Wapi bora zaidi kuoa, mjini au kijijini?

Tatizo siyo kuoa kijijini wala mjini bali ni nani unamuoa,utamaduni wake, imani yake, mahitaji yake, vipaumbele vyake, mtazamo wake katika mchezo kula na kulana na mwisho kabisa je,anakupenda na yuko tayari kuwa nawe katika mazingira yeyote ya kiuchumi in relation to your neighbours
 
Ongeza vigezo.
Waliosoma au la
Ukumbukwe kijijini kuna sekondari za kata vyuo viko mjini zaidi

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Apo kwenye elimu kwa upande wangu naona mambo mawili
1. Anaweza pata elimu na akatambua nafasi yake nakukuheshimu
2. Anaweza pata elimu akataka kulingana na wewe au kutaka kuwajuu zaidi (wanaleta ushindani)
 
Ok
 
Nimepitia thread zote mbili baada yakumalizi kupitia andiko lako nilichoelewa unachomaanisha katika kuamua jambo la kuowa kunahitaji umakini na kuchunguza kabla ya kuamua
 
Elimu,kazi yake,kabila lake,rangi yake,umbo lake,anapotoka si vitu vya msingi.
Oa au olewa na mtu unayempenda kwa dhati.
Hiyo ndiyo kanuni ya msingi na kuu.
Kumpenda mtu tuu haitoshi kukuhakikishia usalama wako
Kumpenda mtu hakudhibiti tamaa au hisia zake kuona na kutamani pengine
Sifa ulizojaribu kuziweka apo zinazingatiwa sana kabla mtu hajaamua kuanzisha tuu mahusiano yakimapenzi na mtu kunanguvu zakihisia zinajijenga kati yenu unafika maali unajuta kwanini ulianzisha mahusiaono nae mnaachana ila inafika maali zile nguvu za kihisia zinakushinda unakuta unarudiana nae
Kuowa unatoka mafichoni unadhirisha na mnafungwa kiimani kwamba ninyi nikitu kimoja alafu ndugu yangu uniambie nipende kwa dhati bila kuangalia mengine??
 
Kuna ya P mawenge yeye hakuowa alikuwa ni dada wakazi na mkeka ulichanika binti alivyopewa simu
 
Tatizo sio sehemu unapoenda kuoa tatizo unaishi wapi kama dar au mikoa iliyochangamka atabadilika tu akikutana na mashost wakware.
Ndiyo marafiki wanabadilisha sana watu na tena mwanamke ni rahisi kushawishika kwaiyo kama utakuwa kwenye eneo unalozungukwa na watu wengi ni wewe tuu kuweka mipaka na kuelimishana uko ndani
 
Popote unaweza vuna siyo inategemea mazao yalitunzwaje kutoa chakula bora
 
Aisee huyu jamaa apone kwa kweli

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
katika kuamua jambo la kuowa kunahitaji umakini na kuchunguza kabla ya kuamua
Sahihi, Ni muhimu sana.

Maisha ya amani na furaha, ya baadae katika familia yako yatategemea MAAMUZI utakayofanya wakati wa kuchagua mke.
 
Oa mwanamke anayekupenda na anayejielewa na kujitambua mwenye hofu ya mungu ana aliye anayeheshimu maagano

Haijalishi katoka mjini au kijijini


La sivyo utaolea wenzio(bila kujali alipotoka)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…