mifano unayotoa hapa ni Kinyume cha ukweli wa yanayowapata watu wa lohingya, wao wameweka uislam mbele at the expenses ya kukarahisha na kuchefua jamii na imani nyingine za Myanmar
Wewe ni miongoni mwa watu wa ajabu kupata kuwaona! Nimekuwekea source mbalimbali zinazotaja chanzo cha madhira ya Rohingya community!
Nimekuwekea international media, NGOs, Human Rights Watch hadi source ya huko huko Myanmar. Tafuta link ya Myanmar Library! Wote hao wanakuambia source ni kwamba hiyo jamii ipo suppressed hata na serikali yenyewe! Hata kusoma shule za umma above primary level hawarushusiwi! Mwaka 1982 serikali ya kijeshi ikatunga sheria inayosema kwamba wao ni stateless community! Wananyimwa hadi haki ya kusafiri!!!
Pale waliposema enough is enough, wakaamua ku-fight back! Halafu unakuja wewe na wenzako eti wameweka Uislamu mbele! Chuki za kidini zinawafanya muwe watu wa ajabu!!!
Gama kama ni jina lako halisi basi possibly utakuwa ni Mngoni!! Kihistoria, Wangoni ni Wazulu kutoka Afrika Kusini kama wa-Rohingya walivyotoka Bengal!
Sasa leo hii serikali iseme hao Wangoni ni Wazulu kutoka Afrika Kusini na hivyo inapitishwa sheria kwamba nyinyi sio Watanzania na hivyo haki za msingi za kiraia mnapokonywa!
Je, mtavumilia uhuni kama huo maisha yenu yote?! And what if in the next 100 years wakatokea wengine wakasema enough is enough na hivyo wakashika silaha kupambana itakuwa ni sahihi kusema mnataka kupandikiza Ukristo au Ungoni?
Narudia, jamii yoyote ikikandimizwa itafika wakati wataungana tu kupinga ukandamizaji huo! Watatumia kitu chochote kinachowaunganisha; iwe dini, kabla, utaifa au chochote kile!! Yaani nakuona kituko unapobisha hadi kilichoandikwa na gazeti la huko huko Burma.
Toa matongo tongo ya kidini ili uwe objective!!!