Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Mimi ni manusra wa ajali ya noah iliyotokea tarehe 18 asubuhi maeneo ya dakawa MOROGORO na kuchukuwa maisha ya watu 10 kati ya 13.Nina maumivu kwenye paji la uso,mataya ya meno na mbavu.Watu wananishauri nifanye CT scan ili nijue nimepata athari kiasi gani mwilini mwangu.Sasa kwa hapa moro sielewi nitapata wapi huduma hii na kwa gharama zipi.