Zanika
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 1,316
- 752
ADUI UNAYELALA NAYE NA KUAMKA NAYE NDIYE MBAYA KULUKO YULE ANAYEKUJA NA KUONDOKA! HUU NDUI UKWELI
NI muda mrefu nchi yetu ya Tanzania imekuwa ikihujumiwa na Wasomi hasa baadhi ya Wanasheria wasio waaminifu wenye kujaa tamaa ya fedha zisizo halali. Wakishirikiana na Wanasiasa wenye tamaa ya mali walioko Bungeni (wapiga deal) pamoja na baadhi ya Watumishi wa umma na baadhi ya vyombo vya habari.
Haya yanafanywa na Wana siasa hoa ambao wako Bungeni na wenye Makampuni ya Uwakili wakishirikiana na Baadhi ya Wanasheria wa Serikalini. Ambapo huhakikisha mikataba inayowekwa itafika mahali Serikali haitaridhishwa na utekelezwaji wa mradi husika. Hatimaye kinachofata watapenyeza wataalam ili waishauri Serikali isimamishe mradi au kuifukuza kampuni husika.
Wakishindwa hapo watatumia baadhi ya Wabunge wapiga deal ili hoja ipelekwe bungeni kama bomu fulani na kuwashawishi bunge liibane serikali ichukue hatua na kuwawajibisha viongozi na kusitisha mkataba.
Sambamba na hilo watatumia mikutana mbali mbali kwenye platforms za vyama vyao vya Siasa,Press za Bunge na Vyombo vya habari kufanya kampeni ya ki-propaganda ili kufanya umma ujikite kwenye mjadala husika na kuufanya wa kitaifa ili kuishinikiza Serikali iingie mtegoni na hata baadaye itakapodaiwa ionekane ni uzembe wa Serilali.
Kinachofata ni Kampuni husika inaibukia mahali kwingine na kufungua madai kwa kutumia mkataba ambao unaifunga Serikali na kupelekea kuwalipa kwa kazi mbovu au Manunuzi mabovu waliyotufanyia.
Na hii ndio siri kubwa ya baadhi ya wanasiasa kutumia fedha nyingi sana na ushirikina kuhakikisha wanaingia Bungeni. Amini usiamini nyuma ya pazia Bungeni kuna blackmail deals nyingi zinafanywa na Wabunge wasio na mapenzi mema na nchi hii. Kadhalika na hilo wako ziko kampuni za Uwakili zinazotumika kuhujumu uchumi na kupindisha na kupotosha ukweli wowote juu ya dhuluma tunayofanyiwa kama Taifa.
Wakati umefika sasa Serikali na Taifa kuwafanyia Examining hawa na ikibidi kuyafutia leseni makampuni haya ya Uwakini na kufuta vibali vya Wanasheria wa aina hii. Halikadhalika kuwatangaza Wabunge na wanasiasa wote wa aina hii ili tuwawajibishe inavyostahili.