'Wapiganaji' walioko CCM wanapigania nini hasa?


wamekaa kimya katika issue zote hizo muhimu wanasubiri uchaguzi ukaribie halafu ndio waamke na kudai walikuwa wanapinga hayo yote uliyoyataja utamsikia hata salim atadai alikuwa anapinga yote haya. kiongozi mzuri utamjua wakati dhuluma inafanyika na sio wakati wa uchaguzi.
 

Mkuu Mwanakijiji

Tafakuri yako jadidi mpaka leo haijapata jibu sahihi.

Pengine, tusubiri kwa miaka mingine minne ndipo tutajua wapinaji waliopo CCM wanapigania nini hasa...!
 
hiki ni kikundi kilichojipambanua kupambana na ufisadi ndani ya ccm na kiliongozwa na samweli sitta akisaidiwa na anna klango, harison mwakyembe,kangi lugola, lukasi sellelii na aloyce kimaro wa vunjo moshi bila kumsahau nape na kinana/mukama.la kujiuliza leo ni kuwa kundi lile limetowekea wapi?je ajemda ya ufisadi ndani ya ccm ndo imefungwa?mbona watuhumiwa bado wapo na wanadunda mitaani?hivi wale walikuwa wakipinga ufisadi kwakwa wanauchhukia au waliwachukia mafisadi kwa sababu zao nyingine?hivi walikuwa wazalendo wa kweli au wapiga kelele?tusaidiane kuliuliza swali hili kila inapowezekana kwa mustakbali mwema wa taifa letu.
 
Unajua CCM wana msemo kuwa "mchawi mpe mwanao akulelee" Sita kapewa wizara katulia pia alikuwa na nguvu pale alipokuwa spika,, akawa kama aliyekuwa anaupinga ufisadi..Alipotolewa kwenye USPIKA akawa kama samaki aliyetolewa kwenye maji,, sawa na nape na Mwakyembe.Walipopewa wizara na kutolewa pale walipokuwa wakijipambanua kama wapinga ufisadi waliweka kipaumbele kwenye wizara zao..Kinachonipa shida na mimi kuwaona nao ni wapinga ufisadi ni pale wanapomkosoa anayepita makanisana kufanya kampen na wao pia wakapita humohumo lakini kwa namna nyingine kuponda na kufanya kampeni ya kundi lao.
 
Mtu kama Nepi sio mpinga ufisadi ila analifanyia kampeni kundi lake la kina Six na Mzee wa kyela kwa kuwachafua wengine walio tishio kwao..HAKUNA msafi hata mmoja ndani ya CCM.
 
Watasikikaje ili hali watanzania tunapenda kitu kidogo, Wananchi kwasasa wanafagilia watu wenye pesa, kama huamini angalia kwenye harambee na makongamano wanaalikwa akina nani kama wageni rasmi.

 
Hii thread ni mwiba mkali mno na mchungu sana kwa magamba Hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha
 
that is a rhetorical question, wanachopigania ni matumbo. nao huvuma kama pepo za kusi.....
 
Walifanya walioyafanya kwaajili ya umaarufu sasa wamepata vyeo so mission acomplished


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
chama kinaweza kuwa mtambo wa kuzalisha mafisadi hasa hasa pale unapoamua kuangalia sura ya mtu na si sheria inavyotaka-refer Tz na ccm.Kosa kwa Y ni kosa kwa X ni halali
 
ACHA WAFU WAZIKE WAFU WAO-Tanzania bila CCM inawezekana!
 
Mbona sijaona gamba ata moja linauza sura humu ndani.......Kweli huu mwiba
 
We are all work for the own benefits first, and even if you contribute to other you depending something later and new reset after misevaluate focus beyond the untouchable target. By mayala masuka
 
With 7 days to go, najikumbusha tuu, hili ni bandiko la 2009 kwenye uzi huu wa Mkuu Mzee Mwanakijiji,

Nilisema kuna makamanda wa aina mbili, makamanda wa kweli, wanaopigania taifa lao, na makamanda njaa, wanaopigania nafsi zao, na matumbo yao!.

Hata sisi humu jf, tulikuwa na makamanda wetu, tukiwadhania ni makamanda kweli, na makamanda wapiganaji wa kweli, yaani ni wenzetu, kumbe sii wenzetu bali ni wenzao ambao nao ni makamanda njaa tuu ambao wao pia wanapigania matumbo yao kwa formular ile ile ya 'if you can't beat them, join them!, sasa wamejiunga nao, ni wamoja na lao ni moja!.

Jumapili Njema.
Pasco

 

Mungu akubariki Pasco jumapili yetu hii imeanza vizuri kwa kuuweka ukweli hadharani, tunakushukura. Ngoja tufanye mengine kwanza kisha tutarudi. Ila nadhani hii itakuwa thread of the day
 
Last edited by a moderator:
Wanapigania matumbo yao maana ikulu ni tyamu sana kwao na wamefadi kwa mika mingi na hawapendi kuachia ndi maana kuna kaul;i za goli la mkono, ushindi ni lazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…