Waooooo ur back!!!!!karibu mwanakwetu
Subira yavuta heri shemeji......subira yavuta heri...naburudika na leo tenaaaaa....thanx gaijinOoh so nice to have you back AshaDii,
U can see, for yourself that apart from the love from me and maself and I, there is a 'plethora' of good samaritans here, with all good will and best wishes for you
"Oooh Rabbi, sinipe mapenzi" (Gaijin hebu do ze nidiful)
I am short of words hapa wajameni.
FF, vipi umemtayarishia nini mdogo wako leo (Vyangu ni vya chumbani zaidi)
My sunday iko poa upweke tu nimetulia ndani hata mapazia sijayanyanyua kama usiku vile....bora karudi naona malalamiko yatapungua....ewaaa umemwona bibie ee Gaga....salamu zangu sijui kama ulizifikisha lakini....how is ur sunday
Boss and Kaizer
pata mashairi kwanza ....audio will be with you shortly
Rabi sinipe mapenzi, hakuna wakuamini
Wapendwa wenye ujuzi, ni wachache duniyani
Pendo la kisikuhizi, kuhadaana nyoyoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.
Niwingi udanganyifu, kweli hakuna nyoyoni
Ambao wathibitifu, ni tabu kuwabaini
Kitu nnacho khofu, kuja vunjiwa thamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.
Wanaopenda wapende, mimi siye asilani
Nimejitowa upande, singii mwao kundini
Moyo nimepiga konde, siwezi kutamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.
Nimefunga moyo wangu, usinitie taabuni
Kuteswa na walimwengu, wasojuwa pendo ni nini
Haiwi fakhari kwangu, kujinasa mtegoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.
My sunday iko poa upweke tu nimetulia ndani hata mapazia sijayanyanyua kama usiku vile....bora karudi naona malalamiko yatapungua....
Una akili sana ndio maana ukawa my shem....hahahahaaaaaaakwa wale walalamishi wanaofikia kumfananisha na bibie FF......
Hapo bold, nimesoma kati kati ya mistari...
Hizi nyimbo za zamani wadada uzitumia sana kwenye kuboresha mahusiano yao ya kwenye ndoa, na wengine uzitumia kutongozea. ah ah ah ah ah!
Si unajuwa wakati mwingine kuna raha yake ukitongozwa na Mkeo au mume kumtongoza tena mke wake.
Leo mimi nina kazi moja tu: kuiba ujuzi.
Wataka tena zabiiibu , umekumbuka utamuuuuu ....halohalo hata kama umetubu kukupatena haramu........halooooooo nimeipenda hii
Ah ah ah mkuu, wazee wa zamani hawakukosea waliposema kuwa za kale dhahabu.Leo mimi nina kazi moja tu: kuiba ujuzi.
Alafu basi hizi nyimbo zote ninazo, wakati mwingine ushinda kutwa nikisikiliza.And this is special dedication to X-Paster
Wache waseme sina budi nawe,
si khofu lawama, sababu ya wewe
Ungekuwa nyoka, hadi uniume,
seuze tausi ,wache walalame
Ungekuwa nyoka, sumu yako dawa
Damu husafika, maradhi hupoa
Uzuri hakika, wewe umepewa
Siwezi kwepuka, liwe litokuwa
Nimefunga nia, katu sibadili,
Hapana hatia, kupenda jamali
sioni hatia, pasiwe suali
mimi meridhia, yeye mekubali
Gaijin nimetafuta hii Insha'Allah Tutaonana ya Sabaha Salum, sijaipata. Ilikuwa hiwe ndio dedication yako
Wewe basi nakupatia hii
Alinidhani bandia ndani ya mikono yake
Akichoka nichezea anache nifedheheke
Nami sikufikiria kama nitarudi kwake
Sitarudi abadan ni kheri niangamie
Lakini leo karudi, kama jambo halikuwa
Na macho yake shahidi, kuja kuniangukia
Kaja niomba nirudi, mapenzi kuyachukua
Kaja omba samahani, vipi nimkatalie ?
Na koja la asumini, kaniletea tamasha
Mapenzi ya utotoni, leo kaja yakumbusha
Yana mwenda mdomoni, ya furaha na bashasha
Kaja omba samahani, vipi nimkatalie?
Zikapita samahani, nyoyo tukazisafisha
Vifundo vilivyo ndani, vyote tukaviondosha
Raha iliyoje jamani, mapenzi kuyarudisha
Kaja omba samahani, vipi nimkatalie?