TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Wiki iliyopita mara tu baada ya Rais kufanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri ambapo Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye alipoteza nafasi ya Waziri wa Habari , Sanaa na Michezo, wapinzani kwa tabia yao ya kuvizia vizia kama Fisi waviziavyo mifupa baada ya Simba kushiba walijua wamelamba dume.
Vijana wa BAVICHA walitanda mitandaoni mithili ya viwavi jeshi kumpongeza nape huku wakilaani uwaziri wake kutenguliwa. Wapo wapinzani waliowahi nyumbani kwa Nape zaidi ya hata Waziri wa Mambo ya ndani , Mwigulu Nchemba alivyowahi eneo la tukio kule Mbande pale majambazi walipovamia benki ya CRDB. Eti walikwenda kumpa moyo.
Jana wakati Mheshimiwa Nape anakabidhi ofisi kwa Waziri Mwakyembe aliufunga mjadala na kupoteza kabisa matumaini ya wapinzani pale alliposema kama kuna watu wanadhani anahama CCM wanapoteza muda, kwamba CCM ni chama bora sana. Nape alipigilia msumari kwa kusema hata kama kuna mambo ya kurekebisha ndani ya CCM hawezi kufanya hivyo akiwa nje ya CCM.
Mytake: Kwa kitendo hiki alichokionesha Nape cha jinsi gani alivyokomaa kisiasa, pongezi za wapinzani ni muhimu zaidi kulikoni zile alizopata baada ya uwaziri wake kutenguliwa. Kufanya hivyo wapinzani watakuwa wanawajenga vijana wao kisiasa ili kuepukana na mihemuko isiyo ya lazima pale wanaporekebishwa na viongozi wao. Vijana kama akina Zitto Kabwe, Devid Kafulila na wengine wengi walijikuta wakitangatanga kwa sababu tu ya kukosa uvumilivu wa kisiasa.
Nisiwasahau vijana wa BAVICHA mitandaoni ambao waliongoza kutoa mapovu kumuona Nape shujaa pale alizungumza na wana habari katika hoteli ya PROTEA.Jana wamemgeuka na kumkandia tena baada ya kuonesha msimamo wake juu ya imani aliyo nayo kwa rais na chama chake.
BAVICHA wanazidi kuonesha utoto, kuwa vigeugeu na pengine tunaweza kusema ni wamekaa kimipasho mipasho tu bila kujua wanasiamia nini. Washauri wa hawa vijana wa BAVICHA mitandaoni bado wana kazi kubwa sana.