Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,374
- 38,248
SOMO WAPI NAKOSEA?
Hapa namzungumzia baba ambaye aliyakimbia majukumu ya kifamilia si kwa vile hakuwa na kipato, laa hasha, alikuwa financially powerful, mtu na ajira yake, mtu na pesa zake! Alikuwa mmoja watu wenye nyadhifa ktk taasisi aliofanyia kazi! Aliishi maisha ya anasa na starehe, wanasema alikuwa mzuri katika anasa za dunia, wapenda anasa wanasema alikuwa mtu mwema sana! Haya yamesemwa na watu wake wa karibu, ndg na jamaa zake waliokuwa nae, akiwemo dadake! Mpaka naandika uzi huu, sijawai kujua nini kilimuachanisha na mamangu mpendwa (rip) na bahati nzuri pia sikuwai kuwa na haja ya kujua sababu!
Maisha ya wakati wa utoto yalikuwa magumu sana, mama hakuwa na uwezo wa kumudu gharama za maisha kwa familia yake kwa kiwango chote, alijitahidi kadri ya uwezo wake kuzimaliza changamoto zetu, na tulimshukuru mungu kwa kile kidogo alichotupatia (rip my hero mama). Pia tulimshukuru mungu kuwa na mama huyu! Bahati iliyopo ni kwamba tulikuwa na uwezo darasani, mimi na kakangu na bahati ikaja tukafaulu la 7 kwenda sekondari! Haya yanatokea baba hajulikani yu wapi! Hajui watoto tu wapi!
Mama aliugua, na 12[SUP]th[/SUP] April 1996 my mama gone to glory [rip mama]. From here, the situation became worse than before! things turned upside down to my side! Na mwishoni mwa mwaka huo ndio kwa mara ya kwanza nakutanishwa na baba, I was 18 yrs old! Naikumbuka ile conversation: Tukiwa mezani tunakula, shangazi anamuuliza baba, huyu kijana hapa unamjua? (mm na baba tukiwa tunatizamana mezani). Baba anamjibu hapana! [akilini baba alihisi dadake kapata new shamba boy] then anaambiwa huyu ni ********! Baba anashtuka! Taharuki! Ananiuliza: ninyi mpo wawili, wewe ndio mkubwa ama mdogo? [wanaume wenzangu hata kama hawa kinamama wana matatizo yao, tusifikie hatua hii] Halafu akaniuliza kuhusu mama, nikamjibu tumemzika mwaka huu! Taharuki! Shangazi anadakia mazungumzo yetu, anamuelezea kwa niaba yangu kuhusu msiba huo, nilishaanza kulia! Shangazi alibahatika kuhudhuria mazishi ya mama.
Nayakumbuka sana maisha yangu ya sekondari, maisha ya mtaa yalinifundisha kitu more or less similar to what I learnt in school system. Nilipokuwa kidato cha pili tayari nilishajua namna ya kufanya biashara za kimachinga tena za aina mbali mbali ktk jiji la DSM (nikienda DSM wakati wa likizo) nyakati ambazo wenzangu wanahaha kubadili tuition 1 baada ya nyingine kutafuta walimu wazuri!
Mpaka nafika Form 4 nilishajua kuuza misokoto, nilishamjua pusha, nilishajua nini maana ya booster! Nilishakuwa na uhusiano wa karibu na mateja! Najua bidhaa yao inapatikanaje pale mkoani kwetu! Nilishajua namna gani DSM mzigo unaingia! Kwa nini nisijue wakati walionifadhili maisha yangu ya mtaani na shuleni, hizo zilikuwa shughuli zao za kila siku! Katika njia hii nilimpoteza my only lovely brother (rip brother). Pengine kukosa muongozo kulichangia, na pia labda iliandikwa iwe ikawa! Thanks lord I had never used such a stuff! Wana-JF mnajua madhara ya mtoto wa rika la sekondari kukosa muongozo wa maisha, kukosa mtu wa kumsimamia kwa karibu! Kumuacha mtoto wa umri huu afanye anachoweza! Hayo maisha niliyapitia!
To cut the story short! Nilifanikiwa kumaliza A level, nikafanya undergraduate, then nikafanya postgraduate udsm. Nina ajira yangu ya serikali! A good loving wife ambae nilikutana nae kipindi cha dhiki iliopitiliza (kama unasoma huu uzi, jua nakupenda sana, una maana kubwa sana kwangu). Tumebahatika kupata 2 baby girls! Mkubwa anasoma shule nzuri, mdogo is only 1.5 yrs old.
Turudi kwa baba. Yupo ktk maisha yake ya uzee. Vijana wanasema amefulia! Amebaki kuwa ni mkulima wa hapa na pale. Sasa hv anapigania afya yake hospitalini, anaumwa huko aliko. Namhudumia na kumpa msaada [tigopesa, mpesa zinahusika hapa] kadri ninavoona naweza. Watu wake wa karibu (wengi wao nawaskia kwa majina tu mf. Baba mdg, baba mkbw n.k) wananilaumu kuwa sijajitolea kiwango cha kutosha! Sijajitolea kama mtoto anavojitolea kwa mzazi wake! Wanasema sina mapenzi na baba. Mimi najua mapenzi ni natural, an inborn attitude, huwezi ambiwa PENDA na wewe UKAPENDA! Kweli sina mapenzi nae, lakini nambieni naanzia wapi kumpenda baba? Naendelea kupokea lawama! Unaesoma uzi huu, naomba nasaha zako, hapa mimi nakosea wapi? Pia zingatia kuwa mimi ni mwanadamu, kama ambavyo yeye pia! Siwezi kuvaa viatu vya kulipiza, ila haya ni maisha yangu na yeye ana maisha yake!