Wapiga kura Monduli wanalia,wanashangaa harambee kwa mamilioni za mbunge wao

Mi mzaliwa wa Monduli mkuu Nicholas uliyoyaongea machache yana ukweli ...na bahati nzuri nshatembelea sehemu nyingi za wilaya hii kwa mjini lami zimewekwa hadi njia zisizostahili ...shule kabla ya za kata zilikuwepo nyingi Sana hadi zenye high school Makuyuni ikiwa mfano ....zahanati kwa kweli labda hapo Engaruka tu lakini kila eneo lina zahanati mfano Monduli juu , mto wa mbu ..makuyuni ....n.k tunayo mahabusu nzuri tu Sema ya zamani ....mbunge wetu tulimdai Sana maji na hospitali nzuri kwa kweli amejitahidi. Hayo makanisa kwetu yapo vizuri tena kama kkkt imejengwa juzi tu mkuu ni nzuri Sana. Mzee ni mchapakazi na hadii ukihitaji kumwona personal unaenda .....hii ni baadhi tu usihoji watu njiani we njoo mwenyewe ...mwaka mpya huwa pana sherehe kubwa tu karibu siku hiyo.

ktk red soma mwenyewe halafu jihukumu ,kisha rudi ktk thread hapo juu halfu linganisha unachotetea na nilichokisema.

Heri ya mwaka mpya....na hizo part za jadi kwani watu wameshazichoka na kuziona ndizo uti wa mgongo wa shida zao.
 
sema mbunge wetu katawala muda mrefu Sana jimboni ....ni mbabe kweli ...mlishasema fisadi sawa ....na kwetu hapaendelei haraka Sana maana ni mwisho wa nchi hakuna njia ya kutoka zaidi ya njia ya kuingia na kutokea tatizo La kijografia kwa ufupi mwenye sifa zake mpeni tu,....fwatilieni wilaya zingine mfananishe.
 
Wapiga kura za Monduli wameanza funguka rasmi.

Wale wanaotoka Engaruka na maeneo mengine yasiyo na mawaziliano wanalia na mbunge wao kuwa,ana visasi na ubabe.Walimwomba ashughulikie suala la minara ya simu .Jamaa akawaaambia voda,wakasema wametumia airtel,na tigo na hivo kuomba nao wawekwe.Mbunge wao akaja juu na kuwaambia km ni hivyo wasahau.Hadi leo wanalia kuwa ndicho anachowaadhibu nacho.Wanauliza anatakaje urais kwa style hii?

Matatizo mengine yanayoliliwa ni haya:

-Monduli hakuna mahakama, watu wanawekwa ktk magodown mara wanapokamatwa.
-monduli hakuna hata mahakama za mwanzo.
-Monduli hakuna zahanati nje ya pale mjini na hakuna hata mpango wa kuweka hata ya chini ya mil 4 tuu.
-Monduli hakuna vituo vya polisi zaidi ya vya mkoloni.
-Polisi hawana nyumba na waliopata hifadhi ni nyumbaya national house iliyochoka na hivyo polisi kugawana kwa pazia.Hao ndio polisi wanamfanyia kazi huyu mbunge.
-Raia wa monduli wanalia na mikopo wanayopewa na mbunge na kuwafanya watumwa baada ya kutolipika.
-Raia wanalia kuwa hela za halmashauri mbunge wao anazichukua km zake na kuzifanyia kazi za kumuandalia urais.
-Monduli haikuwa na shule hadi ujio wa shule za kata, na kwa shehemu kubwa mashirika ya misaada.
-Monduli ina barabara mbaya sana nje ya ile ya lami kufikia makao makuu.
-Monduli wanashangaa hawana makanisa na wanashangaa kusikia mbunge wao ana harambee ktk makanisa mengine kubwa tuu.

-wanashangaa mbunge wao hata Arusha mjini hakuna kanisa lenye hadhi ya mbwembwe zake.

Kuna mengi sana watu wanalia na monduli,huku wakijaribu tuhakikishia wasikilizaji kuwa Kambi ya Jeshi, mabaki ya mkoloni, mashirika ya dini etc ..ndio yaliyofanya haya yanayoonekana sasa Monduli.
Watu wanafunguka na wanafunguka vibaya.Wanasema wanachukia sana dhiki waliyo nayo huku,mbunge wao akionyesha uwezo w akufanya harambee kubwa kila mahali ila si jimboni kwake,ambao harambee moja ingeokoa uhai na shida kubwa sana kwa raia.

Source: wapiga kura niliowahoji ,na kuhakikishiwa na waliofika sehemu mbalimbali za jimbo hilo.

Mkuu ww ni mkongwe sana katika hii jukwaa! inakuwaje unakuja na story isiyokuwa na reliable sources? kama uliwahoji weka ushahidi na vielelezo!! U have been with us since 2006 as GT
 
Jamani unatumika kama.condom unakubali? Mimi nimefika monduli karibuni huo.ujinga unao.post haupo.monduli,Monduli ni wilaya ya mfano tz kwa hatua.kubwa za kimaendeleo,ukisosa cha.maana cha.kuandika.siyo.lazima upost
 
Kwanza tuwe na busara katika majimbo yaliyoakisi maendeleo haraka ni pamoja na Monduli.tatizo hatufanyi tafiti kuna jengwa hospitali ya kisasa,barabara zimejengwe, maji yapo na yametokea mbali arumeru magharibi, shule zipo kila kata tens zina mazingira bora na sio bora mazingira.Tusimhukumu mtu kwa sababu tu za kihafidhina.pia imani zetu zinasema kutoa ni moyo si utajiri.mleta hoja arudi afanye utafiti na si kuleta hoja hojaji hapa.
 
Chakujiuliza, nimiongoni mwa miji mikongwe Tanzania, kwani ulianzinshwa tarehe na siku moja na mji wa nairobi, check sasa hali ilivyo, mwenye macho haambiwi tizama
 
hahaa mkuu Korto monduli ilianzishwa na Nairobi na Mbulu. Monduli hapajawa kama Nairobi kwa sababu ya kijografia hapa gari kubwa linalokuja hapa ni chakito kwa sasa na wilaya hii ni kubwa ilikuwa hadi longido ipo Monduli kwa hiyo kwenye tamthimini yako uangalie hayo pia ....halafu Tanzania ni wilaya gani inalingana na Nairobi?
 
Mleta mada acha uongo mimi kwetu ni monduli,nimezaliwa huko,nimesoma huko ,na nyumbani kwetu ni sinoni monduli ,hakuna hizo shida ulizoziandika hapo ,monduli imepiga hatua katika wabunge,waliofanya vizuri jimboni kwake ni mbunge wetu ,ukiachilia mbali mambo ya kisiasa ,tunajivunia mbunge wetu,na mji wetu,tuulize sisi monduli ulikuwa unaenda kutafuta maji asubuhi unarudi usiku saa 4 na ndoo moja ya maji leo, maji yapo ,huko unakokusemea kunachimbwa kisima kikubvwa kabisa cha maji na ushaidi upo,jamani penye ukweli ni lazima tuseme ukweli tuu.ya ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe.
 
tunakushukuru sana kamanda kwa kuwa kuitupia macho hiyo jamii ya kipekee kabisa , ninao ujumbe kwao kwamba , MISHIKAKI NA ZILE POMBE ZA ASILI Walizohongwa wakati wa uchaguzi si kitu mbele ya umasikini wa milele .
 
mleta mada acha uongo mimi kwetu ni monduli,nimezaliwa huko,nimesoma huko ,na nyumbani kwetu ni sinoni monduli ,hakuna hizo shida ulizoziandika hapo ,monduli imepiga hatua katika wabunge,waliofanya vizuri jimboni kwake ni mbunge wetu ,ukiachilia mbali mambo ya kisiasa ,tunajivunia mbunge wetu,na mji wetu,tuulize sisi monduli ulikuwa unaenda kutafuta maji asubuhi unarudi usiku saa 4 na ndoo moja ya maji leo, maji yapo ,huko unakokusemea kunachimbwa kisima kikubvwa kabisa cha maji na ushaidi upo,jamani penye ukweli ni lazima tuseme ukweli tuu.ya ngoswe tumuachie ngoswe mwenyewe.

miaka yote hiyo , kisima kinachimbwa leo ? Kumbe hata hakijaisha ? Sasa unachobisha nini ?
 
Haaahah tuachieni Monduli yetu jamani tunaifurahia mambo yetu tutayasolve tu hata kama ni mdogo mdogo. cha muhimu tajeni wilaya zenu na mliyofanyiwa na wabunge wenu halafu mtuambie na nyie na Monduli yenu hamna hichi kipo kwetu ....labda tutajifunza kutoka kwenu.

Mi naona Tanzania wote tinahitaji kutoka tulipo na kufahamu vipaumbele tunavyotaka kama maendeleo kwa nchi yetu maana pana wilaya zipo hoi zaidi ya Monduli.
 
Mkuu ww ni mkongwe sana katika hii jukwaa! inakuwaje unakuja na story isiyokuwa na reliable sources? kama uliwahoji weka ushahidi na vielelezo!! U have been with us since 2006 as GT

Relibale source yako ni ipi kuliko wapiga kura wa sehemu zote?
 
Jamani unatumika kama.condom unakubali? Mimi nimefika monduli karibuni huo.ujinga unao.post haupo.monduli,Monduli ni wilaya ya mfano tz kwa hatua.kubwa za kimaendeleo,ukisosa cha.maana cha.kuandika.siyo.lazima upost

wewe unatumika km nini?

Mbona mpo wepesi sana hapa, ndio umejibu hoja gani?Monduli ina initiatives ambazo hata mbunge hajui za wafadhili, na mashirika y akigeni kusaidia sana..sijui ndizo mnataka mfunikia huyo boss wenu.

Si muda mrefu alitoka Mwana mfalme wa denmark kukagua miradi yao...ningefurahi km ungekuwa umefika engaruka.
 
Hamjui kwamba monduli is too small for el? ANAITAKA TANZANIA SIO MONDULI

km Monduli imemshinda ataiweza vipi Tanzania?Si huyu huyu aliumbuka Meru kwa masifa ya kijinga hadi CDM wakawauliza watu km aliwapenda Meru mbona hawana maji ,na maji yote kayapeleka Monduli Jeshini km nyingi sana.
 
miaka yote hiyo , kisima kinachimbwa leo ? Kumbe hata hakijaisha ? Sasa unachobisha nini ?

HIi thread imemshika pabaya sana huyo mbunge aliyekuwa akipita bila kupingwa..Uchaguzi wa Makuyuni ulimwaibisha sana akatumia nguvu nyingi sana kufunika moshi, hajui alikuwa kaitengeneza mkaa unawaka zaidi.

Tunachojadili hapa ni moto unawaka baad aya moshi kufunikwa sana....waliokuwa wanasema haya ni wazee wenye heshima zao wa kimasai ....wana hasira sana na very soon watasimama against him kabla ya NEC ili kutafuta nafasi ya uraia.

Hii Thread ikisurvive itakuwa ni ushahidi wa kitu ambacho walijidanganya sana.
 
Back
Top Bottom