Wapo tayari kufa kuliko kuachia utawala

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Utawala uliodumu kwa miaka zaidi ya 50 lazima unalundo la uchafu ambao umetupiwa uvunguni. Uchafu huu hakuna kiongozi aliyeko madarakani anataka kuutoa,kuugusa, wala kuusikia ukisemwa.

Uchafu wenyewe umelundikwa na wengi, kwa wakati tofauti. Ukitaka kusafisaha nyumba hii lazima uue wengi kwani wengine tayari uchafu huu umekuwa ni mazingira ya kawaida ukibadilisha lazima wauugue.

Kwa nchi yetu ambayo imetawaliwa kwa utawala wa chama kimoja, ambacho kimejipa hadhi na utukufu mkubwa. Chama ambacho maofisa wake hawaguswi kwa kosa lolote tangia uhuru wa Tanganyika na Muungano wa JMT, chama ambacho cheo ni cha familia na marafiki, hawapo tayari kuachia madaraka haya kwa gharama rahisi, wanajua wasipokuwepo ikulu wao na watoto, marafiki watazijaza keko.

Ukiangalia picha ya Yona, Mramba, Balali, MD wa Tanesko na mkewe ni kielelezo tosha kwamba utawala wa sheria na katiba utawapeleka wengi kisutu.

Watawala wa afrika kwa wizi, ufisadi, uhujumu, uuwaji wa wasio na hatia na kila aina ya unyama wanapokuwepo madarakani ndio chanzo cha wao kung'ang'ania ikulu na vyama vyao kwa gharama kubwa.

Dhambi ya mauti inayorithishwa watoto wa watawala ndio inayoingamiza afrika na Tanzania. Wanatumia kodi zetu kujilundikia silaha ili kujilinda na tawala zao dhalimu.

Ni Afrika imebaki viongozi wako tayari kufia madarakani kwa aibu kuliko kuachia madaraka.
Tukiweza kuzalisha viongozi wanaopenda legacy, utu, kuthaminiwa na wenye maono ya kweli huu umangimeza utaisha.
 
strong ruler

JF-Expert Member
Nov 2, 2013
4,787
2,000
ImageUploadedByJamiiForums1401214741.579316.jpg
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Tanzania kuna hicho kinachoitwa demokrasia ya vyama vingi, wasiotaka chama kinachoongoza sasa wasiondoke madarakani ni wananchi ambao hawajaona mbadala ulio na maana.

Mbona toka tulivyoingia kwenye hiyo inayoitwa demokrasia ya vyama vingi tunaona wabunge wa upinzani wakiongezeka bungeni kila uchaguzi? au hilo hulioni?

Hivi unataka tumchaguwe Rais awe Slaa? duh! bora hata likiwekwa jiwe ligombee ntalichagua kuliko mtu kama huyo.

Upinzani uliopo sasa kwa jinsi ulivyo mbovu, hata miaka 200 ijayo CCM itaendelea kutawala.

Hivi chama kinaongozwa na DJ failure wa shule na kinafukuza wasomi unategemea kuna siku kitashika madaraka? nakwambia mawee!
 
Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
3,261
2,000
Kuliko "KUIONA NCHI YANGU IKIANGUKIA MIKONONI MWA MIJIBWA MIHAINI", NIPO TAYARI KUZIKWA NA HAO WATAKAOFIA MADARAKANI!

WATU WAKO TAYARI KUTUUZA KWA MAADUI ILI MRADI TU WASIKIE HARUFU YA IKULU!?

YOU PEOPLE DO REALLY 'STINK!'
 
Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,101
1,195
Sanduku la kura ndio kila kitu, Vyama vingi vimeananzishwa Tanzania toka mwaka 1992,
Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ukafanyika 1995,2000,2005 na 2010. Vyama vya
upinzani vinashiriki. Ila hawashindi na hawapati wabunge wengi nini tatizo???

Nawashauri vyama vya upinzani wapime mambo yafuatayo:-
1. Aina ya chama walichomo kikoje, kinakubalika na wananchi?? (Kuna vyama vyama vya kidini
na kikabila, hakiwezi kushinda wala kupendwa)
2. Aina ya viongozi wanaoongoza chama husika, wana sifa zinazohitajika?? (Elimu yao, Tabia zao,
na mwenendo wao kwenye jamii ukoje)
3. Wananchi wanakikubali hicho chama katika maeneo yote ya Tanzania?? (Kuna vyama vingine kiko
eneo fulani tu ya Tanzania sehemu nyingine hakikubaliki. Kitashinda vip??)
4.Viongozi kwenye chama husika wanapatikana vipi ili kuongoza chama?? ( Je viongozi wa chama husika
wanachaguliwa kihalali kuongoza chama husika?? au wanapeana madaraka.)

Hayo ni machache ninayo yaona mimi, kama huwezi kuyashinda hayo hapo juu huwezi kushinda uchaguzi
katika nchi yeyote ile.

Mandla.
3
 
Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,336
1,500
Tanzania kuna hicho kinachoitwa demokrasia ya vyama vingi, wasiotaka chama kinachoongoza sasa wasiondoke madarakani ni wananchi ambao hawajaona mbadala ulio na maana.

Mbona toka tulivyoingia kwenye hiyo inayoitwa demokrasia ya vyama vingi tunaona wabunge wa upinzani wakiongezeka bungeni kila uchaguzi? au hilo hulioni?

Hivi unataka tumchaguwe Rais awe Slaa? duh! bora hata likiwekwa jiwe ligombee ntalichagua kuliko mtu kama huyo.

Upinzani uliopo sasa kwa jinsi ulivyo mbovu, hata miaka 200 ijayo CCM itaendelea kutawala.

Hivi chama kinaongozwa na DJ failure wa shule na kinafukuza wasomi unategemea kuna siku kitashika madaraka? nakwambia mawee!

Asante,

Nilitaka tujikite kwenye mada, chokozi yangu ni je madaraka yanalevya? Je kunafaida ya ushindani na uwajibikaji? Kama upo tunaupate?

Je unaamini kwa chama kimoja kuishi madarakani bila ushindani wa kweli kuna uwezekanO wa maendelEo ?
Je unaamini kuna mambo yanafanyika ila kwasababu ya kujuana, kutoka mbali, ni sisi sisi yanafichwa tu chini ya uvungu?

Je rasilimali za nchi zinavyokusanywa, tumiwa, tafutwa, na maisha ya Mtanzania zinaendana?

Je udumavu na kurizika madaraka kunaleta uvivu, ukomo wa kufikri na ukosefu wa maarifa mapya?

Chama cha siasa ni kundi la watu, mabadiliko ni hitaji la Wananchi. Je wewe binafsi unapenda kuona mabadiliko yakitokea ya kiuongozi( Assume unaowependa ndio wagombea na sio wa chama chako)
 
Maswali mengi sana kwa wakati mmoja, raha ya mnakasha unakuja na swali moja tunaendelea mpaka linapofikia tunaanza lingine, sasa hapo tutachanganyana tu.

Uliza moja tuendelee.
 
ihs

Member
Jul 24, 2012
93
0
Tanzania kuna hicho kinachoitwa demokrasia ya vyama vingi, wasiotaka chama kinachoongoza sasa wasiondoke madarakani ni wananchi ambao hawajaona mbadala ulio na maana.

Mbona toka tulivyoingia kwenye hiyo inayoitwa demokrasia ya vyama vingi tunaona wabunge wa upinzani wakiongezeka bungeni kila uchaguzi? au hilo hulioni?

Hivi unataka tumchaguwe Rais awe Slaa? duh! bora hata likiwekwa jiwe ligombee ntalichagua kuliko mtu kama huyo.

Upinzani uliopo sasa kwa jinsi ulivyo mbovu, hata miaka 200 ijayo CCM itaendelea kutawala.

Hivi chama kinaongozwa na DJ failure wa shule na kinafukuza wasomi unategemea kuna siku kitashika madaraka? nakwambia mawee!

Haa haaaaaa haaa, wewe kweli ni mwana ccm halisi!! Milele ni ya mungu pekee lakini kwana ccm milele ni ya ccm na viongozi wao. Slaa ana matatizo mangapi kumlinganisha na mwenyekiti wenu wa ccm taifa? Onyesha 5 tu comparatively!! Wasomi waliofukuzwa upinzania ni wepi? wataje 3, je unajua maana halisi ya usomi?? usije ukasema Dr. Mwakeyembe mwenye PHD ni msomi, nitakukatalia mbele ya kadamnasi!!

Arnold Shwaznigger, Ronald Reegan wote hawa walikuwa ma DJ, na mpaka leo tunaenda kwao kuomba vyandarau kwa ajili ya kujifunikia mbu wakati wao wakija kwentu kubeba dhahabu!! Bora kuwa na ma DJ kama hawa kuliko kuwa na majini kama wana ccm!!
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Asante,

Nilitaka tujikite kwenye mada, chokozi yangu ni je madaraka yanalevya?

Madaraka yanalevya sana tu, kuna mwana falsafa maarufu, George Orwell aliwahi kusema:

"Always there will be the intoxication of power, constantly increasing and constantly growing subtler. Always, at every moment, there will be the thrill of victory, the sensation of trampling on an enemy who is helpless. If you want a picture of the future, imagine a boot stamping on a human face - for ever."

Mfano hai kwa ulevi wa madaraka hapa kwetu ni hivi karibuni tu, tumeona chadema wakiwafukuza viongozi wao maarufu kwa kuwa walikuwa na nia ya kugombea ngazi za juu za chama na tukaona hapa hapa JF siri za chama chao zikitolewa kuwa zimefanyika hila kipengele cha uongozi wa juu kwenye katiba yao kimebadilishwa kinyemela na Mwenyekiti wa chadema anaweza kugombea maisha.

Huo ni mfano mzuri sana wa ulevi wa madaraka ambao hata sakata lake bado halijesha na wengine wameenda mahakamani kudai haki zao.
 
NAHINGA

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
1,019
1,500
Sanduku la kura ndio kila kitu, Vyama vingi vimeananzishwa Tanzania toka mwaka 1992,
Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi ukafanyika 1995,2000,2005 na 2010. Vyama vya
upinzani vinashiriki. Ila hawashindi na hawapati wabunge wengi nini tatizo???

Nawashauri vyama vya upinzani wapime mambo yafuatayo:-
1. Aina ya chama walichomo kikoje, kinakubalika na wananchi?? (Kuna vyama vyama vya kidini
na kikabila, hakiwezi kushinda wala kupendwa)
2. Aina ya viongozi wanaoongoza chama husika, wana sifa zinazohitajika?? (Elimu yao, Tabia zao,
na mwenendo wao kwenye jamii ukoje)
3. Wananchi wanakikubali hicho chama katika maeneo yote ya Tanzania?? (Kuna vyama vingine kiko
eneo fulani tu ya Tanzania sehemu nyingine hakikubaliki. Kitashinda vip??)
4.Viongozi kwenye chama husika wanapatikana vipi ili kuongoza chama?? ( Je viongozi wa chama husika
wanachaguliwa kihalali kuongoza chama husika?? au wanapeana madaraka.)

Hayo ni machache ninayo yaona mimi, kama huwezi kuyashinda hayo hapo juu huwezi kushinda uchaguzi
katika nchi yeyote ile.

Mandla.
3

umeshaema uonanyo ww inakuaje unamalizia kwa kusema huwezi shinda uchaguzi kwa kushindwa kufata mtazamo wako? kwani neno lako ni sheria? ndio ulevi wa madaraka unaozungumzwa huu. siku zinaesabika.....
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Haa haaaaaa haaa, wewe kweli ni mwana ccm halisi!! Milele ni ya mungu pekee lakini kwana ccm milele ni ya ccm na viongozi wao. Slaa ana matatizo mangapi kumlinganisha na mwenyekiti wenu wa ccm taifa?

Maswali yako mengi sana ntaanza kukujibu moja moja:

Kwanza, Slaa ni mtu mwenye tamaa, aliyeshindwa kuchunga hata kondoo waliopotea (padri) akaamuwa kupotea yeye mwenyewe kwa matamanio yake.

Kwa hayo hayo matamanio yake akaihama CCM kwa kuwa tu hakupitishwa kugombania ubunge kwenye kura za maoni, inaonesha kuwa alikuwa na tamaa zaidi ya kutumikia wananchi.

Katelekeza watoto zake kwa mwanamke aliyezaa nae na ana kesi mahakamani.

Kapora mke wa mtu kinyume kabisa na mafundisho ya dini yake ya Roman Catholic.

Hawara yake kamfanya ndio mdhibiti wa programu za mapato na matumizi za chadema kwa tamaa yake. Baada ya kupewa kazi hiyo, mchumba akafunguwa NGO yake, ambayo kwa sasa ni NGO yenye pesa kuliko chadema.

Ni mtu ambae kakigeuza chama cha siasa kuwa saccos kwa kujikopesha mamilioni ya fedha kwa tamaa zake.

Ni mtu ambae siasa zake zimekuwa ni za majungu na kusema uongo, mifan ni mingi ukiihitaji ntakuwekea.

Hayo baadhi tu ya matatizo, tena omba Mungu akina MSALANI, Ritz na wengineo wasipite hapa wakaendeleza kumwaga dhambi zake, utatafuta pa kukimbilia.
 
SOCIOLOGISTTZ

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
2,606
1,225
Maswali yako mengi sana ntaanza kukujibu moja moja:

Kwanza ni mtu mwente tamaa, aliyeshindwa kuchunga hata kondoo waliopotea (padri) akaamuwa kupotea yeye mwenyewe kwa matamanio yake.

Kwa hayo hayo matamanio yake akaihama CCM kwa kuwa tu hakupitishwa kugombania ubunge kwenye kura za maoni, inaonesha kuwa alikuwa na tamaa zaidi ya kutumikia wananchi.

Katelekeza watoto zake kwa mwanamke aliyezaa nae na anakesi mahakamani.

Kapora mke wa mtu kinyume kabisa na mafundisho ya dini yake ya Roman Catholic.

Hawara yake kamfanya ndio mzibiti wa programu za mapato na matumizi za chadema kwa tamaa yake. Baada ya kupewa kazi hiyo, mchumba akafunguwa NGO yake, ambayo kwa sasa ni NGO yenye pesa kuliko chadema.

JK hana dhambi? je unaongeleaje ufisadi uliopo kwenye serikali ya ccm? wewe jinsi ulivyo unafurahia mabilioni ya watanzania yakiporwa kila kukicha lakini unachukia sana mtu aliyeachana na mkewe, na huyo mke akapata mume mwingine. Kama ndivyo hivyo uzalenda wako uko wapi?

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
10,685

hayajazidi ya JMK,tena yake yanaleta negative impact kubwa ktk maisha yco na ya wengi ( 99% ) kuliko ya slaa (0.01)
 
Last edited by a moderator:

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
10,685
2,000
Maswali yako mengi sana ntaanza kukujibu moja moja:

Kwanza ni mtu mwente tamaa, aliyeshindwa kuchunga hata kondoo waliopotea (padri) akaamuwa kupotea yeye mwenyewe kwa matamanio yake.

Kwa hayo hayo matamanio yake akaihama CCM kwa kuwa tu hakupitishwa kugombania ubunge kwenye kura za maoni, inaonesha kuwa alikuwa na tamaa zaidi ya kutumikia wananchi.

Katelekeza watoto zake kwa mwanamke aliyezaa nae na anakesi mahakamani.

Kapora mke wa mtu kinyume kabisa na mafundisho ya dini yake ya Roman Catholic.

Hawara yake kamfanya ndio mzibiti wa programu za mapato na matumizi za chadema kwa tamaa yake. Baada ya kupewa kazi hiyo, mchumba akafunguwa NGO yake, ambayo kwa sasa ni NGO yenye pesa kuliko chadema.

Ni mtu ambae kakigeuza chama cha siasa kuwa saccos kwa kujikopesha mamilioni ya fedha kwa tamaa zake.

Ni mtu ambae siasa zake zimekuwa ni za majungu na kusema uongo, mifan ni mingi ukiihitaji ntakuwekea.

Hayo baadhi tu ya matatizo, tena omba Mungu akina MSALANI, Ritz na wengineo wasipite hapa wakaendeleza kumwaga dhambi zake, utatafuta pa kukimbilia.

hayajazidi ya JMK,tena yake yanaleta negative impact kubwa ktk maisha yco na ya wengi ( 99% ) kuliko ya slaa (0.01%:)
 
Last edited by a moderator:

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
JK hana dhambi? je unaongeleaje ufisadi uliopo kwenye serikali ya ccm? wewe jinsi ulivyo unafurahia mabilioni ya watanzania yakiporwa kila kukicha lakini unachukia sana mtu aliyeachana na mkewe, na huyo mke akapata mume mwingine. Kama ndivyo hivyo uzalenda wako uko wapi?

Juliasi Kambarage alikuwa na dhambi zake nyingi tu, muulize Tundu Lissu atakueleza.

Ufisadi uliopo serikalini ni wa miaka mingi sana, toka enzi za Juliasi, ndio kwanza wakati wa Jakaya Mrisho Kikwete tumeona kero za ufisadi serikalini zikishughulikiwa kwa dhati na mambo yanaenda vizuri mpaka sana mpaka sasa, tumeona mabadiliko makubwa kwenye huduma za serikalini, huwezi kulinganisha na majanga ya ufisadi aliyoyarithi Jakaya.

Hayo niliyoyafurahia ni yepi? wacha kuhororoja njoo na hoja.
 
kenwood

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
757
195
Mara Julius Mara Chadema kumgaragaza Zitto ila JK aaaah!! Msiniumizieee!!!

Hamna serikali mbovu iliyowahi kutokea kama ya Jakaya M. Kikwete
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom