Wapi Bora? Kuacha kazi Serikalini mshahara 900k na kuingia Private mshahara 3Mil Contract 4 years

Hizo ni risk factors ila bank kwenyewe growth ni ndogo ukiwa huna risk appetite.
Huyu ni wewe. Ila kuna ambaye aliacha kazi bank akakimbilia ng'o miezi kadhaa katika kazi mpya Fund zikasimama. Sponsors walibadili objectives akalipwa mishahara mitatu ya kuvunja mkataba yupo anapambana mara leo kilimo, kesho kujaribu kuexport furniture idea nzuri ila mtaji ni tatizo.
i
 
Halafu uniambie eti job security.

Eti ooh, serikalini kuna job security!!! Hio security wanayo wakina Makamba na Mwigulu ambao wana access na billions za dili na mishahara ya kufuru.


Mtu analipwa 5 figures salary tena ya madafu anajikuta una job security ya nyokwe 😂😂😂! Raha ya maisha vitu kama Mlimani City pawe kama kwenda kariakoo, unatembelea migahawa ya masaki kama unavyotembelea vijiwe vya kahawa bila presha hela iwe sio ya mawazo yani, sio unakula laki 5 kwa masaa machache unanunua Panadol umeze kuwa umefanya bad spending.
Ilimradi uwe unajituma. Hutakaa utoke huko. Unahama tu NGO
 
Wakuu, umofia kwenu!

Nimepata kazi kwenye Private - NGO ambayo take home ni 3Mil kwa mwezi. Nataka niache kazi serikalini ninakolipwa laki 9 ( Kabla ya Makato) kwa mwezi. Niko kada ya afya hapa Mbeya na umri wangu ni miaka 34.


Naombeni ushauri
Baki serikalini , huko private ni kazi ya muda ni kama tunda la msimu vile
 
Hizo ni risk factors ila bank kwenyewe growth ni ndogo ukiwa huna risk appetite.

i
Na ndo maana nikasema calc ni muhimu sana kabla ya kutake risk. Nafasi ya kutengeneza maisha hujirudia mara chache.

ONE WRONG MOVE INAWEZA KUCHUKUA MUDA SANA KUPATA HIYO NAFASI TENA.
 
N
Katika kazi uliyopo sasa ni lini unaweza fikia huo mshahara wa NGO?

Je, huko NGO ulipopata kazi, mkataba wake ni wa muda gani?

Je, kazi ya NGO inaonesha itakufanya ukue kiuzoefu?

Wakati mwingine unatafuta kazi fulani ili upate uzoefu wa kukupandisha zaidi...
Kinachotakiwa ni kujituma na kujenga networks. Ukifika mwaka wa 3 unaanza kuapply kwenye NGO kubwa zaidi, usisubiri mkatataba uishe ndio uanze kutafuta kazi. Ukipata kuzuri kabla mkataba haujaisha unasepa tu
 
N

Kinachotakiwa ni kujituma na kujenga networks. Ukifika mwaka wa 3 unaanza kuapply kwenye NGO kubwa zaidi, usisubiri mkatataba uishe ndio uanze kutafuta kazi. Ukipata kuzuri kabla mkataba haujaisha unasepa tu
Hata serikalini unatakiwa kujenga network. Nafasi ya kuwa na nafasi za juu zenye power ipo.
 
Simdanganyi, walioanza kazi serikalini mwaka 2019 hawana maisha ambayo kijana wangu alieanza kazi AMREF mwaka jana tu.

Mchizi tayari ana 40M imetulia bank kuna 20 inazunguka mtaani, braza mtu anasota na u lecturer Open university hana hata million 20 kwenye account mwaka wa 3 huu.

Achana na NGO, kuna meanz za kupiga hela nyingi unaweza ukawa unatengeneza hela nyingi nje ya mshahara kwa per diems
Achana kabisa na Amref🙌🏿
 
Wakuu, umofia kwenu!

Nimepata kazi kwenye Private - NGO ambayo take home ni 3Mil kwa mwezi. Nataka niache kazi serikalini ninakolipwa laki 9 ( Kabla ya Makato) kwa mwezi. Niko kada ya afya hapa Mbeya na umri wangu ni miaka 34.


Naombeni ushauri
Mkuu private security ni ndogo mno.
Usiangalie hizo figure...private ukipigwa jungu moja baasi unamrudia mkeo, baki njia kuu.

Huu ni ushauri tu maamuzi ni yako mkuu
 
Na kama nilivyosema kwenye maelezo yangu, baada ya hiyo miaka minne ya kujibana, atakuwa na mtaji wa kutosha sana tu.

Kujiajiri bila ya mtaji, ni sawa tu na kujiingiza kwenye michezo ya kamari aka kubet.
Ni kweli ila mtaji bila experience ni risk sana. Mtaji Unavyozidi kuwa mkubwa ndivyo unavyochelewa kuisha ila utaisha. Tatizo la private huna muda wa kutengeneza uzoefu wa biashara. Unaacha kazi na M200 bank ila huna uzoefu wa biashara. Salama yako inakuwa ni biashara ya nyumba za kupanga. Unless uwe na akili ya kufungua hicho ulichokuwa unakifanyia kazi.
 
Nenda na 2nd option !!! Acha uoga bali piga moyo konde na usonge mbele !! Na kwa uamuzi huo si ajabu ukajiona ulikuwa unafanya nini huko kwingine ambako ukikaa kwa kuwaza MAFAO (Maana hili nalo ni tatizo kwa wengi wa aina yako) utakosa golden opportunities !!
 
Back
Top Bottom