Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Huyu Kamanda alitusaidia sana kuiwajibisha Serikali yetu. Alitusaidia kuibua ajenda za kuipiga CCM kwenye mitandao ya kijamii. Alikuwa ni Jeshi la Mtu mmoja ambaye alijitolea kupambana na Serikali ili kunusuru chama chetu CHADEMA. Nilimuamini na nikajua tumepata mgomba Urais sahihi wa 2020.
Hata hivyo, ikiwa imepita mwezi mmoja baada ya uchaguzi wa TLS na baada ya kuanza kwa Bunge la Bajeti, makeke ya huyu Mwanasheria wetu ambaye ni Rais wa TLS yamepotea. Sijajua amepatwa na nini. Sijasikia pia akitoa tamko lolote kwa niaba ya Wana TLS kulaani tukio la kuuawa askari polisi 8 ambao ni wadau muhimu katika majukumu yao ya kila siku.
Ukimya wa Tundu Lissu hauleti afya njema kwa uhai wa chama chetu. Yeye ndiye mtu pekee aliyebaki wa kukipaisha chama chetu. Ukimya wake maana yake ni kwamba na yeye amezidiwa na utendaji wa Rais Magufuli na Serikali yake. Kama hajazidiwa basi ni vema ajitokeze na kutoa kauli zitakazotusaidia kuanzisha mijadala kwenye mitandao ya kijamii ili na sisi tuonekane tupo hai.