za hiki kitu ni kibaya bila kuchambua na kuonyesha ubaya wake nini!
 
Naomba mtumieni Kingunge nilichoongelea kwenye Waraka wa Mchungaji na muulizeni kama hiki kinahatarisha usalama wa Taifa!

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...lan-restoration-recovery-plan-tanzania-6.html

Uongozi; Serikali, Utawala, Dola
Tanzania (Tanganyika na Zanzibar) zimebahatika kuwa na awamu si chini ya nne za uongozi wa Serikali kuu, ingawa kwenye Bunge na Mahakama, watumishi wake wameendela kuwa ni wale wale kwa muda mrefu.

Tatizo kubwa tulilonalo kama Taifa ni ufinyu wa viongozi bora na utashi binafsi wa wachache walio katika nyanja za uongozi kwa kukosa sifa muhimu kwa viongozi. Mzee Mwinyi amesema majuzi kuwa Tanzania ina viongozi wasomi wasioelimika. Kauli hii ni ya kweli na ni ya msingi kutambua kuwa uongozi si lelemama, ni kipaji na ni kazi ngumu.

Uongozi ni kujitolea na kuweka matwakwa na maslahi ya wengine kuwa mstari wa mbele na si matakwa binafsi na kujinufaisha. Marehemu John Kennedy rais wa Marekani alitoa kauli moja maarufu iliyosema kuwa “kiongozi ajiulize ni vipi atalitumikia Taifa na si Taifa kumtumikia yeye Kiongozi” Umashuhuri na uzuri wa Kiongozi unatokana na hekima, busara, uchapakazi, ufanisi, ufuatiliaji, uimara, uungwana, uwajibikaji na unyenyekevu wake. Ama fikra endelevu na upeo wa kuongoza ni muhimu na si kauli tamu au uzuri wa sura.

Uwezo wa Tanzania kuwa na maendeleo ya kweli utaanza na Uongozi bora.

Uongozi bora ni ule;
· wenye mapenzi ya kweli na dhati na kujivunia Utaifa wake
· wenye kujali na kulinda maslahi ya Taifa lake na watu wake
· wenye uwezo wa kupanda mbegu imara ya Uzalendo kwa kila mwananchi bila kujali itikadi, rangi, kabila, dini, elimu, umri au jinsia
· wenye uwezo wa kuhamasisha na kuchochea juhudi za maendeleo ya jamii, umma na Taifa
· wenye nidhamu, watiifu, kuwajibika, tija, ufanisi, kujituma na ufuatiliaji wa hali ya juu
· wenye usikivu, uungwana na unyenyekevu kukiri makosa, kukubali kukosolewa na kupokea na kufanyia kazi maoni ya wengine
· wenye uwezo wa kufanya kazi, kufikiri, kuwa na upeo na wepesi wa kukabili na kufanya maamuzi magumu
· usiolea uzembe, ubaguzi, unyanyasaji, uhujumu, ubadhirifu, rushwa, kudharau, kudhalilisha, kujuana au kulinda maslahi ya wachache au kikundi Fulani

Wajibu wetu kama Taifa na haki yetu kama wapiga kura kuchagua viongozi kutuongoza unabidi uachane na mfumo duni tulioujenga wa kuangalia sura na chama na tuangalie wagombea wetu wa uongozi kwa vigezo hivyohapo juu ili kuunda tabaka jipya la viongozi ambao ni wachapakazi na watakuwa manahodha wazuri kutuongoza katika safari yetu ya kulijenga Taifa.

Tukilegalega katika hili na kupuuzia wajibu juu mkubwa na kuendelea kuchagua viongozi na wawakilishi wabovu, tutakuwa hatuna sababu yeyote kulia na kulalamika kuwa tu masikini au wanyonge kwa kuwa ni Ujinga na Upumbavu wetu kutumia akili na busara zetu tulizopewa Mungu tumekimbilia kurudia makosa ya kuwapa dhamana ya uongozi watu ambao hawafai kutuongoza.

Tuchague viongozi si kwa kuangalia vyama au sura, bali tuangalie uwezo wao wa kuongoza, kuhamasisha na kufanya kazi. Tupime kauli zao na matokeo ya kazi zao kama wanavyojinadi.
Serikali ni watu, inaundwa na watu tuliowachagua na tunawapa watu hawa na Serikali mamlaka makubwa ya kutuongoza, kupanga na kulinda Taifa na Katiba yetu. Dhamana hii imefanywa kwa kuaminiana kuwa Serikali itafanya kazi kwa manufaa ya Wananchi wake na kwa matakwa na utashi wa Wananchi wake.

Inapotokea kuwa Serikali inafanya kazi tofauti na dhamana iliyopewa, ni wajibu na haki ya kila Mwananchi kudai na kuhoji mapungufu yanayoonekana au kuzungumzwa. Ni wajibu wa Serikali na Uongozi kujibu na kuwajibika kwa Wananchi waliowapa dhamana ya kuongoza Taifa.
Ikiwa Serikali na watendaji wake na Viongozi wanashindwa kufanya kazi zao kama wanavyotegemewa kuzifanya na kushindwa kutimiza matarajio ya Wananchi na Taifa, ni wazi kuna umuhimu wa kupima uwezo wa viongozi na kuhoji Uzalendo wao na kama bado wanastahili kulitumikia Taifa.

Kuanzia Rais, Mawaziri, Majaji, Mahakimu, Wabunge, Wakuu wa Taasisi na Mashirika, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Polisi, Magereza,Jeshi na watendaji wengine wa Serikali, tumaini la Watanzania na Taifa ni kuwa watu hawa wamepewa nafasi hizo kwa kuwa wanauwezo wa kitaaluma na kiutendaji kuwa viongozi na walinzi wa nguzo za Taifa letu kupitia Katiba na Sheria zake.
Hivyo basi pamoja na kuwa ni jukumu la sisi kama Raia na Taifa kudai uwajibikaji, lakini uzito wa kuhakikisha ufanisi wa Uongozi na uwajibikaji wake utaanzia na Mkuu wa Nchi ambaye ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu.

Wasifu wa Uongozi bora nilioutaja hapo juu, si wa Rais pekee, ni wa kila mtu aliye kiongozi na ni shurti kila Mtanzania aishi kwa kuviangalia na kuvitumikia vipengele hivyo bila kujali yeye ni Kiongozi au la.

Serikali yetu ni kubwa sana na ina watendaji wengi ambao sitaficha kusema kuwa asilimia 55% hawastahili kuwa viongozi kutokana na kushindwa kuwa na sifa nilizozitaja hapo juu.

Hii ni hatari sana kwa Maendeleo na Usalama wa Taifa letu. Hatuwezi kuendelea kujiongoza kiholela huku zaidi ya nusu ya viongozi wetu hawana Uzalendo au uchungu na nchi yao. Swali kwako Mtanzania ni kwa nini basi ukubali kuendelea kujichagulia viongozi wabovu wasiofaa na kuwapa dhamana kubwa sawa na kumpa Simba jukumu la kulinda Mbuzi wako?

Kinachokosekana kutoka Uongozi Mkuu hasa Urais na hata Mawaziri ni uwezo wa kudai kwa nguvu uwajibikaji na uadilifu. Hadithi na tuhuma za ufisadi zilizotawala Taifa letu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 ni kutokana na kuwa na Uongozi dhaifu, usiojali maslahi ya Taifa, uongozi uliojaa woga na kulindana na kushindwa kusimama kidete kulinda rasilimali za Taifa letu.

Viongozi wakuu wa jamii kuanzia wakuu wa vijiji, kata, tarafa, wilaya, mikoa hata Taifa, wameendelea kufanya kazi bila kupimwa na waajiri wao wawe Wananchi au Serikali kuu kuhusiana na ufanisi na uwezo wao katika safari ya kulijenga Taifa na kuleta maendeleo.

Mapendekezo yangu ambayo yataanzia na wewe Mtanzania ni kuwapima viongozi wako kwa kutumia vipimo vyepesi sana. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo;
· kupitia ripoti za kila mwezi, robo, nusu na mwaka mzima za maendeleo na kupima mafanikio na matatizo ya shughuli za maendeleo
· kuhoji na kuhakiki viwango vya kuongezeka vita dhidi ya ujinga katika wilaya au mikoa kupitia shule za msingi, sekondari, vyuo na elimu ya watu wazima
· kuhoji maendeleo ya afya kupiga vita maradhi, kuangalia takwimu za kupungua vifo vya Uzazi, vifo vya watoto, kupungua kwa uadimu wa lishe na magunjwa kama Kwashiakor, Utapiamlo, kupungua kwa magonjwa na vifo vya Malaria na Ukimwi
· ongezeko la nyumba bora, maji safi, barabara nzuri, shule, hospitali na zahanati, vyanzo vya ajira, viwanda na shughuli za kilimo
· hifadhi za chakula kukabiliana na njaa, mauzo ya mazao ya biashara na chakula
· matumizi bora ya fedha za bajeti ikiwa pamoja na kubana matumizi yasiyo ya muhimu, kudhibiti matumizi na mahesabu ya fedha za bajeti za matumizi na maendeleo
· kukagua na kuhakiki shughuli za maendeleo kuwa ni endelevu na kuhakikisha hazizoroti

Kwa kifupi ni kuhoji na kutathmini, ni shule ngapi tulizonazo, ni ngapi zimeongezeka, ni wanafunzi wangapi wamehitimu shule, ni hospitali ngapi tulizonazo zina uwezo gani, msisitizo wa kinga ni mkubwa kiasi gani kulingana na tiba, kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji mali na hifadhi za mazao, kubana matumizi na matumizi mazuri ya fedha.

Nimeweka wajibu huu kwako wewe mwananchi kwanza na si ile kasumba ya kusubiri Kiongozi Mkuu-Rais au Waziri Mkuu ndio wawe wenye jukumu na uhalali wa kuhoji haya.
Vipimo hivi haviishii kwa Mbunge, Mkuu wa Wilaya au Mkoa ni mpaka kwenye Serikali kuu na hata vigezo hivi vinaweza tumika katika mashirika na taasisi za umma na zile binafsi.

Kama vigezo hivi vya uongozi bora na kupima uwajibikaji vingekuwa vikifuatwa kwa makini, tungeweza kuona uwiano wa maendeleo wa Taifa letu. Lakini ni mpaka pale tutakaboshinikiza na kudai kwa nguvu Utawala na uongozi bora, ndipo tutakapoona mafanikio na hivyo kuanza kupata tumaini la maendeleo ya Taifa zima.

Uongozi na Utawala bora huendana sambamba na dola. Katika Utawala bora, Serikali na Viongozi ni wabunifu wa mipango mizuri ya maendeleo, ni wapimaji wa kasi ya maendeleo na hufuata kanuni na sheria katika kufanya kazi zao.

Panapokuwa na Uongozi na Utawala mzuri, kero za wananchi hupungua na hata matumizi ya dola na vyombo vyake huheshimika na huwa ni kwa ajili ya manufaa ya Taifa.
Hali halisi ya Tanzania imejenga mfumo wa utawala unaolinda utashi na maslahi ya chama tawala au kikundi chenye nguvu za madaraka nja mali. Hali hii imefikia hatua ya kikundi hiki cha watawala kutumia nguvu za dola kutawala kwa mabavu, kukiuka sheria na kanuni alimradi wanatumia kinga ya uongozi.

Utawala wa namna hii si mzuri na hauna manufaa hata kidogo kwa nchi yetu au Taifa lolote. Tunapaswa kukemea na kuondokana na mfumo huu mbovu wa Utawala ambao unatumia dola na kuweka wajibu wa kwanza wa Uongozi ni kulinda matakwa ya Chama au kikundi maalum.
Aidha matumizi mabovu ya dola na vyombo vyake, Bunge, Mahakama, Polisi, Jeshi na Usalama wa Taifa yamesababisha kwa kiwango kikubwa kuzorota kwa Uongozi, kuweko kwa utawala mbovu ambao umeishia kuangamiza uchumi na juhudi za maendeleo ya Taifa.

Wajibu wa vyombo kama Bunge na Mahakama ni kuwa mihimili mingine ya Serikali. Bunge likitunga Sheria, Mahakama ikitoa tafsiri za sheria na Serikali kuu kufanyia kazi sheria. Badala ya vyombo hivi kuwa huru na hata kuhakiksha vyombo visaidizi kama Polisi, Jeshi, Mahakama, Magereza, Usalama wa Taifa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu vinabakia kuwa vyombu huru ndani ya mfumo wa kisiasa, vyombo hivi vimegeuzwa na kutumika kama silaha ya kulinda chama kinachotawala kwa kutoa vitisho kwa wananchi na vyama visivyo na madaraka.

Suluhisho la haya yote ni kuundwa kwa Katiba mpya na Sheria mpya ambazo zitalenga;
· kutoa haki sawa kwa kila mwananchi bila upendeleo
· kutofungamana na chama au kikundi cha siasa au watawala,
· kuwajibisha Watanzania wote bila kujali nafasi zao katika jamii na Taifa,
· kulinda maslahi, haki , uhuru na mali za Watanzania wote bila kujali itikadi, dini, elimu, jinsia, umri au kabila
· kutoa tafsiri na maelezo ya kisheria na kanuni ambayo hayana utata au kukosa nguvu kufanyiwa kazi na kufuatiliwa
· kumpa kila Mtanzania fursa na haki sawa katika kuchangia kwake ujenzi wa Taifa na hata kuongoza bila kuwa na vipingamizi vya kibaguzi ambavyo vimewekwa maksudi katika katiba ya sasa na Sheria kuzuia ushindani au kuwepo kwa uhuru kamili wa kujieleza na kufanya mambo ya siasa na uongozi
· kujenga miiko mikali na maadili kwa viongozi, utawala na wanachi kwa ujumla
· kuweka mfumo bora wa uteuzi au uchaguzi wa viongozi na wawakilishi

Penye nia pana njia, kama wote tutakaa mstari mmoja na kukubaliana kwa pamoja kuwa haya ndiyo tunayoyataka kutoka kwa viongozi wetu, mfumo wetu wa utawala na dola, nafasi ya kupata viongozi wazuri, kuwa na mipango mizuri itafanikiwa na hivyo kuruhusu wananchi na viongozi kuwajibika kwa dhati na kujituma ili kuhakikisha kuwa shughuli za Ujenzi wa Taifa kiuchumi unafanikiwa kukiwa na Amani, Mshikamano, Sheria na Uongozi Bora.
 
Kanisa Katoliki lagoma

KANISA Katoliki limekataa kuuondoa waraka wake kuhusu elimu ya uchaguzi na limewashangaa wanaouogopa.

Kanisa hilo limesema, limefunga mjadala kuhusu waraka huo, unafaa, na halitamjibu yeyote atakayehoji uhalali wake.

Limesema, waraka huo ni nguvu ya hoja na si ya kiimani, kila mtu anaruhusiwa kuwa nao bila kujali dini, kabila au rangi.

Kwa nyakati tofauti, Kanisa Katoliki limewahi kusema kuwa waraka wa elimu ya uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu mwakani na ule wa mwaka 2015 unafaa na hauna tatizo lolote.

Kwa mujibu wa uongozi wa kanisa hilo, halihitaji mjadala na mtu yeyote kuhusu waraka huo hivyo, watu wenye mapenzi mema wausome na kuuelewa kabla ya kuujadili.

Askosu Mkuu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini amesema, Kanisa hilo limetoa baraka kila mtu mwenye mapenzi mema autumie waraka huo kama jukumu mojawapo la kanisa kuelimisha jamii kimwili na kiroho.

Askofu Kilaini amesema, si mara ya kwanza kwa kanisa hilo kutoa waraka kama huo ila anadhani umewagusa sana watu kwa sababu umegusia suala la ufisadi.

Kanisa hilo limesema, halitamjibu chochote Mbunge wa Kuteuliwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru kwa kuwa linamheshimu.

Kanisa hilo limemshauri Ngombale mwiru aainishe eneo lenye utata katika waraka huo ili kanisa nalo lifahamu kasoro za waraka huo badala ya kutoa hoja juu juu.

“Nina muheshimu sana yule mzee, kachangia sana kujenga taifa hivyo heshima yangu kwake ni kubwa na nisingependa kumjibu ila faida ya wengine ni kwamba nchi hii si ya chama kimoja bali kila mtu ana uhuru wa kusema, na hao wanataaluma wametumia haki hiyo kutoa maoni yao, watu wautafute waraka maana unapatikana na wausome ili wapate mantiki yake kwa kina,” amesema Kilaini.

Kilaini amesema leo kuwa, kama kuna mtu anaona unahatarisha amani abainishe wazi kipengele husika kwa hoja, na kwamba, suala si kuuondoa au kuuacha.

“Tumeshazungumza sana suala hili, kanisa limejaliwa neema za kuwa na taasisi nyingi ndani yake na hii ya Wanataaluma Wakatoliki ni moja wapo, hivyo hao wametoa maoni yao ambayo kanisa imeyapa baraka kutumika kwa kila mtu mwenye mapenzi mema kama jukumu moja wapo la kanisa kuielimisha jamii kimwili na kiroho” ameisema Kilaini.

“Hao wanaoogopa sijui ni kwa nini? kama nilivyosema awali wabainishe kipengele chenye shida na ikumbukwe si mara ya kwanza kutoa waraka kama huu, unatoka mara nyingi, wa kwanza waliutoa mwaka 1989 na wameendelea kutoa nyaraka nyingi, naona kipindi hiki inawagusa watu sana kwa kuwa ufisadi umeguswa humo, waraka huo ni nguvu ya hoja na si nguvu ya kiimani na kila mtu anaruhusiwa kuwa nao bila kujali dini, kabila wala rangi.”

Kilaini amesema, taasisi za dini zipo huru kuchangia mawazo endapo zikiona suala hilo lina maslahi kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Kilaini, kilichofanywa na Kanisa Katoliki si kitu kipya, ni utaratibu wa kawaida.

Naye Katibu wa Habari wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Modesti Katonto amesema,kanisa liimefunga mjadala kuhusu waraka huo.

Amesema, kanisa halimjibu Kingunge au yeyote atakayetaka malumbano kwa kuwa limetimiza wajibu wake.

Padri Katonto amewaeleza waandishi wa habari Dar es Salaam kuwa, kanisa halina nia mbaya na liliubariki baada ya kuusoma kwa kina na kuona unafaa.

Ngombale Mwiru jana aliliomba Kanisa Katoliki liuondoe waraka huo kwa madai kuwa unahatarisha mshikamano wa taifa.

Mbunge huyo alisema bungeni mjini dodoma kuwa, kutolewa kwa waraka huo ni dalili za nchi kuanza kubabaika juu ya mshikamano wa udugu ambao ndiyo utamaduni wa nchi.

“Nasema hivi, kwa heshima zote, nawaomba viongozi wa Kanisa Katoliki warudishe mwongozo wao. sisi tunataka nchi moja, watu wameshikamana, hatutaki kugawanyika kama Lebanon” alisema Mbunge huyo
 
Askofu Kilaini: Kingunge anajadili hewa kuhusu mwongozo

*Asema kanisa litazidi kuusambaza nchi nzima


Na Leon Bahati


KANISA Katoliki Jimbo la Dar es Salaam limesema kauli ya mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru ya kulitaka kanisa kufuta mwongozo wake kwa wananchi juu ya namna ya kuchagua viongozi katika uchaguzi mkuu ujao, ni ya hewani kwa kuwa haijajadili hoja yoyote iliyo kwenye waraka huo.

Isitoshe, limesisitiza kuwa Kanisa Katoliki halitaufuta mwongozo huo na badala yake litaendelea kuuchapisha na kuusambaza kote nchini, ili elimu hiyo ienee kwa watu wengi.

Askofu msaidizi wa Jimbo la Dar es salaam, Methodius Kilaini alisema jana katika mahojiano na gazeti hili kwamba, anamheshimu sana Kingunge Ngombale Mwiru kwa sababu ana mengi mazuri ambayo amelifanyia taifa hili.


Lakini akasema kuwa katika kauli aliyoitoa bungeni juzi kwamba Kanisa Katoliki lifute mwongozo wake, haina nguvu kwa sababu haikosoi kipengele chochote cha taarifa hiyo bali inatoa maelezo ya jumla.

Alisema kanisa lingeweza kumsikiliza na kuipima kauli yake kama angekuwa amechambua vipengele anavyoona havifai na askofu huyo akaongeza kuwa anaamini kuwa haiwezekani kwa Kingunge kuukosoa mwongozo wote.

"Tunatakiwa tufike mahali tujibu jambo hili kwa hoja. Labda wangesema pale waliposoma kwenye mwongozo huu ingepasa kuwa hivi, na akatoa hoja ili tuendane na hoja," alisema Kilaini.

"Kwa jinsi hiyo tungepata hoja ya Wakatoliki, tungepata hoja ya vyama vya siasa... kuna NGO nazo zingetoa hoja, kuna vikundi na madhehebu ya dini nayo yangetoa pia maelezo yao.

"Tusichanganye (mwongozo) wote kwa pamoja bali zitolewe hoja. Pale penye hoja nzuri ndio patashinda. Twende kwa hoja na siyo kusema tuutoe (mwongozo). Hii hapana."

Alishangazwa na kitendo cha Kingunge na hata wanasiasa wengine kuujia juu mwongozo huo wakati kanisa limekuwa na utamaduni wa kutoa taarifa za namna hiyo tangu mwaka 1912, na hakukuwepo mtu aliyejitokeza kupinga.

Alifafanua kuwa taarifa hiyo si waraka wa kichungaji kama inavyoelezwa na watu wengi bali ni mwongozo uliotolewa na Wataalamu wa Taasisi ya Kanisa Katoliki (CPT) na kuridhiwa na kanisa.

Alifafanua kuwa waraka huo hawaulengi waumini wa Kanisa Katoliki peke yake, bali wananchi wote bila kubagua dini.

Pia alisema kuwa mwongozo huo haujakiuka taratibu za nchi kama baadhi ya wanasiasa wanavyouelezea kwamba unachanganya dini na siasa na wala hauwezi kuligawa taifa bali unahimiza mshikamano.

"Umeandikwa kwa ajili ya watu wote wenye mapenzi mema. Na wala hakuna kipengele hata kimoja kinachosema waumini wa Kanisa Katoliki wafanye hivi na hivi," alisema akielezea kuwa unawaelimisha wananchi juu ya sifa za mtu ambaye ni kiongozi bora.

Aliongeza kuwa Kanisa Katoliki halifungamani na chama chochote cha kisiasa na lina imani kuwa mtu yeyote bila kujali dini wala kabila anaweza kuliongoza taifa ili mradi awe ni mwadilifu.

Askofu Kilaini alifafanua kuwa maaskofu, mapadri na watawa wa kanisa hilo si wanachama wa chama chochote cha siasa.

Tofauti na miaka mingine, Kilaini alisema kuwa mwongozo wa wakati huu umeonekana kuwachanganya wanasiasa wengi kwa sababu umegusia suala la ufisadi.

Kilaini alisema kuwa waraka huo hauwezi kufutwa labda kama kuna kipengele ambacho kitaonekana kuwa kina kasoro na kanisa kukiridhia, ndicho kinaweza kubadilika.

Alifafanua kuwa mwongozo huo ambao upo kwenye kitabu chenye kurasa 95, umekuwa ukinunuliwa kwa wingi sehemu mbalimbali nchini.

Kutokana na hali hiyo, Kilaini alisema wanaendelea kuchapisha kwa wingi na kuusambaza kote nchini ili kutekeleza kiu ya watu wengi ambao wanauhitaji.

Aliweka wazi kuwa kasi ya manunuzi imeongezeka baada ya baadhi ya wanasiasa kuushutumu.

Exuper Kachenje na Anna Lusana wanaripoti kuwa jopo la masheikh na wanazuoni, wamekemea vikali kile walichokiita tabia ya baadhi ya madhehebu ya dini kuchanganya dini na siasa.

Akijibu swali kutoka kwa waandishi wa habari waliotaka kujua iwapo watatoa waraka kuelekeza kiongozi anayefaa kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu kama lilivyofanya Kanisa Katoliki, katibu wa jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu, Sheikh Khamis Mattaka alisema jopo hilo linakemea vikali tabia ya baadhi ya madhehebu hayo na viongozi wake kuchanganya dini na siasa.

Alisema kimsingi jopo hilo linaelekeza kiongozi kuchaguliwa kutokana na Utanzania wake na siyo kigezo cha dini yake.

"Sisi tulishakemea tabia ya kuchanganya dini na siasa katika kikao chetu cha kwanza mwezi uliopita, leo tunakemea tena kuchanganya dini na siasa," alisema Mattaka na kuongeza;
"Tunataka watu wachaguliwe kwa Utanzania wao na sifa walizo nazo na si kigezo cha dini."

Aliongeza kuwa iwapo mtu yeyote anataka kugombea uongozi, basi auze sera za chama chake kwa wananchi badala ya kutumia mwavuli wa dini.

Wakati huo huo Daniel Mjema anaripoti kuwa mkongwe nchini, Peter Kisumo amemjibu mwanasiasa mwingine mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru kuhusu waraka wa Kanisa Katoliki, akisisitiza kanisa hilo halipaswi kukemewa kama vile limefanya makosa.

Akizungumza na Mwananchi jana, Kisumo alipinga kauli ya Kingunge kuwa waraka huo unaweza kuigawa nchi kama Lebanon, akisema hilo haliwezi kutokea kwani Lebanon ina vyama vya kidini wakati Tanzania ina vyama vya siasa.

Kisumo aliyewahi kushika nyadhifa kadhaa za juu katika serikali ya awamu ya tatu, alisema kilichopaswa kufanyika ni kwa vyama vya kiraia kuchukua jukumu la kutoa elimu ya kiraia badala ya kuliachia kanisa moja moja kufanya hivyo.

"Ninaamini Kanisa Katoliki limesukumwa kutoa mwongozo huo wakati huu tukielekea katika uchaguzi kwa sababu vyama vya kiraia vimekaa kimya… lakini tusiliachie kanisa peke yake kufanya kazi hii," alisisitiza Kisumo.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo alikiri kuwa kama vyama vya siasa na serikali vitaachia makanisa pekee kutoa elimu hiyo ipo hatari kubwa ya kusababisha mfarakano, lakini si kwa kiwango kama cha nchi ya Lebanon.

"Kazi hii ya kutoa elimu ikiachwa ifanywe na kanisa pekee inaweza kusababisha mfarakano, lakini hatuwezi kulikemea Kanisa Katoliki kuwa limefanya makosa kwa sababu serikali na vyama vyetu vimekaa kimya, nani aelimishe umma," alihoji.

Kisumo alisema mazingira ya Tanzania ya sasa yanadhihirisha kuwepo kwa mbegu mbaya iliyoanza kupandwa na ambayo inaweza kuvuruga umoja wa kitaifa kama hoja za kisiasa zitaachwa zishughulikiwe na vyombo vya dini.

"Iko mbegu imeshaanza kupandwa ambayo inaweza kuvuruga umoja wetu na mbegu hiyo itaweza kustawi tu kama hoja za kisiasa hazitashughulikiwa na vyombo vya kisiasa na ikaachwa ishughulikiwe na vyombo vya dini," alisema.

Kisumo alisema idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza katika chaguzi ndogo za Tarime, Mbeya na Biharamulo ni kielelezo tosha cha kuonyesha mwamko wa wananchi umeshuka na akashangaa vyama vya siasa kutoliona hilo.

Alivitaka vyama vya siasa vikiwamo CCM, Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kuichukua agenda ya kutoa elimu ya uraia kama hiyo kwani ndivyo vyombo vya kiraia.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni juzi, Kingunge aliushambulia waraka huo unaoelezea namna ya kupata kiongozi anayefaa katika uchaguzi ujao.
 
Mzee Kingunge yuko kisiasa zaidi, (kiCCM). Hawa wakatoliki wameangalia zaidi maslahi ya kitaifa na ustawi kijamii ya watanzania kwa ujumla wetu.

Ni lazima ifahamike kuwa taasisi za dini hazianza leo kuhamasisha maendeleo ya wananchi. Taasis za dini zimeshiriki kuleta maendeleo ya KIELIMU, AFYA, UCHUMI nk. kwa watanzania kwa muda mrefu na ni kwa malengo hayo hayo ya kuwasisia watanzania kwamba wanaamini, na ndivyo ilivyo kuwa haya yote yatafanikiwa chini ya uongozi imara na makini.

Uongozi huu imara sio lazima utoke CCM unaweza kutoka kwa mtanzania yeyote.

Isitoshe wakatoliki hawa hawahamasishi watu kukikataa CCM bali kukataa viongo wabaya na kuchagua viongozi makini, wamewametoka humo humo CCM au chama kingine. Kwa nini CHADEMA hawajalalamika kwani wao hawana wagombea? halikadhalika vyama vingine kama CUF nk.

Ushauri wangu kwa mzee Kingunge ni lazima asome alama za nyakati. Njia pekee ya kikinusuru chama chake ni kuhakikisha wanawaletea watanzania maendeleo waliyoahidi wakati wa chaguzi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom