Wapinzani Kigeugeu.

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,701
1,389
Nyimbo mpya iliyotolewa na CCM,

Hawa wapinzani kigeugeu,
Nikitaka kuiba kura wananigeukia,
Nikitaka kununua vitambulisho wananigeukia,

wananigeukia,wananigeukia,

Hawa wapinzani kigeugeu,
nikitaka kuorodhesha vitambulisho wananigeukia,
nikitaka kuhonga chakula wananigeukia,

wananigeukia,wananigeukia,

Hawa wapinzani kigeugeu,
nikitaka kutumia polisi wananigeukia,
nikitaka kutisha wananchi wananigeukia,

wananigeukia,wananigeukia,

Hawa wapinzani kigeugeu,
nikitaka kuandikisha mamluki wananigeukia,
nikipinga mgombea wao wananigeukia.

wananigeukia,wananigeukia.
kigeugeu,kigeugeu.
 
Nikitaka kutmia uddini wananigeukia,
DC kumgeuza mwislamu huku anafuga kitimoto wananigeukia
WANANIGEUKIA, WANANIGEUKIA

Nikisema wanaleta wapalestina, wananigeukia
Nikasema wamechanganya na Walibya, wananigeukia
WANANIGEUKIA, WANANIGEUKIA....
 
Hahahaha! Mkuu hapo kwenye DC mwislam afu anafuga kitimoto umenvunja mbavu mbili...lol... Kweli wapinzani kigeu geu! Wamemgeukia mpaka DC na kumvua kanzu...ooh sorry i mean hijabu!
 
Hawa wapinzani kigeugeu,
Nikitaka kujiburudisha na wake za wanachama wananigeukia,
nikitaka kuchoma nyumba wananigeukia.

Wananigeukia,wananigeukia,

Hawa wapinzani kigeugeu,
Nikitaka kuleta makatapila(Mkapa) wananigeukia,
Nikimwomba Rostam aokoe jahazi wananigeukia,

Wananigeukia,wananigeukia,
kigeugeu,kigeugeu.
 
Pole upinzani siku hizi ni tofauti na miaka ile ndiyo maana kila kila kitu wanakugeuzia! Jipange nawe uwageuzie kibano kwa kitumia wizi wa kura hapo tu ndiyo watashindwa kukugeuzia.
 
Ninapofanya juu chini ili kuchakachua poll results-wapinzani wananigeukia.>>>Hata wale waliolia alipojiuzulu R.A-C.C.M wameigeukia.>>>Mpiga kura kigeugeu>>>Wamekula ubwabwa lakini vigeugeu>>>Msimamizi kigeugeu>>>Tumewapa khanga lakini vigeugeu.
 
Hapa mkuu naona Rostam anatuma salamu CCM anauma na kupuliza hahaha!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom