Wapi nitapata ngao ya kidonge?

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
5,524
17,058
Mimi sipendi kulala ndani ya neti. Usiku wa leo nimeumwa na mbu kupita maelezo. Hii imenifanya niikumbuke dawa ya ngao ambayo ilikua inatumika siku za nyuma. Ukweli ni kwamba, kwa uzoefu wangu ngao ya kidonge ile orijino kabla hawajatoa ngao ya maji ilikua ni kiboko sio tu kwa mbu bali kwa wadudu wote wanaoruka na wanao tambaa.

Nakumbuka mara ya kwanza kuitumia nilimaliza takribani miezi minne sijaona mdudu wa aina yoyote chumbani!Watu ilifikia mahali tukawa tunaichanganya na maji kisha una pulizia ukutani, kwenye mapazia n.k na wadudu wote wanatoweka! Ipo wapi dawa hii? Kwanini siku hizi haipatikani? Kuna anaejua dawa nyingine kama ile inayoweza kufukuza mbu na wadudu wengine chumbani?

Asanteni
 
Back
Top Bottom