Wapinzani waumia Serikali kupokea wakimbizi

Wapinzani waumia Serikali kupokea wakimbizi

rajabs

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
384
Reaction score
73
Baada ya serikali ya Tanzania inayosifika duniani kuwa kisiwa cha amani kupokea wakimbizi kutoka Burundi na kupongezwa na mataifa makubwa duniani, kumbe ndani ya nchi hii kuna watu wenye mlengo tofauti na serikali wamepinga suala hilo japo hawana ujasiri wa kuinua sauti zao hadharani juu ya suala hilo.

Baadhi ya watu hao wameanza kuzusha kuwa wakimbizi wapatao 20,000, wameingizwa Tanzania kuja kupiga kura ili CCM ipate ushindi. Suala hili linaonyesha kuwa watu hao ambao walikuwa wanafurahia mgomo wa madereva na kuombea mvua izidi kunyesha ili serikali ipate msukosuko katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Jambo hili limewauma watu hao kwani serikali imepiga goli la kisigino.

Ushauri ni mdogo tu hapo. Jamani tusubiri wakati wa kampeni ndio mzungumze mambo yenu. Kwa sasa tushirikiane kujenga Taifa letu Tanzania na serikali yetu ikifanya jambo zuri kama hilo tuisifu. Pia tunazidi kuaminiwa na mataifa makubwa. Au mnataka tuwakatae ili mseme serikali ya Tanzania imewatimua wakimbizi ili mataifa makubwa yatuchukie?
 
Safari hii ule wizi wa kura mliouzoea INTRAHAMWE mmeumia,maana kuna vijiji ambavyo watu wake wameapa kutoipa ccm kura.Maalim Seif kishaanza ulinzi zanzibar,hata BMK mliwapigisha kura marehemu
 
Chama kikiongozwa na watu wa aina ya DJ Zero lazima watakuwa na mawazo ya kipuuzi kama hayo.
 
Mleta mada naona umeishi miaka mingi katika propaganda dhidi ya watanzania waliokosa elimu ya uraia sasa naona umekuja na hoja ya kujishuku. Muda si mrefu mwenzako ataanzisha mada nyingine kwa kichwa tofauti lakini maudhui ni hayo hayo akisema " ni upi msimamo wa cdm kuhusu wakimbizi wa Burundi"
 
Suala la Burundi
lipo Wazi Kama Wewe Ni Mtanzania Huwezi Kufurahia Jirani Yako yaani Warundi Wamerudishwa Kwao 2014

Halafu Kambi zikafungwa leo hii yaani 2015
tayari wamerudi, huoni huo ni mchezo mchafu unaofanywa na Viongozi wa Kirundi tena mchana kweupe.

Ukweli hakuna Anayependa Wakimbizi
hata huko Lampaduso siyo hivyo.
Nkurunzinza ni tatizo kwa yote
 
Safari hii ule wizi wa kura mliouzoea INTRAHAMWE mmeumia,maana kuna vijiji ambavyo watu wake wameapa kutoipa ccm kura.Maalim Seif kishaanza ulinzi zanzibar,hata BMK mliwapigisha kura marehemu
Nchi hii ni kubwa sana na CCM inapendwa kwenye vijiji vingi. Kijiji kimoja tu kikijitoa haitunyimi usingizi
 
Taarabu unaiweza.....vipi nikudhamini ukarekodi?
 
Chama kikiongozwa na watu wa aina ya DJ Zero lazima watakuwa na mawazo ya kipuuzi kama hayo.

Hapo umeonyesha ccm hawakukosea kwa kuamua kuleta watu wa kujibu mapigo mitandaoni. Tunaona jinsi ccm ilivyoimarika na itaendelea kukaa madarakani milele hasa kwa ujengaji hoja wa aina hii. Big up chama cha mapinduzi kwa kuleta watu wa kujenga hoja makini mitandaoni na sasa watanzania wanajivunia kwa kuongozwa na chama chenye wajenga hoja wa namna hii.
 
Baada ya serikali ya Tanzania inayosifika duniani kuwa kisiwa cha amani kupokea wakimbizi kutoka Burundi na kupongezwa na mataifa makubwa duniani, kumbe ndani ya nchi hii kuna watu wenye mlengo tofauti na serikali wamepinga suala hilo japo hawana ujasiri wa kuinua sauti zao hadharani juu ya suala hilo.

Baadhi ya watu hao wameanza kuzusha kuwa wakimbizi wapatao 20,000, wameingizwa Tanzania kuja kupiga kura ili CCM ipate ushindi. Suala hili linaonyesha kuwa watu hao ambao walikuwa wanafurahia mgomo wa madereva na kuombea mvua izidi kunyesha ili serikali ipate msukosuko katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Jambo hili limewauma watu hao kwani serikali imepiga goli la kisigino.

Ushauri ni mdogo tu hapo. Jamani tusubiri wakati wa kampeni ndio mzungumze mambo yenu. Kwa sasa tushirikiane kujenga Taifa letu Tanzania na serikali yetu ikifanya jambo zuri kama hilo tuisifu. Pia tunazidi kuaminiwa na mataifa makubwa. Au mnataka tuwakatae ili mseme serikali ya Tanzania imewatimua wakimbizi ili mataifa makubwa yatuchukie?

Hapo kwenye bold ndipo ulipoanza kuweka ID yako ya CCM na hapo umepoteza ladha ya thread maana nilishaanza kuelewa nikajua ni jambo jema serikali imefanya kumbe ni sehemu ya promo ya chama chako?
 
Acha kumumunya maneno mkuu, hayo si ma-CHADEMA. hayana sera kazi kunywa viroba tu mpaka wanajiondoa ufahamu kuwa wahajui kinachoendelea BURUNDI.
 
Hapo kwenye bold ndipo ulipoanza kuweka ID yako ya CCM na hapo umepoteza ladha ya thread maana nilishaanza kuelewa nikajua ni jambo jema serikali imefanya kumbe ni sehemu ya promo ya chama chako?
Msumari umekuchoma siyo? Na bado.
 
Mzee wa mahaba niue kazi kweli kweli
Wazee wa mahaba hawa hapa:
IMG_518397614652376.jpegIMG_150564246704619.jpegIMG_348786904836289.jpegView attachment 250970IMG_274141205649915.jpeg
 
Wajinga wote mnaendeshwa na mr.Zero

Sio Dr.? Mnajipa matumaini tu wakati nchi ilishawashinda. Huyo mnayemwita zero ndo amewapeleka mputa mputa kweli mpaka sasa hamjui la kufanya. Kila kitu kimewashinda tazama mpaka dola inafikia 2030 hii si hatari? Kama huyu mnamwita zero basi nyie ni Mr. Negative
 
Wanakazana kuwaingia wakimbizi waokoe jahazi la kura maana hali ni mbaya sana. Na msipomweka Lowasa kugombea kibarua mnacho. Ndoorooooobo we

Ila kwa akili ya kawaida tu, hv kura 20,000 zitasaidia nn? Nadhan mlitaka serikali ikatae kuwapokea ili muongee. Kiohoja nadhan mmefariki.
 
Watu wanapoongea kuhusu HISIA ZISIZO NA MASHIKO ni SHIDA sana. Unaowasema hawajatamka lolote angalau uwe na reference,ukiulizwa sababu ya hizo hisia zako utasemaje?Any source?Moja ya maadui wakubwa wa Taifa hili ni Ujinga,bahati mbaya UJINGA UMEKUWA RAFIKI WA CCM, ndiyo maana mleta mada naye ni Mjinga!
 
Back
Top Bottom