Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,435
- 1,995
Asubuhi hii (29 May, 2018) WAPO Radio wamesoma taarifa za magazetini kwamba "Benki sasa kushindana kushusha riba" kama vile ni neema kwa umma! Jambo ambalo si kweli, kwasababu kiini cha habari ni kwamba: "ukikopa Tsh.100,000,000/- unapewa muda (usiozidi) miaka saba kurudisha".
Hakuna unafuu wowote hapo:
100,000,000÷7=14.285 million
14.285÷12=1.2 million
Hii ina maana kwamba ukikopa kiasi hicho utatakiwa kurudisha 14.285 m. kwa mwaka! Na ili umudu masharti ya mkopo huu lazima ufanye biashara itakayokupa faida na ziada sh. 1.2 million kwa mwezi! Kwasababu ukilipa faida yote kwenye deni utakula nini? Halafu hujalipa kodi hapo! Sasa hii itakuwa biashara gani? Ndio mana nasema watangazaji wamesoma hii habari kiukasuku.