Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,464
Utawala uliodumu kwa miaka zaidi ya 50 lazima unalundo la uchafu ambao umetupiwa uvunguni. Uchafu huu hakuna kiongozi aliyeko madarakani anataka kuutoa,kuugusa, wala kuusikia ukisemwa.
Uchafu wenyewe umelundikwa na wengi, kwa wakati tofauti. Ukitaka kusafisaha nyumba hii lazima uue wengi kwani wengine tayari uchafu huu umekuwa ni mazingira ya kawaida ukibadilisha lazima wauugue.
Kwa nchi yetu ambayo imetawaliwa kwa utawala wa chama kimoja, ambacho kimejipa hadhi na utukufu mkubwa. Chama ambacho maofisa wake hawaguswi kwa kosa lolote tangia uhuru wa Tanganyika na Muungano wa JMT, chama ambacho cheo ni cha familia na marafiki, hawapo tayari kuachia madaraka haya kwa gharama rahisi, wanajua wasipokuwepo ikulu wao na watoto, marafiki watazijaza keko.
Ukiangalia picha ya Yona, Mramba, Balali, MD wa Tanesko na mkewe ni kielelezo tosha kwamba utawala wa sheria na katiba utawapeleka wengi kisutu.
Watawala wa afrika kwa wizi, ufisadi, uhujumu, uuwaji wa wasio na hatia na kila aina ya unyama wanapokuwepo madarakani ndio chanzo cha wao kung'ang'ania ikulu na vyama vyao kwa gharama kubwa.
Dhambi ya mauti inayorithishwa watoto wa watawala ndio inayoingamiza afrika na Tanzania. Wanatumia kodi zetu kujilundikia silaha ili kujilinda na tawala zao dhalimu.
Ni Afrika imebaki viongozi wako tayari kufia madarakani kwa aibu kuliko kuachia madaraka.
Tukiweza kuzalisha viongozi wanaopenda legacy, utu, kuthaminiwa na wenye maono ya kweli huu umangimeza utaisha.