Wapo wa kuijadili nchi yetu, ila wa kuichukulia hatua zozote zile, hawajazaliwa bado

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,504
3,499
Kama kichwa cha habari kilivyo!

Tanzania ni nchi yenye historia ya pekee barani Afrika na duniani kote.

Ni taifa lililopigania Uhuru wa nchi nyingi Afrika na ni Taifa la kuigwa si barani Afrika pekee bali duniani kote

Ni taifa lililojipatia Uhuru wake pasi na kumwaga damu, na hii si kwa sababu mbinu nyingine zilishindwa, la hasha.

Zipo sababu nyingi za kufanya Taifa letu kuwa ni taifa la pekee sana katika Dunia hii tuliyonayo. Wengi wa watu hulitazama Taifa letu katika nyanja ya kiuwezo pekee wa vitu, lakini wanashindwa kuona muunganiko wa Tanzania na mataifa mengine duniani jinsi Taifa letu lilivyo kiungo mhimu katika Dunia.

Na kama hayo mtu huyajui, ni bora kukaa kimya, waacheni wakosa kazi wajaribu wawezavyo kama watapata matokeo.

Tunayo mataifa ya kuijadili nchi yetu, ila hayapo mataifa ya kuichukulia hatua nchi yetu

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
08:26
Monday, 23 November 2020 (GMT+1)
Time in The Hague, Netherlands
Acha kutetema mahakama inafunguliwa sasa hivi watu wazame ndani na makabrasha pages 100,000
 
Kama kichwa cha habari kilivyo!

Tanzania ni nchi yenye historia ya pekee barani Afrika na duniani kote.

Ni taifa lililopigania Uhuru wa nchi nyingi Afrika na ni Taifa la kuigwa si barani Afrika pekee bali duniani kote

Ni taifa lililojipatia Uhuru wake pasi na kumwaga damu, na hii si kwa sababu mbinu nyingine zilishindwa, la hasha.

Zipo sababu nyingi za kufanya Taifa letu kuwa ni taifa la pekee sana katika Dunia hii tuliyonayo. Wengi wa watu hulitazama Taifa letu katika nyanja ya kiuwezo pekee wa vitu, lakini wanashindwa kuona muunganiko wa Tanzania na mataifa mengine duniani jinsi Taifa letu lilivyo kiungo mhimu katika Dunia.

Na kama hayo mtu huyajui, ni bora kukaa kimya, waacheni wakosa kazi wajaribu wawezavyo kama watapata matokeo.

Tunayo mataifa ya kuijadili nchi yetu, ila hayapo mataifa ya kuichukulia hatua nchi yetu!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
Hata wewe pia nawe bado hujazaliwa, au jukumu ulilolitaja hapa wewe halikuhusu, linawahusu wengine watakaozaliwa baadaye?
 
Yule mzungu wa EU hajui lolote kuhusu Tanzania, ana akili zile zile za kwamba nchi ya afrika haipaswi kuwa na mawazo ya kutafuta maendeleo.

Hilo suala la covid19 ni gia tu ya kutafuta kuona tunakuwa na vurugu, jambo ambalo aliondoe kabisa kichwani kwake na vichwani mwa watu kama yeye.
 
Back
Top Bottom