Waone SIDO au VETA,machine zao ni mkataba.Habari wana JF nataka machine ya kukamua mafuta ya alizeti for small scale industry nasikia mashine nzuri zinatoka india sababu zina uwezo wa kukamua mafuta kwa 100% je kuna watu wanaziuza hapa nchini?au km ntapata link ya hiyo co ya india!nimejaribu link ya china alibaba but cjui km ni trusted site ya kuagiza na cn uhakika na quality ya mashine zao.
....Je mashine za kukamulia mafuta ya alizeti zinapatikana wapi hapa nchini? Au ni mpaka kuagiza nje ya nchi? Na zinahitajika shilingi ngapi ili kununu mashine moja?
Mimi nina shamba pia ambalo nina mpango wa kuanza kulima alizeti hizi karibuni. Najua soko la mafuta ya alizeti lipo kote kwenye ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na kati!
Kama unataka za india nenda india street utapata.Lakini kwa uzoefu wangu za kichina naona ndo nzuri zaidi kuanzia no 95 na 118.Nilizozifanyia uchinguzi nimegundua za kichina ziko poa kuliko za india
Ericus kilimo kwanza siku hizi mpango mzima ngoja nami niwacheck hao troika
Kuwa Mzalendo na Mpenda vitu vya ndani ya nchi yako waone VETA, SIDO au SUMA JKT uchangie kukuwa kwa viwanda vya ndani.
Hata nami ninasikitika ninaposikia watu wana-promote vitu vya nje ndani ya nchi yetu, yaani tunawasaidia hadi marketing. Hata kama vya kwetu havina ubora unaokidhi, tunaponunua na kutumia inakuwa ndio njia pekee ya kugundua madhaifu na kuwapa fursa watenegenezaji wa kuboresha mashine hizo, TUPENDE BIDHAA ZA KWETU, hata hawa tunaowaona mashine zao zina ubora hawakuanza na ubora.
Mende0,
Hilo halina ubishi wala halihitaji maelezo.
Wajua kwa upande wa Alizeti na Mafuta, Tanzania tunazalisha 40% tu ya mahitaji yetu ambayo ni sawa na 35,000MT. Hii haitoshi hata mahitaji yetu ya miezi miwili! Kwa mwezi Tanzania tunatumia 18,000MT na ili kufidia mahitaji tunaagiza zaidi ya 200,000MT kwa mwaka!
Mafuta ya kula kwa miongo mingi yamechukua nafasi ya pili katika vitu vinavyoongeza nakisi ya fedha za kigeni Tanzania. Kama tukijidhatiti kwenye hili zao si kama tutaweza kuzalisha ajira, kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja tu, bali tutapunguza nakisi (Deficit) ya mizania ya malipo (BoP-Balance of Payments) na kuongeza fedha za kigeni kwani hata sasa huwezi amini; kwenye hizo 40% tunazozalisha, double refined oil yote inakwenda Holland. Hii ni kuonyesha uzuri wa mafuta yetu na mahitaji katika ulimwengu.
Kama kweli una nia kwenye hii sekta tuzidi kuwasiliana