Inategemea na mazingira na mtu mwenyeweHabari zenu wanajamvi
Tushirikishane mada hii nawakaribisha kuchangia kile unachoona ni sawa
Jee wewe kama kijana unatakiwa kuchagua moja kati ya mawili unapotafuta binti wa kumuoa, jee utachagua lipi na kwanini?
1. Kumuoa binti anayetoka kijijini (hajayajua mengi na hana mambo mengi )
2. Kumuoa binti mliyekutana mjini (ameshayajua mengi na hakuna asichokijua)
Karibuni
Tabia na mwenendo wa binti husika, haijalishi ni wa kijijini au wa mjini.1. Kumuoa binti anayetoka kijijini (hajayajua mengi na hana mambo mengi )
2. Kumuoa binti mliyekutana mjini (ameshayajua mengi na hakuna asichokijua)
Hata kama anafanya biashara ya kujiuza sio??Oa mwanamke unayempenda.
Wewe unaweza kumpenda mwanamke anayejiuza?hili mbona ni suala dogo wala halihitaji uwe Dr kama Msukuma kulifahamu?siku hizi vijana mnasoma shule za aina gani?Hata kama anafanya biashara ya kujiuza sio??
Ila inategemea pia nakundi la marafiki atakao kutana nao mjini, rahisi sana mwanamke kubadilishwa na kundi la marafiki ila kama utamtunza inavyostaili nakumwonyesha anatakiwa kutembea vipi kwenye barabara mpya aliyokanyaga hatokuchafulia mezaAliyeona mengi ana uzoefu, hawezi kurubuniwa, huyo wa kijijini atakusumbua akisha yaona hayo mengi. Wanawake wengi wa mikoani wakija mjini wanakua malimbukeni, wanataka ku prove kitu au ku compensate ushamba wao kwa kufanya vitu ili waonekane wa mjini, wanakua wajuaji. Ushamba ni mzigo, unaweza ukamtoa mtu shamba lakini usitoe ushamba kichwani mwake.