Wapi nitapata best Video graphic adapter kwa ajili ya modern PC?

Ni
Nimekitumia picha mkuu
 
Poa mkuu yenyewe ile core i7 ya hp sema naweza nunua dizaini ingine kali zaidi kwa gpu nishauri tu maana naweza ieka ikawa soecific kwa games
 
Afu games hizi za unreal engine technology zilizotengenezwa na microsoft naona zina sumbua kwenye ile gpu ya nvidea gt 630
 
Afu games hizi za unreal engine technology zilizotengenezwa na microsoft naona zina sumbua kwenye ile gpu ya nvidea gt 630
mkuu utofauti wa 1650 na 630 ni mbingu na ardhi. 630 inapitwa zaidi ya mara 10 nguvu yake.
 
Haupendi mademu? Unakula godoro?
 
Kwani mbona niliona kama gtx 1650 inasapoti 4k pia chief?
 
Kwani mbona niliona kama gtx 1650 inasapoti 4k pia chief?
Inasupport ndio mkuu, hata kimeo changu Gt 1030 kinasupport 4k, sema natumia tu kuangalizia video na game ndogo sana. Games kwa 4k ni demanding sana compare na kuangalizia video ama content nyengine za 4k.

kwenye competitive games kwa 4k inabidi upate top end kama Rtx 2080 tena wengine wanaweka 2 kwa mpigo.

Mfano angalia benchmarks hapa
https://www.notebookcheck.net/NVIDIA-GeForce-GTX-1650-Desktop-GPU-Benchmarks-and-Specs.421420.0.html

Kwa games nyepesi kama fifa unapata hadi 80fps kwa 4k, ila games heavy kama just cause 4, battlefield v, division 3 etc fps hazifiki hata 20.
 
Duuh rtx 2080 mbili kwa mpigo si mchezo😀

Unatumia monitor au TV kuangalia hizo video za 4K?
 
Duuh rtx 2080 mbili kwa mpigo si mchezo😀

Unatumia monitor au TV kuangalia hizo video za 4K?
TV, monitor yangu ni 1080p. tv yenyewe ni clips tu za hapa na pale, internet 20mbps na 4k inataka angalau 25mbps inabidi udownload kwanza then uangalie baadae.
 
TV, monitor yangu ni 1080p. tv yenyewe ni clips tu za hapa na pale, internet 20mbps na 4k inataka angalau 25mbps inabidi udownload kwanza then uangalie baadae.
Kwa huku kwetu naonaga mambo ya 4k ni magumu video ya nyimbo ya dakk 3-4 nilishangaa unakuta ina mb 500-700+, sasa movie si itakuwa na gb 10+😀

Nilitamani niushuhudie video au games la 4k linavyokuwa quality ya picha.
 
mkuu unafikiri kwanini games za ps3 zina gb 8 na game hio hio kwenye pc ina gb 50 ama 60? sababu kwenye pc unadownload texture zote za hd, full hd, 4k etc hivyo kuna uwezekano mkubwa game hio hio uliodownload ukiweka gpu kali ukacheza 4k.

na kwenye 4k mkuu kitu kikubwa kabisa ni HDR10, ambayo inafanya nyeusi iwe tii, nyeupe iwe pee na kila rangi ipop out. hivyo ukipata right display utofauti ni mkubwa sana.

kwenye movie ndio movie zake ni kubwa sana na cd za bluray zinakuwa humo humo kwenye gb 50, kwa codecs za sasa x265 inaweza kupunguzika hadi around 10gb, sema kuna codecs mpya za Av1 na nyengine fvc pengine by 2021 zitakuwa tayari hizi zitapunguza zaidi ukubwa. ukumbuke dvd ni 4.7gb na quality yake ni 480p, siku hizi unapata movie ama episode ya 480p hadi mb200 hivyo usishangae miaka ijayo 4k movie ikawa gb 2 ama 3
 
Asante sana mkuu, umefafanua vyema sana.
 
asa chief,
mbona ujaweka anunue aina gani ya card, ili iwe best kwake.
na sisi wapenzi watazamaji
 
asa chief,
mbona ujaweka anunue aina gani ya card, ili iwe best kwake.
na sisi wapenzi watazamaji
Page ya kwanza kumezungumziwa aina za graphics card.

Na kutegemea na matumizi, aina ya power supply, urefu/upana wa pc yako ndio unachagua gpu. Bila kujua hivyo vitu ngumu kupata gpu inayokufaa.
 
Page ya kwanza kumezungumziwa aina za graphics card.

Na kutegemea na matumizi, aina ya power supply, urefu/upana wa pc yako ndio unachagua gpu. Bila kujua hivyo vitu ngumu kupata gpu inayokufaa.
Mkuu nini maana ya bottleneck nimeicheck google wanasema cpu lazima iendane na gpu otherwise kutakuwa na bottleneck
 
Mkuu nini maana ya bottleneck nimeicheck google wanasema cpu lazima iendane na gpu otherwise kutakuwa na bottleneck
Bottleneck inatokea either kwa cpu ama gpu na ni ile hali ya cpu ama gpu kuwa slow kuliko mwenzake na kusababisha hata kile unachorun kuwa slow.

1. Mfano kwa gpu, una gpu kali Rtx 2080 inaweza kurun kila game duniani, lakini cpu yako ni core 2 duo, hivyo unaporun game la kisasa unapata fps 10 ama 20, hapa tayari kuna bottleneck sababu gpu ya kisasa kama hii kwanini ipate fps hizi?

2. Same kwa cpu unaweza kuwa na cpu kali kama i9 10900k lakini gpu yako ni ya enzi Hizo Nvidia Gt 210 hivyo japo cpu ni nzuri sana tegemea itoe perfomance mbaya.

Ndio maana wanapofanya benchmark za gpu wanatumia cpu yenye nguvu sana na wanapo benchmark cpu wanashusha games resolution ili kupata nguvu zao halisi.

Kwa machine yako i7 2700/2600 na monitor zetu hizi sidhani kama utapata bottleneck kwa gpu yoyote ile ya consumer ya kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…