Wapigania uhuru wa Zanzibar waungwe mkono!

24 hrs ni muda mrefu sana kwa siasa za Tanzania let alone Zanzibar! Hivyo April 2011 ni sawa na mwaka 1947. Mambo yanakwenda kwa speed kubwa.

Na kama niliandika, wapo wakubwa wengi sana wanaokubaliana na hoja za Maalim Seif (Tofauti na huko awali). Ndio maana sikubalini na hoja yako kwamba "tuwape watu wenyewe na sio kundi la watu". For better for worse, wanzanzibari waachwe wafanye wanavyotaka. LET ZANZIBAR GO.
Ahahaha! hahaha! acha madongo mkuu wangu Mzee Yusuph yupo pale na Bi Kidude tunaye na ndio wasanii wanaotamba hadi kesho. tena JK kambeba Yusuph na kumleta huku Mtanzania kutumbuiza represent ZnZ...Zanzibar hubadilika kila miaka 200 maana mitaa ni ile ile na watu maarufu ni wale wale toka 1947, kama katokea mwingine basi muuza Unga!..
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Mkuu wangu mawazo ya serikali moja DULITY ni kupuuza Muungano wa nchi mbili.. Zanzibar ni nchi ina soveign yake na muhimu sana ktk majadiliano kama haya tuheshimu kuwepo kwa Zanzibar na kuenzi Muungano uliopo..Hivyo kuifananisha Zanzibar na Mikoa ya Mwanza, Arusha na kadhalika ni wazo linalopotosha zaidi..

Kuna njia mbili tu zinazoweza kukubalika 1. Kuunda serikali tatu,(Ya UMoja wa Taifa, na zile za Tanganyika na Visiwani) ama 2. Kuuvunja Muungano kutokana na kura za maoni za Wazanzibar ambao wataambiwa ukweli na wawakilishi wa makundi mawili majukwaani. Ikiwa ni pamoja na kundi la wale wanaoutaka Muungano wakiwaeleza wananchi kwa nini muungano ni muhimu kwao, halafu wale wanaopinga Muungano na kwa nini hautakiwi.. Kisha wananchi wakisha elimishwa hilo Wazanzibar wote watapiga kura za maoni yao na yataheshimika. Kura za Hapana zikiwa nyingi tutaendelea na mfumo uliopo wa serikali mbili na pengine kurekebisha tu kero zilizopo..

Mkandara, Zanzibar (or Seif & co if you like) wamemwaga mboga, sasa ni zamu ya Tanganyika kumwaga ugali. Zanzibar wanataka muungano wa mkataba, sasa Tanganyika wanasema DUALITY. Vinginevyo tugawane mbao, lakini hatuwezi kuendelea na kelele tena, kuna mambo mengi ya msingi ya kushughulikia, wanafunzi wanakaa chini, huduma za afya ni mgogoro, usafiri ni tabu tubu. Muungano ni kitu gani? DUALITY or MBAO. basi. LET ZANZIBAR GO!
 
Mkandara mimi sikubaliani na wazo la kuona hizi nchi kama ziliumbwa kwa amri ya mungu. Kama zilianzishwa na wanadamu basi wanadamu hao hao wanaweza kuzivunja. Nani alitaka Zanzibar iwe nchi, ni hawa waliopo sasa? Historia inaonyesha nchi ya Zanzibar ya sasa ni ile iliyokuwa mwaka 1884?
 
Last edited by a moderator:
Ahahaha! hahaha! acha madongo mkuu wangu Mzee Yusuph yupo pale na Bi Kidude tunaye na ndio wasanii wanaotamba hadi kesho. tena JK kambeba Yusuph na kumleta huku Mtanzania kutumbuiza represent ZnZ...Zanzibar hubadilika kila miaka 200 maana mitaa ni ile ile na watu maarufu ni wale wale toka 1947, kama katokea mwingine basi muuza Unga!..

Ndio sababu nikakuuliza lini mara ya mwisho kufika Zanzibar? Ile ya 2011 haipo na haitorudi tena!
 
Mkandara, Zanzibar (or Seif & co if you like) wamemwaga mboga, sasa ni zamu ya Tanganyika kumwaga ugali. Zanzibar wanataka muungano wa mkataba, sasa Tanganyika wanasema DUALITY. Vinginevyo tugawane mbao, lakini hatuwezi kuendelea na kelele tena, kuna mambo mengi ya msingi ya kushughulikia, wanafunzi wanakaa chini, huduma za afya ni mgogoro, usafiri ni tabu tubu. Muungano ni kitu gani? DUALITY or MBAO. basi. LET ZANZIBAR GO!
Hiyo DUALITY kaisema nani? Hakuna kitu Muungano wa Mkataba kwa nchi zilizokwisha vunja Muungano..Ni maajabu haya kudai ndoa uvunjike kuwe na mahusiano ya kujamihiana tu.. Ile ya mwaka 2011 ndio nini ikiwa leo rais wa Zanzibar ni wa mwaka 2010 bado kiongozi na huyu Maalim Seif yupo toka tupate Uhuru!..

Bora waseme tu tunataka kuuvunja muungano na tuishie hapo kuiko wao kuendelea kudai muungano wa Mkataba kwani kawaambia tunataka mkataba?. Unajua hawa wanasiasa wetu hawajui kabisa kujenga Hoja maana wakisema kuvunja muungano tu inatosha kuliko kuwalazimisha Wazanzibar kuingia ktk Mkataba ambao miaka 10 ijayo watasema hawautaki na kusema ni JK na Dr. Shein mdio walotuweka ktk Mkataba. hawa vigeugeu sana na wepesi sana kubadilisha maneno..

Juzi tu walishangilia serikali ya mseto lakini bado wanasema bara inawatawala ilihali tazama hapo juu biongozi wa nchi za nje wakikutana na rais wa zanzibar na mawaziri wake.Hapo watamsifia Dr.Shein wakati umeme unatoka bara..
 
Mkandara mimi sikubaliani na wazo la kuona hizi nchi kama ziliumbwa kwa amri ya mungu. Kama zilianzishwa na wanadamu basi wanadamu hao hao wanaweza kuzivunja. Nani alitaka Zanzibar iwe nchi, ni hawa waliopo sasa? Historia inaonyesha nchi ya Zanzibar ya sasa ni ile iliyokuwa mwaka 1884?
Bila shaka nchi ipo na itaendelea kuwepo lakini kina nani watapewa dhamana ya kuiongoza hilo ni swala la Wananchi wenyewe. Mbona Mkoloni alitupigisha kura tunachagua chama na uongozi tunao utaka mbele ya UHURU wetu.. iweje leo hii tuwakabidhi nchi wahuni waliokuwa wakiitumikia serikali ya Sultan kwa sababu tu wameweka matangazo kila nyumba..Wafanye referendum kisha uchaguzi tutawapa wanaostahili kuchukua dhamana hiyo na tutawalinda, tatizo liko wapi?..
 
Hawa jamaa wangefanya haraka hii movie yao, Usiku umeendelea sana mchana umekaribia movie iishe tukalale!!!

Kwa ufupi swala la Zanzibar linanikumbusha sana yaliyotokea East Timor (Timor Leste), pamoja na kufahamu historia ya nchi hii miaka ya nyuma, nilijionea hali halisi baada ya kukaa huko kikazi kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa ufupi
Walipata uhuru 1975
Baada ya siku 9 wakawa chini ya indonesia (Invaded)
Wakapigana sana na indonesia (of course they were right to fight)
2002 wakapata uhuru wao
April 2006 (after 4 years) zilipigwa sana wao kwa wao (mambo ya East and West), raha ya uhuru ikawa imechafuka vibaya sana


Zanzibar, tunawatakia mema wasiwe kama East Timor, ila waondoke haraka tumechoka na kelele zao.
 
Hiyo DUALITY kaisema nani? Haukna kitu Muungano wa Mkataba kwa nchi zilizokwisha vunja Muungano..Ni maajabu haya kudai ndoa uvunjike kuwe na mahusiano ya kijamiana.. Ile ya mwaka 2011 ndio nini ikiwa leo rais wa Zanzibar ni wa mwaka 2010 bado kiongozi na huyu Maalim Seif yupo toka tupate Uhuru!..

Bora waseme tu tunataka kuuvunja muungano na tuishie hapo kuiko wao kuendelea kudai muungano wa Mkataba kwani kawaambia tunataka mkataba?. Unajua hawa wanasiasa wetu hawajui kabisa kujenga Hoja maana wakisema kuvunja muungano tu inatosha kuliko kuwalazimisha Wazanzibar kuingia ktk Mkataba ambao miaka 10 ijayo watasema hawautaki na kusema ni JK na Dr. Shein mdio walotuweka ktk Mkataba. hawa vigeugeu sana na wepesi sana kubadilisha maneno..

Juzi tu walishangilia serikali ya mseto lakini bado wanasema bara inawatawala ilihali tazama hapo juu biongozi wa nchi za nje wakikutana na rais wa zanzibar na mawaziri wake.Hapo watamsifia Dr.Shein wakati umeme unatoka bara..

Ndani ya miaka 2 na nusu hivi Seif na wenzake wameshabilisha kauli mara chungu nzima. Kwanza ilikuwa 'nitashughulikia kero za muungano' then ikaja 'serikali tatu' ghafla tukasikia 'muungano wa mkataba'. Na hapa kwenye muungano wa mkataba ndipo ngoma imelia kweli kweli, na hakuna jibu la maana la 'mkataba wa nini?

Mwanasheria mkuu wao yeye alishauri muungano wa mkataba kama wa Swiss (please don't ask me Swiss wana mkataba wa aina gani?), bado akabadilika na kusema muungano kama EU! Yuko bwana mwingine maarufu anaitwa Ahmed Rajab, yeye alishauri -kwa mtindo wa kupiga Watanganyika darasa, kuwa tuwe na muungano kama ule uliofeli wa Senegambia. Yaani tuige kitu kilichofeli (brilliant!).

Kauli mbiu nazo zimekuwa zinabadilika; Mwanzo ilikuwa tuachwe tupumue, baadae ikaongezeka 'uhuru kamili'. Na wakati series yote hii inacheza Tanganyika anatizama tu huku billl zinalipwa!

Kitu ambacho Maalif Seif hajafanya hadi sasa, ni kutamka waziwazi kuwa muungano 'uvunjwe'. Neno kuvunja hajatamka kwa sababu anajua hata huu muungano wa sasa ni wa mkataba. Na ili kuwa na muungano wa aina yoyote ile ni lazima kwanza kuvunja huu wa sasa. Atakwepa kutamka neno 'kuvunja' hadi lini, na ni kweli anataka Zanzibar huru au anataka Zanzibar na Cash Cow?

November inakuja, tuangaze macho ili tuone nani anashuka kwenye boti kuelekea Dodoma.
 
Mkuu Mwanakijiji, nakuunga mkono kabisa hoja yako.

Tunataka maneno ya Wazanzibar wanaodai wanabanwa na wanatawaliwa na mkoloni mweusi yaendane na matendo yao. Waoneshe kabisa kuwa hawataki Bunge la Muungano, hawataki kufanya kazi kwenye serikali ya muungano, wasusie mambo ya muungano.

Tumechoka na kelele zao, na kwetu Watanganyika tunawaona Wazanzibari wanazidi kutukera.

Please Wazanzibar, chukueni hatua zinazoonesha mnakusudia kweli mnachokisema. Na sisi hatupendi kuwa wakoloni, Mwende na Zanzibar yenu, nasi tubaki kwa amani na Tanganyika yetu.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji: Blogs zinazinduliwa kila siku kudai Zanzibar huru na kututukana kuwa ni wakoloni weusi:

NA FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI
12th August 2012
Vigogo wachache wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wanaolilia Muungano wa mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar ni viongozi haswa wanaojuwa nini Zanzibar na inawauma sana ndio maana wakaipigania kwa nguvu zote kama ilivyo kuwa na Chama cha Afro Shraz Party. Kada maarufu wa CCM Zanzibar, Baraka Mohamed Shamte, alitoa matamshi hayo katika mahojiano maalum na mwandishi wetu wa siri wa FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI nyumbani kwake Mkunazini mjini Unguja jana.

Shamte alisema kundi linalojaribu kuzuia mabadiliko yasije hapa Zanzibar ni la vibaraka na wasaliti wapya waliolipwa ujira na fedha nyingi toka ndani ya Jamhuri ya Muungano wa (Tanzania.)Tanganyika. Shamte alisema Waraabu toka Oman walijenga zanzibar na kuifanya nchi maarufu duniani na kuikuza kiuchumi na kuifanya kutambulika ulimwengu mzima Zanzibar inajulika kwa uchumi na biashara na wasomi walio bobea kuanzia miaka 132 tokea mwaka 1832 hadi 1964 hadi pale chama cha ASP kilipofanyiwa shawishiwa na Watanganyika na kupandikizwa sumu kali ya Wazanzibari kuwachukia dungu zao kutoka Oman nakuamuwa kufanya mapinduzi yaliyo sababisha vifo vya watu wasio kuwa na hatia na kunajisiwa wanawake na kulazimishwa kuolewa kwa nguvu wanawake wa kizanzibar na kuolewa na mwatana ya kibara ambayo kwa wakati huo yalikuwa hata kutahiriwa hayajatahiriwa.wabara wakiwandanganya Wazanzibari kuwa huu ni ukombozi wa haki kupitia njia ya Mapinduzi ya damu Januari 12, 1964.kumbe ilikuwa Wazanzibari wanapinduliwa wao na mwatwana ya bara mpaka leo wazanzibari tunatawaliwa na wabara nusu karne sasa.

Alisema jumla ya wafalme 11 waliishi hapa Zanzibar kwa zamu na Wazanzibari walifurahi sana na kuishi kwa amani na utulivu isipokuwa wale wanaojita wafrika kutoka Tanganyika na nchi nyengine walikuwa wakija hapa kwa kitambulisho maalum na kuchuma karafu msimu ukisha lazima warudi kwao Tanganyika hilo liliwachoma sana Watwana hao wa kiaafrika waliokuwa wakiona kama wanakandamizwa kwa karne nyingi, wakionewa na wakibaguliwa katika nchi hii ya Zanzibar kwa sababu hawakuweza kufanya mambo yao machafu kama wanavyofanya sasa pia waliona kama wamenyimwa haki za msingi bila ya kuruhusiwa kuishi hapa au kaka hapa bila ya kibali maalum.
"Utawala wa kifalme uliotawala Zanzibar uliitisha kura na kufunga mkataba na wanyeji wa Kizanzibari,maana Wazanzibari walishawahi kuvamiwa na Mreno na ikabidi wawaite watu wa Oman kuja kumuondoa kwa nguvu mtawala wa Kireno maana mtawala wa kienyeji enzi hizo aliyeitwa Mwinyimkuu hakuweza kupigana na Mreno.na mara zote Mreno alitaka kuitawala Zanzibar bila ya ridhaa," alieleza Shamte.
Alisema wanaojitokeza sasa kutaka Tanganyika na Zanzibar ziwe na Muungano wa mkataba, aliwaita hao ndio Wazanzibari na ndio majabari wanaopigania kuurudisha Zanzibar yetu tunayo itamani kwa miaka mingi sana. ukoloni huo kwa sasa basi lazima Zanzibar ijitawale yenyewe.

" Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume walifunga mkataba uliokuwa na ridhaa kupitia ndani ya nyoyo zao vyama vyao havikujuwa lolote,wala hawakuwauliza wananchi wa Tanganyika wala wa Zanzibar pamoja na Baraza la Mapinduzi Zanzibar halikujuwa lilijuwa baadaye na Bunge la Tanganyika halkathalika halikujuwa hii ilikuwa ni mipango ya chini kwa chini baina ya nyerere na waliomtuma huku akimhada mzee karuma," alisema Shamte.

‘Namtaka Hassan Nassor Moyo na wenzake wadai Zanzibar kwa nguvu zote mkataba mkataba hakuna cha mkataba hii ni nchi yetu kwisha habari yake". Alisema Shamte. Kada huyo wa CCM alieleza kuwa Waoman walikuja hapa Zanzibar kabla ya mabeberu wa nchi za Ulaya kuigawa Afrika katika mkutano uliofanyika mjini Berlin huko Ujerumani mwaka 1884/1885 kinyume na hiari ya waafrika wenyewe isipokuwa Wazanzibari mabeberu hao wa nchi za Ulaya hawakufanikiwa walipofika Zanzibr.

Shamte ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Zanzibar Mohamed Shamte Hamad, alisema Waoman walipokuja Zanzibar waliunganisha utawala wa kienyeji ulioongozwa na Mwinyimkuu ambaye alikuwa na Makao Makuu yake huko Dunga Mkoa Kusini Unguja baina ya utawala wa Zanzibar na wakiomani na ndio maana makao makuu ya Omani pia yalihamishiwa hapa Zanzibar. Mwanasiasa huyo machachari alisema chama cha ASP kiliwachukulia waaarabu toka Oman ni dungu zao walio changanyika na wazanzibar kwa nguvu zote na mashirikiano na kuishi nao kwa pamoja hapa Zanzibar kwa miaka mingi kwa hishima na adabu na utu na kusaidiana kwa kila hali yao yoyote.

Alisema Uhuru kamili wa Wazanzibari ni ule wa mwaka 1963 na siyo wa 1964 kama inavyoaminiwa na vibaraka walioosalia Zanzibar wakienddelea kumuunga mkono Mkoloni mweusi Tanganyika kama unavyosema wewe hahahahaha akacheka kidogo aliyepinduliwa Zanzibar Januari 12,1964 Jamshed bin Abdullah. Alitoboa siri na kutaja kuwa hata baba yake alijuwa kama kuna plani ya kupinduliwa ila hakujuwa afanye nini maana wakati ule wazanzibari waligawiwa kama hivi sasa tunavyo sabaratishwa hatimaye tukapinduliwa na kufikiri tumepinduwa.

Alisema kitendo hicho peke yake kilionyesha ni jinsi gani hila na hadaa zilivyoandaliwa baaina ya Nyerere na walio mtuma Nyerere kuimaliza Zanzibar kati ya vyama vya ZNP , ZPPP,na ASP mfalme wa Waingereza alianzisha kwa makusudi maana alijuwa watu hapa watabaguwana na kuchukiana na hiyo ndio ilikuwa njia yao ya kututia ndani ya tumbo la Tanganyika na kuwalaghai Wazanzibari.

Shamte ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa ASP Youth League, alisema ili kuthibitisha ZNP na ZPPP na ASP ni vyama vya wananchi wa Zanzibar,isipkuwa vililetwa na Mgereza ili awagawe tuchukiane kama ilivyo sasa ooh wewe CCM ooh wewe CUF ooh wewe UAMSHO matokeo yake vilishindwa kupeperusha bendera yao na kujikuta tunapinduliwa na Watanganyika na wakajikuta wakipeperusha bendera aliyo kuja nayo JOHN OKELLO ya Kitanganyika chini ya utawala wa Kitanganyika.

Alisema chama cha ASP baada ya Mapinduzi, mara moja kilipeperusha bendera ya Kitanganyika iliokuwa na rangi nyeusi, buluu ya maji bahari na kijani ili kuionyesha dunia kuwa chama cha waafrika wa Zanzibar kimeleta ukombozi wa haki na kuunda dola mpya hivyo ndivyo ilivyo thaniwa kumbe ndio ukoloni wa Kitanganyika umetuvaa mpaka leo nusu karne bado tunatawaliwa na wafanyaji kazi maana hawa wakati wa Zanzibar Zanzibar Zanzibar alirudi Zanzibar Zanzibar hawa Watanganyika walikuwa ni wafanyaji kazi wa ndani kama unavyo ona sasa na kuchuma karafu tu hawa leo hii wanatutawala na kutupeleka kipunda punda hapa lazima Zanzibar itoke katika tumbo lao.alisema Shamte.
​FREE ZANZIBAR PEOPLE FROM MKOLONI MWEUSI: SHAMTE ASAMA WANAOLILIA MUUNGANO HUU AU SEREKALI MBILI NI VIBARAKA WA WATANGANYIKA

Nasi tunawaombeni muoneshe kwa vitendo kuwa mmedhamiria.

Jitoeni Bunge la Muungano, Jiuzuluni nyadhifa zenu Serikali ya Muungano.

Tumewachoka nendeni na Zanzibar yenu
 
Bila shaka nchi ipo na itaendelea kuwepo lakini kina nani watapewa dhamana ya kuiongoza hilo ni swala la Wananchi wenyewe. Mbona Mkoloni alitupigisha kura tunachagua chama na uongozi tunao utaka mbele ya UHURU wetu.. iweje leo hii tuwakabidhi nchi wahuni waliokuwa wakiitumikia serikali ya Sultan kwa sababu tu wameweka matangazo kila nyumba..Wafanye referendum kisha uchaguzi tutawapa wanaostahili kuchukua dhamana hiyo na tutawalinda, tatizo liko wapi?..
Tatizo liko kwenye nyekundu. Mbona unaongea kama sisi ni wakoloni kweli tunaotaka kusimamia nchi nyingine kujitawala? Wao hawataki huu muungano tulio nao wanataka wa mkataba ama tuachane nao au tukubaliane nao. Ama waachane nasi au wakubaliane nasi. Suluhisho ni serikali moja, shirikisho au Mkataba?
 
Tunaitaka Tanganyika yetu. Naunga mkono hoja ya Mwanakijiji tukivunja Muungano huu tujihesabu tumeshindwa kuungana. Tubaki na Tanganyika au tubaki na Tanzania moja.
 
Tunaitaka Tanganyika yetu. Naunga mkono hoja ya Mwanakijiji tukivunja Muungano huu tujihesabu tumeshindwa kuungana. Tubaki na Tanganyika au tubaki na Tanzania moja.

SG8

Hivi sasa Tanzania ziko ngapi?

Soma hii:
Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.Uk 11-12 link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Unajua kuwa kuna EAC au vipi? Na pia linakuja shirikisho la EA. link https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/100638-shirikisho-ndani-ya-shirikisho.html

Kama umefahamu baada ya kusoma hapo, hili ndio la kulisimamia na kulifanya.
Saidia kusambaza ujumbe. Waamshe ndugu, jamaa, marafiki. Ufumbuzi wa tatizo hili upo tokea 1994 bado utekelezaji tu.
 
Mimi ni muumini mkubwa sana wa muungano....lakini kwa hizi kelele za kila siku, nataka muungano uvunjike hata leo.
Wazanzibar wanatakiwa waelewe kuwa tatizo si Watanganyika bali ni Baadhi ya Viongozi wa Tanganyika......
Wazanzibari wengi hasa wale ambao hawajawahi kufika Tanganyika wamekuwa wakifikiri watanganyika wote wanafurahia matatizo ya Zanzibar....Polisi wanavyopiga wananchi zanzibar ,lawama zinakwenda kwa kila Mtanganyika ,Dawa zinavyokosekana hospitali zanzibar lawama zinakwenda kwa kila Mtanganyika,Ukianagalia vizuri....watanganyika wengi Hawajui hata zanzibar inafananaje ,kwa hiyo si haki hata kidogo kumtwika Mtanganyika wa kawaida lawama za matatizo ya Zanzibar.....

Wazanzibar wana haki ya kujitenga ..kwani miaka mingi imepita tangu huu muungano ufanyike..lakini hali za maisha zinazidi kuwa mbaya siku hadi siku....hali za maisha zimekuwa mbaya kuanzia Zanzibar mpaka Kigoma,Arusha mpaka Mtwara......Kwa hiyo hata Mtwara wakitaka kujitenga mimi ntakuwa wa kwanza kuwaunga mkono.....

lakini wazanzibar wanatikiwa wajue kumpigia kelele mtanganyika wa kawaida hakuwezi kuwasaidia...wapeleke
hoja bungeni ...baraza la wawakilishi...baraza la mawaziri..wafungue kesi mahakamani.....

Lakini wasinambie mimi Mtanganyika wa kawaida niwaachie wapumue.. sikumbuki hata siku nliyo wakaba

Wazanzibari ni ndugu zangu na nawaheshimu sana,jaribuni kupeleka malalamiko yenu sehemu zinazohusika..
 
Tunaitaka Tanganyika yetu. Naunga mkono hoja ya Mwanakijiji tukivunja Muungano huu tujihesabu tumeshindwa kuungana. Tubaki na Tanganyika ...

SG8

Tutakuwa hatujashindwa kuungana lakini tutakuwa tunaleta muungano mkubwa zaidi.

Mkataba wa kufufua EAC ulikubaliwa 1999 na ulianza kutumika mwezi wa saba 2000. http://www.eac.int/index.php?option=com_content&view=article&id=1&Itemid=53
Badala ya kwenda EAC kama Tanzania, tulipaswa kwenda kama Tanganyika na kama Zanzibar.

Tumechelewesha tatizo kwa miaka 12. Wakati Mwalimu Nyerere ambaye ndie mwasisi wa Muungano alishasema ili kufanya mambo kuwa rahisi, tukifufua EAC basi tutaepuka ugumu wa muungano wa Tanzania kwa kufufua serikali ya Tanganyika.Pia nia ni kuungana na nchi nyengine nyingi ili kufanikisha umoja wa Afrika. Basi jambo lililo rahisi ni kuwa na serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar na kuingia mchakato wa muungano mkubwa zaidi, wenye wanachama zaidi.

Ni kusema kuwa mwalimu aliamini katika Muungano wa mfumo wa Shirikisho.
Tarehe muhimu... 1994.....1999....2000.....2012.

"Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. " Mwalimu Nyerere ansema hayo uk 11. link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Kwa nini tunaogopa kitu ambacho tunajua kuwa kitatokea tu hata kama tunakichelewesha?
 
Unafikiri wazanzibar wako tayari kwa aina hiyo ya "duality" ambapo kunakuwa na Pemba na Unguja kama mikoa si taifa moja. Unataka kusema Wanzibar si wamoja na jina lao la sasa la nchi yao walipeleke wapi? HIvi kwenye muungano wetu ni lazima kuwasikiliza Wazanzibar au hata Watanzania (Tanganyika?) wanaweza kuwaambia wazanzibar "nendeni zenu" kama wewe unavyowahimiza "watoke" kwenye muungano?

bado watabakia Wazanzibari; Uzanzibari wao haufutiki kwa kuwa kwenye taifa moja. Texas ilikuwa ni nchi kabla ya kuingia kwenye Muungano wa Marekani. Na leo bado wapo na watu wanaendelea kuitwa "Texans" na wanaendelea na baadhi ya mambbo yao kama ilivyokuwa zamani. Mbona tulishakuwa na tawala nyingine kabla ya kuingizwa kwenye Tanganyika? Wanyamwezi, Wasukuma, Wahaya, Wachagga walikuwa na himaya zao na wote wameingia kwenye nchi inaitwa Tanzania lakini haijawafanya wasiwepo Wachagga au Wanyakyusa. Identity ya Wazanzibari haifutiki kama vile identity ya watu wa maeneo mengine isivvyofutika.

Binafsi siwaambii watoke kwani Watanganyika hatujawahi kuwakataa Wazanzibari ni wao wanatukataa sisi na kutuona kuwa ni wakoloni. Msimamo huu siyo wa mtu mmoja mmoja ni wa serikali ya Zanzibar chini ya Dr. Shein. Sasa ili tusionekane kuwa ni wakoloni ni vizuri tuwasaidie watoke na kurejesha 'dola yao" ili wasionewe tena. Hili si jambo baya hata kidogo kwani hakuna furaha yoyote kwa Watanganyika kuonekana wanainyonya nchi maskini, ndogo kama Zanzibar.
 
Bora waseme tu tunataka kuuvunja muungano na tuishie hapo kuiko wao kuendelea kudai muungano wa Mkataba kwani kawaambia tunataka mkataba?.

hii ndio ugomvi wangu vile vile; kutaka kutokana wanataka wao, na ni wao wanaoona kuwa tunawanyanyasa na kuwabana na kuwakandamiza lakini hawataki kutoka. Wanataka kutoka na kurudi kwa njia ya "muungano wa kimkataba"! Swali lako linasimama: wakishatoka nani kawaambia tunataka muungano wa mkataba. Binafsi sitaki hata kujaribu kujibu swali hilo ninachotaka ni kuwa watoke kwanza halafu wakishatoka waone kama tutaitisha kura ya maoni huku bara kutaka muungano wa mkataba nao.
 
Mzee Mwanakijiji, nimesoma kwa umakini sana andiko lako na kulielewa. Kama alivyosema Hayati Baba wa Taifa Mwl. J. K. Nyerere, chochoko za kutaka muungano uvunjwe zinaletwa na watu wachache na wengi wao ni wazanzibar ambao ni viongozi wakiwemo akina Maalim Seif na Jussa. Binafsi mpaka sasa sioni manufaa yoyote ya maana specific ambayo watanganyika tunayapata kutoka Zanzibar kiasi cha kufikia hatua ya kuogopa kuvunjika kwa muungano. Nionavyo mimi, manufaa yanaweza kuwa ni ya kijumlajumla tu kwamba MUUNGANO UMELETA UMOJA na kama wote tujuavyo, UMOJA NI NGUVU.

Kuuvunja muungano ni hatua kubwa ambayo haiwezi kuchukuliwa kwa kufuata kelele za akina Maalim Seif, Jussa na watu wengine wachache yumkini wenye malengo yao binafsi. Kwa kuwa kelele na chokochoko za kuuvunja muungano zimesikika muda mrefu na hasa kutoka Zanzibar, ni vizuri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ichukue jukumu la kuitisha seriously kura ya maoni. Lengo kuu la kura ya maoni liwe ni kuwataka wazanzibar waseme kama wanataka muungano au hawautaki, full stop. Kura hiyo isielekee kuuliza kwamba kama wanataka muungano wanataka uwe wa aina gani. Katika hili, nakubaliana na Mzee Mwanakijiji kwamba aina yoyote ya muungano iwe ya mkataba au mahaba (sijui ndiyo nini!!!!) haiwezi kukosa chokochoko kama inavyotokea Ulaya.

Kura ya maoni itoe jibu moja tu TUNATAKA MUUNGANO au HATUTAKI MUUNGANO. Suala la muungano uboreshwe au kero ziondolewe kamwe haliwezi kuisha hata tuwe na muungano wa aina gani. Kinachotakiwa ni kuwa na utashi na utayari wa kuungana with a long term target ya kuwa kitu kimoja, kama Mwl. Nyerere alivyotaka kwamba watanganyika na wazanzibar wote kwa pamoja wajivunie utanzania wao na siyo utanganyika au uzanzibar wao. Hatua hiyo ya kuungana na kuwa kitu kimoja ni nzuri sana lakini tatizo ni watu wachache wenye malengo ya kisiasa. Watu hao wanachoangalia ni je, hatma yao kisiasa ikoje. Wakifikia hapo na kuona giza mbele, lazima wapige kelele za chokochoko. Hao ndiyo akina Maalim Seif na Jussa.
 
Back
Top Bottom