Boss and Kaizer
pata mashairi kwanza ....audio will be with you shortly
Rabi sinipe mapenzi, hakuna wakuamini
Wapendwa wenye ujuzi, ni wachache duniyani
Pendo la kisikuhizi, kuhadaana nyoyoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.
Niwingi udanganyifu, kweli hakuna nyoyoni
Ambao wathibitifu, ni tabu kuwabaini
Kitu nnacho khofu, kuja vunjiwa thamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.
Wanaopenda wapende, mimi siye asilani
Nimejitowa upande, singii mwao kundini
Moyo nimepiga konde, siwezi kutamani
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.
Nimefunga moyo wangu, usinitie taabuni
Kuteswa na walimwengu, wasojuwa pendo ni nini
Haiwi fakhari kwangu, kujinasa mtegoni
Mapenzi yamepotea, sasa ni adimu sana.